Morgan Tsvangirai.
Chama cha upinzani
nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha
kiongozi wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.
Taarifa hiyo imetolewa
na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika
katika mji Mkuu Harare.
Tangu mwaka 2009 hadi
2013 Bwana Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu
katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa sasa
Robert Mugabe.
Serikali ya Umoja wa
Kitaifa ilifikia kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda
kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa
madai ya udanganyifu.
Kushindwa kwake
kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais
Mugabe.
Waangalizi wanasema
ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.
Viongozi wengine wa
ngazi za juu wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya
jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment