Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 30 June 2016

TAASISI YA UTAWALA BORA NA DEMOKRASIA NCHINI TANZANIA YAWAKUTANISHA WADAU WA MAZINGIRA

Jimmy Luhende, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utawala Bora na Demokrasia nchini (ADLG), akizungumza katika Mjadala wa Mwezi June uliofanyika hii leo Jijini Mwanza. 

Taasisi ya ADLG huendesha mijadala tofauti tofauti kila mwisho wa mwezi ambapo wadau mbalimbali hukutana na kujadili mada husika. Mjada wa mwezi june umeangazia Fursa, changamoto na athari za kimazingira zitokanazo na shughuli za migodini.

RC MAKALA AAGIZA KUKAMATWA KWA MKANDARASI WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SONGWE BAADA YA KUSHINDWA KULIPA MAFAO YA VIBARUA ZAIDI YA 50

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla,akitolea ufafanuzi na kujibu kero mbalimbali zilizotolewa na wananchi wa Mkoa wa Mbeya, katika kikao maalum cha kupokea kero za wananchi kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mkapa, ambapo kubwa zaidi katika siku hii, Makala amesema serikali itahakikisha inamkamata mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe kutoka kampuni ya Kundan Sigh, baada ya kushindwa kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.


Na Emanuel Madafa, Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameagiza kukamatwa kwa  mmiliki wa kampuni ya Kundan Singh, ambaye alipewa tenda ya kujenga uwanja wa ndege wa Songwe, baada ya kushindwa  kulipa mafao ya vibarua zaidi ya 50.



Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya ametoa kauli hiyo , wakati akijibu na kutatua kero mbalimbali za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa kipindi kirefu, hali iliyochangia wananchi kuichukia serikali kwa madai ya kushindwa kuwatendea haki.

WAZIRI UMMY MWALIMU, MELINDA GATES WAYAPONGEZA MASHINDANO YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YANAYO ENDESHWA NA OXFAM TANZANIA

Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.

KONGAMANO LA KUBADILISHANA UZOEFU WA MAFUNZO YA TAALUMA UFARANSA NA TANZANIA LAFANYIKA DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak.(Picha na Modewjiblog)

KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda.

SERENGETI BOYS YAPAA, MCHAWI MWEUSI ATAMBA


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.

Wednesday 29 June 2016

HIKI NDICHO KIKOSI CHA TWIGA STARS MPYA

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Tanzania, Nasra Juma ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Twiga Stars.

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUTOA ELIMU YA KINGA NA TAHADHARI JIJINI DAR

Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Amani Hassan (kulia) akimuonyesha mwananchi aliyetembelea Banda la Maonyesho la jeshi hilo jinsi ya kutumia mtungi wa kuzimia moto wa awali, katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Kituo cha Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam.

BANDA YA MAHAKAMA LAVUTIA WENGI SABASABA

Mtendaji Mkuu wa Mahakama  Tanzania Bw. Hussein Kattanga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bi. Mary Shirima wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijin Dar es Salaam.

A TANZANIAN WINS HER MAJESTY THE QUEEN’S YOUNG LEADERS AWARD


By  Ayoub  Mzee-London
Her Majesty The Queen, Head of the Commonwealth, accompanied by Prince Harry, has hosted a special ceremony in the Ballroom at Buckingham Palace to present medals to the 60 winners of The Queen's Young Leaders Awards for 2016. 
Among them  was Rachel Nungu  from  Tanzania  a doctor and the national co-ordinator of a medical programme to help children who are born with clubfoot. The programme uses a non-surgical method called the Ponseti method to treat patients.

SMZ YAAHIDI KUENDELEZA MIPANGO YA UCHUMI INAYOCHAGIZWA KIMATAIFA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika Mkutano wa wadau wa sekta za maendeleo nchini wanaojadili utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) visiwani Zanzibar ambao umeandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na Tume ya Mipango Zanzibar chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuhakikisha mipango yote ya kimaendeleo inayochagizwa na malengo endelevu ya kimataifa inatekelezwa kwa vitendo ili wananchi waweze kunufaika.

TRA YAKUTANISHA WADAU KUJADILI UANZISHWAJI WA CHOMBO CHA KURATIBU, KUSIMAMIA WANATAALUMA WA KODI

Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi akitoa neno la ufunguzi katika kongamano lililoandaliwa na TRA na kukutanisha wadau mbalimbali wa kodi. (Picha zote na Rabi Hume - MO Blog)

TRA yakutanisha wadau wa kodi kujadili uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi
Katika kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya walipa kodi na wakusanyaji wa kodi, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imefanya kongamano la pamoja na wadau wa kodi nchini likiwa na lengo la kujadili kwa pamoja kuhusu uanzishwaji wa chombo cha kuratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Kamishna wa Sera na Bajeti kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Shogholo Msangi alisema wamekutanisha wadau hao wa kodi ili waweze kutoa maoni na kukubaliana kwa pamoja jinsi gani chombo hicho kitaweza kufanya kazi.

"Kutakuwa na chombo ambacho kitakuwa kinaratibu na kusimamia wanataaluma wa kodi na lengo ni kupitia kongamano hilo wadau wa kodi wataweza kukubaliana kwa pamoja kuona ni jinsi gani chombo hicho kitafanya kazi,

"Unaweza kukuta kuwa mlipa kodi kwa sasa ndiyo anaumia au TRA ndiyo inaumia lakini chombo hicho kitaweza kusimamia na kuweka kila jambo sehemu sahihi kama linavyotakiwa kuwapo," alisema Msangi.

Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo alisema kuwa chombo hicho kama kikianzishwa kitaweza kufanya kazi zake kwa uhuru bila kuingiliwa na TRA ili kuhakikisha kuwa kinatoa na haki kati ya mlipa kodi na wakusanyaji wa kodi (TRA) bila kuumiza upande wowote kwani jambo hilo linawahusu wote.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Kodi (ITA), Prof. Isaya Jairo akitoa neno la ukaribisho katika ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika Bagamoyo, Pwani.

Alisema kupitia kongamano hilo wamekutanisha wataalam wa kodi, wahasibu, walipa kodi, wanasheria, washauri wa kodi na walimu wa kodi kutoka vyuoni ili kuweza kupata maoni ya pamoja na kupata maoni ya makubaliano ya pande zote ambayo yatatumika katika kuendesha chombo hicho.

Na Rabi Hume - MO Blog)
Baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo la siku moja lililofanyika Bagamoyo, Pwani.






Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja (group one).
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja (group two).

DKT. NDUGULILE ATAKA MABUNGE KUSHIRIKISHWA KWENYE MPANGO WA “AFYA MOJA” (ONE HEALTH)

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile (Mb) (kulia), akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia.

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni (CCM) Dkt Faustine Ndugulile(Mb) ameyataka Mataifa kushirikisha Mabunge katika kufanikisha mpango wa Usalama wa Afya Duniani (Global Health Security Agenda).

Akizungumza kwenye mkutano wa masuala ya Usalama wa Afya ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kufanyika Jijini Bali, Indonesia,, Dkt Ndugulile alisema, “Mabunge yanaweza kutoa mchango mkubwa sana kwenye utekelezaji wa Mpango wa Usalama wa Afya Duniani kwa kusimamia Serikali na kuhakikisha hatua zote muhimu zinatekelezwa; kutunga Sheria zitakazosimamia utekelezaji wa mpango huu pamoja na kuhakikisha mpango huu unapata fedha za kutosha kutoka kwenye Bajeti ya Serikali”.

PBZ YAADHIMISHA MIAKA 50 KWA KUSAIDIA JAMII NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA KIDONGOCHEKUNDU


Wafanyakazi wa PBZ wakijumuika na Mkurugenzi Mtenda wa PBZ Ndg Juma Ameir katika kutoa huduma kwa wateja ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya PBZ tangu kuazishwa kwa benki hiyo wakiwa katika Tawi la Malindi Zanzibar. 

+AUDIO: SABABU ZA KUNDI LA MUZIKI LA PAYUS & MECRAS KUTOKA JIJINI MWANZA KUBADILI JINA.

