Waziri wa Masahuri ya Kigeni wa Marekani, John
Kerry, (Anaetoa hoja, kutoka kushoto) akiwa na wajumbe wa amani wa Israel na Palestina siku
zilizopita.
Marekani inasema imesikitishwa na makubaliano kati ya makundi
makuu Palestina ya kuiunda serikali ya Umoja.
Imeoya huenda hatua
hiyo ikatatiza zaidi jitihada za amani. Uamuzi huo unalijumuisha kundi lenye
msimamo kali za kidini, Hamas, unaliotawala eneo la Gaza na limetajwa na
Marekani na Israeli kama kundi la kigaidi.
Msemaji wa Wizara ya
Mashauri ya Kigeni wa Marekani Jen Psaki amesema wakati wa kutangaza uamuzi
hduo ndio unaotia wasiwasi.
Tangazo hilo
limefanywa wakati ambapo Marekani ilikuwa ikijitahidi kushawishi Israil na
Wapalestina kukubali kuendelea kufanya mashauriano ya amani ambayo hadi kufikia
sasa hayajazaa matunda yo yote.
Bi Psaki amesema
mapatano kati ya Wapalestina yatavuruga vibaya sana juhudi hizo na akatangaza
kuwa itakuwa vigumu kwa Israil kufanya mashauriano nakundi ambalo haliamini
kuwa Israili ina haki ya kuwepo kama taifa; jinsi wanavyoamini wanachama wa
Hamas, alisema Serikali ya Marekani itaendelea kuchunguza kwa makili hatua
zinazochukuliwa kuhusiana na uamuzi huo na Wapalestina siku na hata masaa
yanayokuja.
Wamarekani na mataifa washirika wake wamesisistiza kuwa muda
mrefu kuwa taifa lo lote la Wapalastina inapaswa kuwa lile linaloshutumua vita,
litambue Israil na kukubalia mapatano yote yanayohusisha taifa hilo la
Wayahudi.
Wapalestina wanasisitiza kuwa umoja wao
utampa uhalali zaidi Rais Mahmoud Abbas, kufanya mashauriano kwa niaba yao kwa
sababu atakuwa akiwakilisha Wapalestina wote na wala sio baadhi yao tu.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment