Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 31 January 2016

VIWANDA VITANUSURU ZAO LA NYANYA IRINGA


Na Daniel Mbega, Iringa

CHINI ya miti ya mikaratusi, kando ya Mto Mlowa, vijana wanaonekana wakijaza nyanya kwenye matenga ya mbao huku pembeni yao kukiwa na malundo makubwa ya zao hilo.
“Hii ni hasara kubwa, nimekuja na matenga hamsini, lakini inaonekana yametoka thelathini tu, haya malundo yote ni nyanya zilizolainika (masalo) ambazo haziwezi kwenda mahali popote,” anasema Jacob Kamota, mkulima wa nyanya kutoka Kijiji cha Iyayi, Kata ya Image wilayani Kilolo.
Jacob analalamika kwamba, huko shambani pia ameacha malundo ya nyanya zisizofaa kusafirishwa, ingawa zinafaa kwa matumizi ya nyumbani au hata kwa kusindikwa, hali ambayo inazidi kumtia umaskini badala ya kujikwamua kiuchumi.

UWEKEZAJI KATIKA ARDHI NI MAJANGA


Na Daniel Mbega, Morogoro

SERIKALI, kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) iko kwenye mchakato wa kupitia zabuni kwa ajili ya uwekezaji kwenye mradi mkubwa wa kilimo cha miwa na mpunga wa Mkulazi, Wilaya ya Morogoro Vijijini, mkoani Morogoro katika eneo la hekta 60,000.
Taarifa zinasema, hekta 40,000 katika mradi huo zimetengwa kwa kilimo cha miwa kitakachokuwa na mashamba mawili yenye hekta 20,000 kila moja na hekta 20,000 zilizosalia zimetengwa kwa kilimo cha mpunga katika mashamba manne yenye ukubwa wa hekta 5,000 kila moja.

TUKIFUATA MAADILI NA MIIKO YA UONGOZI TUTAMSAIDIA MAGUFULI

Rais John Magufuli wakati alipokula kiapo Novemba 5, 2015

Na Daniel Mbega
YEHU mwana wa Yehoshafati, mwana wa Nimshi alikuwa miongoni mwa wafalme wa Israel na alitawala baada ya Ahabu katika Samaria.
Kabla ya kuwa mfalme, yeye ndiye aliyekuwa jemedari wa jeshi la Israel.
Katika kipindi hicho wafalme waliotangulia walikuwa wamemuasi Bwana, Mungu wao ambaye aliwakomboa kutoka utumwani Misri, wakaabudu miungu ya kigeni ambayo Mungu, kwa kinywa cha Nabii Musa, aliwakataza.

TANROAD YA BOMOA NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKA HIFADHI YA BARABARA MAENEO YA BUZA, LUMO TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) na Polisi , wakisimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana. Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na Tanroad lakiwa wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.

WACHINA WAISHIO NCHINI WAADHIMISHA MWAKA MPYA 2016 "NGEDERE"

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akifungua Mwaka Mpya Kichina wa 2016 unaojulikana kama mwaka wa “Ngedere” kulingana na utamaduni wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kushoto ni mshereheshaji ajiyejitambulisha kwa jina la “Sharobaro”.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA AISHUKURU TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE, WANANCHI WA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

DC. Paul Makonda
Mnamo tarehe 23 wilaya yangu iliamua kufanya upimaji wa bure wa magonjwa ya moyo, upimaji ambao niliamini ungebeba faida kubwa nne: moja, kujenga utamaduni wa kupima afya mara kwa mara miongoni mwa wananchi, pili kubaini watu ambao tayari wanasumbuliwa na magonjwa ya moyo, tatu kuchukua hatua za awali za kuwasaidia wale ambao tayari wameshashambuliwa na magonjwa hayo na mwisho kutoa elimu juu ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yote ya moyo. 

Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa unaoweza kuzalisha magonjwa mengi sana na kama hujafanya vipimo sahihi ni rahisi kushughulika na matokeo ya ugonjwa huku ukiacha chanzo kikizaa magonjwa mengine. Mathalani, unaweza kujikuta unahangaika na kuvimba kwa miguu au kuhangaika na macho ama figo aukisukari na hata kupoteza nguvu za kiume ukifikiri ndio tatizo kumbe tatizo la msingi ni moyo. 

MTAA WA GONGO LA MBOTO MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WAENDELEA KUUNGA MKONO KAULI YA RAIS DK.MAGUFULI YA KUFANYA USAFI

 Mwenyekiti wa Kikundi chaYetu Envirotec Group kinachojishughulisha na kufanya usafi katika Mtaa wa Gongo la Mboto Manispaa ya Ilala,  Ali Mwinyimkuu (kulia), akishiriki kufanya usafi na wananchi Dar es Salaam jana, ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya usafi kila baada ya wiki mbili ili kuunga mkono kauli Rais Dk. John Magufuli ya kufanya usafi katika maeneo tunayoishi na kufanyia shughuli zetu nchini.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ASIFU MIRADI YA UFUGAJI GEREZA LA UZALISHAJI MIFUGO MTEGO WA SIMBA, KINGOLWIRA MKOANI MOROGORO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, (kushoto) akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Magereza alipotembelea Gereza la uzalishaji mifugo Mtego wa Simba lililopo Kingolwira mkoani Morogoro.