Wakali wa wimbo wa Chausiku, Payus na Mecras kutoka Jijini Mwanza, ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Muziki la Payus & Pacras, wamebadili jina la kundi lao na sasa wanaitwa WAPANCRAS.

BENKI YA NMB YAZINDUA HUDUMA YA MALIPO YA VING'AMUZI VYA STAR TIMES


Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa (kushoto) na Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za malipo ya Star Times kupitia benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi. Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa (kushoto) na Meneja Huduma kwa Wateja wa Star Times, Gaspar Ngowi (kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za malipo ya Star Times kupitia benki ya NMB jijini Dar es Salaam. Sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi.

RC MAKONDA ATEMBELEA BANDA LA UN KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (katikati) alipotembea banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.

Tuesday 28 June 2016

THREE NEPTUNE HOTELS RAZED IN KWALE, OCCUPANTS EVACUATED

A fire razed three hotels, Village, Palm and Paradise beach hotels, on June 28, 2016 in Kwale County. No one was injured in the incident. PHOTO | FAROUK MWABEGE | NATION MEDIA GROUP 

By FAROUK MWABEGE
Three hotels belonging to Neptune Hotel and five cottages in Diani, Kwale County, have been razed to the ground by a heavy inferno on Tuesday evening.
According to the hotels resident manager Jackson Kifoto, the fire started at around 5:30 pm in one of the bungalows at the Palm Hotel, part of the connected chain of hotels.

TATIZO LA MIKOPO KWA WAFANYABIASHARA KUPATIWA UFUMBUZI


Na Immaculate Makilika- MAELEZO, tarehe 28/06/2016 Dar es salaam.

SERIKALI kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa mkakati ya kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa mikopo linalowakabili wafanyabiashara wengi nchini ili kusaidia uanzishwaji wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Afisa Biashara wa Wizara hiyo Bw. Baruti Mwaigaga wakati akizungumza katika Viwanja vya Mwl Nyerere wakati wa maonesho ya Sabasaba yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

WATEJA WA SIMBA CEMENT KUNUNUA SARUJI WA M-PESA

 Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi  Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga (TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja  kunua saruji kwa M PESA bila tozo yoyote  popote nchini.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA RAIS WA COMORO PAMOJA NA BALOZI WA JAPAN NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.

Wateja kutoka mitandao yote kufurahia huduma ya Tigo Pesa ndani ya Tanzania

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha kutoka Tigo, Ruan Swanepoel akiongea kuhusu uzinduzi wa kampeni mpya iitwayo NITIGOPESA, ambayo watumiaji wa huduma za kifedha kutoka mitandao mingine wanaweza kutuma na kupokea pesa kutoka kwa watumiaji wa TigoPesa kwa bei ile ile na wafanyabiashara wanaopokea malipo kwa njia ya Tigopesa sasa wanaweza wakalipwa na wateja wa mitandao mingine bila gharama za ziada, Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga.

Dar es Salaam Juni 28, 2016-Tigo Tanzania  imetangaza kwamba wateja kutoka mitandao yote  hivi sasa wanaweza  kutuma na kupokea  pesa kwa mteja yeyote wa Tigo nchini  kupitia huduma salama na ya uhakika ya Tigo Pesa.
 Hatua hiyo imetangazwa wakati wa  kuzindua kampeni mpya  inayojulikana, ‘NITIGOPESA’ ambayo lengo lake  kuu  ni kuhakikisha wateja kutoka mitandao yote mikubwa ya simu wanaweza kufanya  huduma zao za fedha kwa njia ya simu pamoja na wateja wa Tigo Pesa na wafanya biashara  nchini Tanzania.

RC MAKALLA AIOMBA BENKI KUU IFANYE UTAFITI KUHUSU UNUNUZI WA MAZAO YAKIWA SHAMBANI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makala (Katikati)akizungumza na viongozi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya,kulia Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya Jovent Rushaka na Meneja Utawala na fedha Bakali Ally kushoto katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano benki kuu ya Tanzania (BOT)tawi la Mbeya ,June 28 -2016.

