Picha ya mtandaoni
VIJANA wenzangu, natumaini mnaendelea
vyema na shughuli zenu za kila siku katika ujenzi wa taifa na jamii, au siyo?
Kama ni mwanafunzi, zingatia zaidi masomo, kama ni kibarua kama mimi, zingatia
wajibu wako kazini, kama ni mkulima kama wale ndugu zangu wa kule Kibaigwa,
wazingatie ushauri wa wataalamu kwa kupanda mbegu bora zinazostahimili ukame na
kutoa mazao mengi.
Leo nazungumzia mada inayosema ‘Kupoteza Bikra’. Mada hii imetokana na maswali mengi ambayo nimewahi kuyapata kutoka kwa wasomaji wangu, hususan wasichana, ambao wanasema; “Brother Danny, sijawahi kukutana na mwanamume, lakini siku niliyokutana naye, damu haikutoka. Hii imenipa wakati mgumu kwa mume wangu ambaye nilimwambia kwamba mimi ni bikra na sikuwa tayari kukutana naye mpaka tulipofunga ndoa, sasa anasema kwamba nilimdanganya. Tatizo ni nini?” Hili ni moja kati ya maswali mengi ninayoyapata.
Leo nazungumzia mada inayosema ‘Kupoteza Bikra’. Mada hii imetokana na maswali mengi ambayo nimewahi kuyapata kutoka kwa wasomaji wangu, hususan wasichana, ambao wanasema; “Brother Danny, sijawahi kukutana na mwanamume, lakini siku niliyokutana naye, damu haikutoka. Hii imenipa wakati mgumu kwa mume wangu ambaye nilimwambia kwamba mimi ni bikra na sikuwa tayari kukutana naye mpaka tulipofunga ndoa, sasa anasema kwamba nilimdanganya. Tatizo ni nini?” Hili ni moja kati ya maswali mengi ninayoyapata.
Kwanza kabla sijaendelea, ningependa
kufafanua bikira au mwanamwali ni nani, na ubikra ni nini. Bikira ni
mtu yeyote, msichana au mvulana, ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa hata mara moja. Kwa hiyo basi, ubikira ni hali ya mtu kutokutana kimwili na mtu wa jinsia nyingine. Nadhani hapo wasomaji wangu mnaweza kunielewa japo kwa ufupi.
mtu yeyote, msichana au mvulana, ambaye hajawahi kufanya tendo la ndoa hata mara moja. Kwa hiyo basi, ubikira ni hali ya mtu kutokutana kimwili na mtu wa jinsia nyingine. Nadhani hapo wasomaji wangu mnaweza kunielewa japo kwa ufupi.
Nini maana ya kupoteza bikira?
Hili ni swali zuri sana. Kama
nilivyosema hapo juu; wewe unakuwa bikira mpaka pale utakapokuwa umefanya tendo
la ndoa na mtu wa jinsia tofauti. Hata hivyo, tafsiri hii huwaacha watu wengi
wakiwa njia panda.
Wakati watunga sera kwingineko duniani
wanatafsiri ndoa kwa kueleza kwamba hata kufanya ngono na mtu wa jinsia yako
(kama mashoga na wasagaji) kunatoa bikira yako, labda ungekuwa wakati muafaka
wa kuangalia kwa undani nini maana ya bikira.
Wakati tunapozungumzia bikira,
tunafikiria kuhusu “ndoa haramu za Wazungu wanaopendelea ushoga na usagaji” ambao wanatafsiri ngono kama kigezo cha jinsia. Lakini ukweli ni
kwamba, tafsiri muafaka ya ubikira inakufanya uone kwamba kufanya vitendo mbalimbali vya ngono kungeweza
kukufanya ukajiita bikira wakati siyo kweli.
Kwa nadharia, chini ya tafsiri ya jadi
ya ubikira, mtu ambaye anajihusisha na vitendo vya ushoga (kwa mwanamume) na usagaji (kwa mwanamke) anaweza kufanya ngono kila siku na bado
akawa bikira. Mtu anayefanya mapenzi ya bila kujamiiana (oral sex) kila mara
pia ni bikira. Kuna ukweli wowote katika hili? Nadhani hapa kuna upungufu.
Tafsiri nzima ya ubikira kwa hakika
inahitaji kuandikwa upya. Labda kabla sijaendelea zaidi, wacha niwatoe shaka wale ambao hawajawahi kufanya mapenzi lakini siku ya siku
wakajiona kwamba hawana bikira.
Bikira inaweza kutoka kwa njia nyingi
zaidi ya kufanya mapenzi. Msichana anayeshiriki michezo mbalimbali anaweza
kuitoa bikira yake. Au kama anabeba mizigo mizito, au ana matatizo kwenye tumbo
la uzazi na wakati wa ‘period’ anatokwa na damu sana, na mambo mengine kadha wa
kadha yanayoweza kufafanuliwa kwa kina na wataalamu wa afya.
Ubikira ni hali ya kutokuingiliwa
kimaumbile, yaani kwa viungo vya uzazi vya kiume na vya kike, lakini inaweza ikawa na tofauti kwa namna fulani pia. Kama mvulana au hajawahi kufanya
mapenzi na mwanamke, lakini akawa anajichua, ama anafanya mapenzi kinyume cha
maumbile; awe basha au msenge, hakika hawezi kujiita bikira. Atajiita bikira
kinadharia tu, lakini kivitendo siyo bikira kwa sababu raha ama karaha ya tendo
la ndoa anaijua!
Kwa hiyo basi, kabla ya kueleza tafsiri
mpya, fikiria katika mambo haya yafuatayo na uyatafakari jinsi yanavyoweza
kusimama katika suala zima la ubikira.
* Mtu aliyebakwa au kutomaswa huwa siyo
bikira tena?
* Hivi ngono ndiyo njia pekee ya
kuangalia ubikira wa mtu?
* Kama utajihusisha na vitendo vingine
vya mahaba, lakini si vya kuingiliwa kimwili, ni busara kujiita wewe bikira?
* Utatafsiri vipi kupoteza bikra yako
kama wewe ulikuwa/au bado ni msagaji au shoga ama wa kawaida?
* Kuwa bikira kunaegemea kwenye hisia
zako, shughuli zako, au vyote kwa pamoja?
* Kuna jambo lolote la kihisia katika
kupoteza bikira yako, kwa maana kwamba kama utafanya mapenzi na mtu na
ukashindwa kuona dalili za bikira kutoka au tofauti yoyote?
Tafsiri mpya...
Tafsiri mpya...
Napendekeza kwamba ubikira una pande
mbili. Nadhani kuna ubikira wa kihisia na ubikira wa kimwili. Nadhani kama
kweli mtu anataka asiwe bikira anatakiwa kuachana na mambo yote ya kihisia
kuhusu ubikira na kujihusisha na vitendo vya ngono kimwili.
Katika tafsiri yangu hii, kitendo
chochote cha ngono kinachohusisha watu kuchojoa nguo na kusisimkwa mpaka kufikia
mshindo hata bila kuingiliana kimwili basi ni ngono. Nadhani kuwa uchi na
kusisimuana ni ‘hatua ambayo haina kurudi nyuma’, siyo kuingiliana kimwili.
Haijalishi kama kitendo hicho ni cha
mwanamke na mwanamume kwa asili au ni cha wanaume kwa wanaume (mabasha na
mashoga) au wanawake kwa wanawake (wasagaji), kama utashirikiana mwili wako na
mtu mwingine, au kama utampa raha ya kimahaba mtu mwingine mpaka akafikia mshindo
na kutoa manii au ukiwa na madhumuni atoe manii, basi umefanya ngono.
Pia nadhani kwamba ubikira siyo kitu
fulani ambacho ‘unapoteza’ au ‘kinachukuliwa’, bali kitu fulani ambacho
unashirikiana na mtu mwingine, mara moja tu katika maisha. Kama hukumpatia mtu
mwingine, basi utaendelea kujihesabu kama ni bikira.
Nadhani watu ambao wamebakwa au
kutomaswa bado wataendelea kuwa bikira katika hisia hata kama miili yao
imefanya mapenzi. Hawajakoma kuwa bikira, na wala hawajawahi kufurahia na
kuijua raha ya hisia za kimapenzi ambayo huenda sambamba na kuutoa mwili wako
kwa mahaba kwa mtu mwingine.
Kama bikira yako imetolewa na mtu
mwingine kwa mabavu, japokuwa ni kwa kufanya mapenzi kimwili, sidhani kama ni
busara kusema kwamba wewe si bikira tena. Bado utaendelea kujichukulia kana
kwamba hujawahi kufanya mapenzi, bado utaona ngono kama kitu kigeni kwako.
Kuwa mwathirika wa kubakwa hakuwezi
kukakulazimu uishi na alama ambayo hukuiomba au kuitaka. Ubikira siyo kitu
ambacho mtu anakipoteza kwa bahati mbaya, kutokuwa bikira ni jambo ambalo mtu
analichagua mwenyewe.
Mtu aliyebakwa na kwa bahati mbaya
akapata mimba, bado kwa fikra zake ataendelea kujiita bikira, na hilo linaweza lisiwe kosa kwake! Haijui raha ya mapenzi, hajui maana ya mapenzi,
mpaka pale atakapoamua mwenyewe kwa nafsi yake kwamba anahitaji kufanya mapenzi, ndipo anapoweza
kuamini akilini mwake kwamba si bikira tena!
Nini kinachokufanya uwe bikira?
Nimekwishaeleza tafsiri halisi za
ubikira. Lakini unapozungumza na watu kuhusu suala hili, unagundua kwamba kuna
mambo mengi yanayojitokeza katika ‘mapenzi kwa mara ya kwanza’ ambayo yana
umuhimu kimwili, kihisia, kiakili, na hata kisiasa.
Inaweza kuwa si rahisi kusema kwamba
ubikira siyo tafsiri rahisi kama tunavyosema sasa, hivyo ngoja tuangalie mambo machache ambayo yanaweza kusaidia katika uelewa wetu:
Tafsiri ya kale
Tafsiri inayojulikana zaidi ni kwamba
bikira ni mtu yeyote ambaye hajawahi kufanya mapenzi na mtu wa jinsia nyingine.
Hata tafsiri hii inaonekana kupwaya, kwani ukiangalia kwa undani utagundua
kwamba hili lilikuwa ni suala la kimwili zaidi, au la kitiba.
Mwanamke mwenye uke uliobana (intact
hymen) alikuwa anachukuliwa kwamba bado bikira, na huo ndio ulikuwa mwisho wa
mjadala. Wanawake katika zama za kati, kwa mfano, walikuwa wanachukuliwa kwamba
ni bikira kama walikuwa na uke unaobana. Kama mwanamke alikata ‘utepe’ (hymen)
wakati amepanda punda au kukimbia, alichukuliwa kwamba si bikira tena. Kama
mwanamke alizaliwa huku sehemu zake za siri zikiwa ndogo sana, alikuwa
anachukuliwa kama si bikira.
Ni muhimu pia kutambua kwamba bado kuna
tamaduni mpaka leo, kama watu wa Mashariki ya Kati, ambao bado wanashikilia
msimamo kama huu. Na kwa hakika, hakukuwepo na kipimo kwa wanaume.
Ubikira ni kitu ambacho kilikuwa na
nguvu zaidi kwa wanawake tu. Kulikuwa na tafsiri ndogo sana ya ubikira kwa
mwanamume, lakini umuhimu wa ubikira kwa mwanamke ulikuwa mkubwa zaidi. (Hulka
hii bado inaendelea mpaka leo, wakati ambapo ukweli ni kwamba neno hili linawahusu
wanaume na wanawake pia, lakini bado watu wanadhani kwamba ni ‘suala’ la
wanawake na ndio wanaopaswa kutunza bikira zao.)
Hili linaweza kuwa jambo geni kwetu,
lakini ni muhimu kuzingatia kwa nini ‘utepe’ (hymen) kwa mwanamke ulikuwa
unachukuliwa kwa umuhimu mkubwa – hii ilikuwa ni dalili tosha kwamba kama hakuwa
na hali hiyo basi ni wazi kwamba aliwahi kufanya mapenzi na mwanamume mwingine.
Mwanamke ambaye alikuwa ‘amekata utepe’ alikuwa hana thamani kwa sababu
ilionekana kama ni uzembe wake ndiyo maana ‘utepe’ ukakatika, kama alivyokuwa
mwanamke ambaye kiungo chake cha uzazi kilikuwa kidogo sana. Kwa maana hiyo,
bikira alikuwa mwanamke ambaye angeweza kuthibitishwa ubikira wake kimwili,
hakuwahi kupitishwa uume kwenye uke wake.
Na tena hakukuwa na kipimo kwa
mwanamume kuhusu suala hili. Kwahiyo kutafsiri ubikira siyo rahisi kama
tunavyoweza kufikiria sasa, na tafsiri imebadilika kutoka ile ya kale na sasa.
Jinsia nyingine?
Tafsiri ya sasa, inayowahusu wanaume na
wanawake, iko kama hivi: Kama umefanya ngono (kuingiliana kimwili), basi wewe
siyo bikira.
