BENKI ya NMB Tanzania imeingia makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Star Times ambapo kwa sasa wateja wa Star Times wanaweza kulipia huduma hizo kwenye tawi lolote la Benki ya NMB au moja kwa moja kwa wajeta wa NMB waliojiunga na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi.
Ushirikiano huo umezinduliwa jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za Star Times, ambapo Kaimu Ofisa Mkuu wa Wateja Binafsi wa NMB, Boma Raballa alisema wateja wa NMB waliounganishwa na huduma za kibenki kwa simu za mkononi sasa watafanya malipo yao popote walipo na kwa urahisi, huku wateja wa Star Times ambao hawana akaunti na benki hiyo kuweza kulipia huduma katika tawi lolote la Benki ya NMB.
Alisema huduma hiyo licha ya kuwarahisishia kazi wateja itakuwa haina tozo kwa wateja wa NMB hivyo kuwataka wananchi na wateja wa Benki ya NMB waitumie ipasavyo.
Alisema hatua ya Benki ya NMB yenye zaidi ya wateja milioni mbili Tanzania huku ikiwa na matawi zaidi ya 176 itasogeza zaidi huduma za malipo ya ving'amuzi vya Star Times kwa wateja mbalimbali.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa NMB, Bwana Damien alisema wateja wa NMB na wengine wasio na akaunti watakapoitaji huduma ya malipo watatakiwa kubofya *150*66# na kuchagua huduma ya malipo ya Star Times na kuendelea kupata maelekezo rahisi katika kufanikisha malipo yao.
No comments:
Post a Comment