WAKULIMA WADOGOWADOGO NA WADAU WA KILIMO WAKUTANA KUJADILI BAJETI YA KILIMO NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo  juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.

NYOTA 7 MBEYA CITY WAONYESHWA MLANGO WA KUTOKEA, HAWATAKUWEPO 2016/17

Kipa Hanningtony Kalyesubula

Orodha ya  wachezaji ambao  walikuwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc msimu uliopita  na mikataba yao kufikia tamati baada ya kumalizika kwa  ligi  kuu ya vodacom Tanzania bara  Mei 22  tayari  imetolewa  ikiwataja nyota saba kutokuwepo tena  kikosini  msimu ujao.
Muda mfupi uliopita, Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe amesema kuwa, wachezaji saba wanaotajwa kwenye orodha  hii ni wazi mikataba yao imemalizika na klabu haitafanya tena  mazungumzo yoyote  na tayari wamesha taarifiwa  juu ya hilo.

ZULMIRA ATAKA KAZI KWA PAMOJA KUHAMI MAENEO YA URITHI WA DUNIA

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akizungumza katika warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na shirika lake kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Marangu, mkoani Kilimanjaro.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues amewakumbusha wadau wa urithi wa dunia na maeneo ya hifadhi kufanyakazi kwa pamoja kwa lengo la kuhifadhi na kuyaendeleza maeneo hayo bila kuondoa ushiriki wa wananchi wanayozunguka.

Kauli hiyo ameitoa katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lake kwa wadau wa mazingira ya hifadhi na urithi wa dunia mjini Marangu Moshi, kufuatia makubaliano na serikali ya Tanzania.

MCHEZAJI BORA WA UMMISETA MUSA SAID KUONDOKA JUMATANO JUNI 28, 2016 KWENDA NCHINI UFARANSA

 Meneja Msaidizi wa Chapa ya Coca – Cola, Mariam Sezinga, akizungumza na waandishi wa habari kuwaelezea juu ya safari ya mchezaji Musa Said anayetarajia kuondoka Jumatano ya Juni 28, 2016 kwenda nchini Ufaransa kwenye kambi ya kimataifa ya Copa Coca-Cola. Pembeni ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja, Mchezaji Musa Said Bakari na Mwalimu wake wa Kibasila. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 

Na Devotha Kiwelo
MCHEZAJI bora wa mashindano ya UMMISETA yaliyofanyika mwaka jana mkoani Mwanza, Said Musa Jumatano ya Juni 28, 2016 kuelekea Ufaransa katika kambi ya Kimataifa ya Copa Coca - Cola ambayo imeandaliwa na kampuni ya kinywaji cha Coca - Cola . 
 Akizungumza jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja alisema udhamini wa kampuni ya Coca - Cola imetambua umuhimu wa michezo hivyo kukubali kudhamini michezo kupitia shule za sekondari ili kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi ambao wanamalengo makubwa katika kuitumikia nchini yao kupitia michezo. 

TAASISI YA NITETEE YAITAKA SERIKALI KUTOA RUZUKU KWA TAASISI ZINAZOFANYA KAZI VIZURI

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Nitetee, Flora Lauwo akipungia mkono alipokuwa akitambulishwa bungeni Dodoma.

KITUO CHA HUDUMA NA MTOTO EAGT LUMALA MPYA CHA JIJINI MWANZA CHAKABIDHI MSAADA KWA WATOTO WENYE UHITAJI

Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma na Mtoto EAGT Lumala Mpya, Jorum Samwel (kulia mwenye suti), akitoa ufafanuzi juu ya msaada wa vitanda, magodoro na vyakula uliotolewa na Kituo hicho ambacho kiko chini ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza.
Na BMG
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba katika Manispaa ya Ilemela mkaoni Mwanza, limekabidhi misaada ya vitu mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na vyakula kwa watoto wanaotoka katika familia duni ambao wanaolelewa na kanisa hilo.