Fikiria kama kiungo cha kiume
hakijahusika hapo? Ina maana kwamba wasagaji wawili ambao hawajawahi kukutana
na mwanamume hata mara moja, lakini wamekuwa wakisagana pengine kwa miaka mingi
wanaweza kuwa bado bikira? Hata kama wana uzoefu wa masuala ya mahaba? Inaweza
kuwa hivyo, kutegemeana na tafsiri yako mwenyewe!
Lakini katika hili, huwezi kusema
kwamba wanawake hawa wawili bado bikira kwa sababu hawajawahi kukutana na
mwanamume ingawa wana uzoefu wa ngono. Kukutana kwao kwa mara ya kwanza na
kufanya mapenzi ya kusagana, wakajitosheleza wenyewe namna walivyojua, tayari
kuliwatoa bikira kwa sababu tangu dakika ile waliweza kutambua raha ya mapenzi.
Hisia zao zote zilikuwa kwenye ngono na kwa hakika waliweza hata kufikia
mshindo na wanaendelea kufanya hivyo. Tofauti yao pekee ni kule kutoingiliwa na
mwanamume tu.
Na vipi kuhusu kumwingilia mtu kinyume
na maumbile, yaani kwa mashoga? Mwanamume ambaye ni shoga na mwingine ambaye ni
‘basha’ ambao hawajawahi kufanya mapenzi na mwanamke wanaweza kuendelea kujiita
ni bikira kwa sababu tu wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile? Kitendo hicho
hakiwezi kuwa kimeipoteza bikira yao? Kuna baadhi ya tamaduni, ingawa si
nyingi, ambazo zinaruhusu mapenzi ya kinyume cha maumbile kwa mwanamke na
mwanamume ili tu kuilinda bikira ya mwanamke. Binti anaweza kuwa anampenda
mwanamume, lakini kwa kuwa mila zinamtaka akiolewa akutwe na bikira, anaridhia
kufanya mapenzi kinyume cha maumbile na mwanamume ampendaye ili ailinde bikira!
Unashangaa? Wenyewe wanajijua. Sasa kama kujamiiana kinyume na maumbile siyo
muafaka, vipi kwa wanaume kwa wanaume?
Tafsiri hii huwa ngumu zaidi kwa watu
ambao ni bisexual, yaani wanaoweza kufanya mapenzi na watu wa jinsia mbili tofauti. Je, huyu anaweza kuwa bado bikira kama atafanya mapenzi
na mtu wa jinsia yake na kisha kufanya mapenzi na mtu wa jinsia tofauti?
Hapa tena hakuna neno rahisi kwa suala
hili la kihisia, kama ubikira unatafsiriwa kwa mtu kuingiliana kimwili na mtu
wa jinsia tofauti. Na pamoja na ukweli kwamba mtu anaweza akafikiri kitu fulani
na kukielezea vizuri, kile ambacho kinathaminiwa na mila huonekana ndicho
muhimu zaidi.
Mtu aliyebakwa
Dhana halisi ya bikira ni mtu ambaye
hana uzoefu kuhusu kujamiiana kwa mwanamke na mwanamume, lakini haiishii hapo.
Pamoja na hayo pia kuna wazo la mtu fulani ambaye anaweza akawa na msongo wa
mawazo, asiye na uhakika, au hana uzoefu wa kile kinachoweza kuwafurahisha au
namna ya kumridhisha mwenzake – jambo ambalo linaweza kufanana na mtu ambaye
amedhalilishwa ama kubakwa. Na kusema kwamba kuingiliwa huko kunaweza kukawa
mwanzo wa kuelewa utamu wa ngono katu hakuna nafasi hapa kwa sababu hakulingani
na hisia za mtu aliyeridhia kufanya ngono na yule aliyelazimishwa ingawa wote
wameshiriki tendo la ngono kimwili.
Uzoefu wakati mwingine unaonekana kama
kitu ambacho mtu mwingine anajifunza. Ni dhahiri kwamba mtu ambaye amebakwa
hajajifunza kitu chochote kinachoweza kufurahisha, na anakuwa hawezi kuwa na
hamu ya kujifunza. Na kusema kwamba kuingiliana kimwili kwa mwanamke na
mwanamume kwa mara ya kwanza kama ndiko kutolewa bikira kutaitweza furaha ya
mtu huyu na hatakuwa na uzoefu wowote.
Alamsiki!
Niandikie: brotherdanny5@gmail.com
No comments:
Post a Comment