KITWANGA AKABIDHI RASMI OFISI KWA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA, JIJINI DAR JANA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Sunday 26 June 2016

TFF YAIPIGA MKWARA MZITO YANGA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea taarifa juu ya mpango na kauli za baadhi ya viongozi wa Young Africans SC kushawishi mashabiki wao kufanya vurugu dhidi ya warushaji matangazo ya televisheni ya moja kwa moja wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika ngazi ya Makundi kati ya Young Africans ya Tanzania na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) utakaofanyika Juni 28, 2016 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Dar es Salaam.

Naibu Spika Dk. Tulia Aosha Magari ya Wabunge, Mawaziri kuwaunga mkono waandishi wa habari

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) akiosha moja ya magari ya wabunge na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Katika zoezi hilo Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alichangia shilingi milioni tano na Dk. Kigwangalla shilingi milioni moja.

KAMATI YA MASHINDANO NA USAJILI YA COASTAL UNION YAWEKA BAYANA MIKAKATI YAO


Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili  katika Klabu ya Coastal Union, Hemed Aurora akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kujadili masuala ya usajili na mashindano kilichoketijuzi kwenye ukumbi wa makao makuu ya klabu hiyo, kushoto ni mjumbe wa kamati hiyo, Abdallah Zuberi, kulia ni Hussein Chuse na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Klabu ya Coastal Union Salim Bawazir.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWATAKA WAISLAMU NCHINI KUDUMISHA AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  wakati wa tafrija ya Futari iliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waisalm wa Tanzania  (Bakwata) iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kinondoni Muslim ambapo alimuwakilisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli na kuwahimiza viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) waendelee kuombea amani katika Taifa na kukemea ipasavyo vitendo vya uhalifu katika jamii ya Kitanzania.

RAIS WA VoWET MAIDA WAZIRI AZINDUA UMOJA WA WANAFUNZI WA BIASHARA (BAA) ATOA SEMINA YA UJASIRIAMALI (TIA) DAR ES SALAAAM

Rais wa VoWET na Mkurugenzi Mtendaji wa IBRA Construction  Limited Bi. Maida Waziri akiongea na wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu  TIA wakati wa uzunduzi rasmi wa umoja wa wanafunzi wa Biashara (BAA), ambapo aliwahimiza elimu wanayoipata wasiitumie kwenda kuombea kazi tuu lakini pia waitumie kwa ajili ya kufanya ujasiliamali kwa kujiajili wao wenyewe.

Saturday 25 June 2016

SHELISHELI WAIHOFIA SERENGETI BOYS


Kocha Mkuu wa timu ya soka ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Shelisheli, Gavan Jeanne ameonesha kuihofia Serengeti Boys ya Tanzania katika mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa utakaofanyika Juni 26, 2016 kuanzia saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Jeanne alionesha hofu hiyo leo Juni 25, 2016 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na mbele ya Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime ambao kwa pamoja walikuwa wakmizungumzia namna walivyoandaa timu zao kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.

BENKI KUU TANZANIA TAWI LA MBEYA (BOT) YAFUTURISHA KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA KUANZISHWA KWA BENKI HIYO

Waumini wa dini ya kiislamu Mkoa wa Mbeya pamoja na wadau mbalimbali wakifuturu futali iliyoandaliwa na benki Kuu ya Tanzania (BOT)Tawi la Mbeya ambapo benki hiyo ipo katika kuadhimisha miaka ya hamsini ya kuanzishwa kwake.Picha E.Madafa na D. Nyembe.

Wageni waalikwa ,viongozi wa serikali na viongozi wa dini mbalimbali mkoani Mbeya  wakipita kupata  futari kwenye ukumbi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la Mbeya .

Mkurugenzi wa benki kuu Tanzania( BOT) tawi la mbeya  Jovenant Rushaka akiongoza kupata futari.


Wafanyakazi benki kuu Tanzania tawi la Mbeya wakipata futari

Wageni waalikwa Viongozi wa serikali na wadau mbalimbali  wakibadilishana mawazo pamoja na kupata futari iliyoandaliwa na benki kuu Tanzania(BOT) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwa benki hiyo.

wadau wakipata futari.