DKT. KIGWANGALLA AWAPA FUNZO WATUMISHI WA SEKTA YA AFYA, AWATAKA KUWA WABUNIFU

Licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kuboresha sekta ya afya nchini, watumishi wa sekta ya afya wametakiwa kuwa wabunifu ili kuweza kutoa huduma kwa watu wote hususani wenye kipato cha juu.
IMG-20160130-WA0029
Licha ya kutembelea wodi mbalimbali za wagonjwa, Dkt. Kigwangwala alitembelea maabara ya hospitali hiyo na kuridhika na vifaa vilivyopo kwenye hospitali, kushoto ni mtaalamu wa viwango vya maabara, Felix Zelote akimpatia maelezo waziri huyo

SERIKALI YATOA VIPAUMBELE VYAKE KWA WANANCHI.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ilivyojipanga kuboresha na kuhudumia sekta mbalimbali nchini ikiwemo elimu, umeme, maji na miundombinu.  Kulia ni Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alfayo Kidata na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu.

WAZIRI MAKAMBA ATOA MSAADA MABATI 300 KWA WAHANGA AMBAO NYUMBA ZAO ZILIZOEZULIWA NA UPEPO JIMBONI KWAKE.

January Makamba

NA RAISA SAID, BUMBULI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshugulikia Muungano na Mazingira,January Makamba ametoa msada wa mabati 300 kwa wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mbalimbali jimboni humo.

NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA

Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENZI MKOANI KILIMANJARO.

Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Majaliwa Kassim Majaliwa akiwasili Ikulu ndogo ya mjini Moshi.

WATUMISHI WA HOSPITAL YA SEKOUR TOURE, HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA NA CHUO CHA IFM WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI LA KILA MWEZI.

Dkt.Magreth William Magambo ambae ni Daktari Bingwa wa Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa ufafanuzi juu ya Ushiriki wa Watumishi wa Hospitali hiyo la kushiriki Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.

Saturday 30 January 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA KASSIM MAJALIWA KUSHIRIKI IBADA YA KUMUINGIZA KAZINI ASKOFU MKUU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHELI TANZANIA (KKKT) MJINI MOSHI.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Amos Makala akizung4umza na wanahabari ofisini kwake kuhusu ugeni wa Waziri mkuu ,Majaliwa Kassim Majaliwa mkoani Kilimanjaro.

WATANZANIA WENGI WANAKOSA FURSA ZA KIMAENDELEO KUTOKANA NA KUTOJUA LUGHA.

Charles Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara.

MWONEKANO WA KUUDHI KATIKA LANGO KUU LA KUINGILIA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA.

Mwonekano katika lango Kuu la Kuingilia katika Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba Jijini Mwanza pindi mvua inaponyesha. Ni zaidi ya Usumbufu, kero na adha kwa wanaoingia na kutoka Uwanjani hapo pindi mvua inaponyesha.

WAZANZIBAR WAANDAMANA NCHINI CANADA KUPINGA KURUDIWA KWA UCHAGUZI ZANZIBAR

Na Mwaandishi wetu Washington 
Wakati hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar ikiwa inazidi kutokota, bila kujali theluji na baridi kali, Wazanzibari waishio nchini Canada mnamo tarehe 27 mwezi huu walifanya maandamano katika Mji Mkuu wa nchi hiyo, Ottawa katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kusaka suluhisho la amani kwa mgogoro wa kisiasa Visiwani humo.
Mandamano ya Wazanzibari waishio nchini Canada wakiwa mwenye ofisi ya European Union  Mjini Ottawa
Wazanzibari hao waliandamana hadi kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Canada kwa lengo la kufikisha ujumbe wao kukhusiana na hali mbaya ya kisiasa huko Zanzibar.

FLAVIANA MATATA NA MO DEWJI FOUNDATION WAKABIDHI MSAADA WA CHOO S/M MSINUNE, BAGAMOYO

002Meneja Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Pwani. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto (kulia). Katikati ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation.

SUMAYE AIANGUKIA SERIKALI WANANCHI KUVAMIA SHAMBA LAKE LA EKARI 33 MABWEPANDE JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye  Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kuwasili eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kuangalia eneo la ekari 33 la Sumaye lililovamiwa na wananchi.

UMOJA WA WANAWAKE TUGHE TAWI LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAKUTANA, WAJADILI UMOJA NA USHIRIKIANO JIJINI DAR ES SALAAM



Mwenyekiti wa Mfuko wa Kusaidiana wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jackline Semu (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa Umoja huo walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano uliopo ndani ya umoja wao. Katikati meza kuu ni Katibu wa Mfuko huo, Joyce Ngonyani na kushoto meza kuu ni Mweka Hazina wa mfuko huo, Christina Kaale. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WANAMAUZO 4,760 WAPEWA ELIMU YA UJASIRIAMALI NA TIGO

Baadhi ya wanamauzo wa kanda ya pwani ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya mahafali yao ya kuhitimu mafunzo maalum ya ujasiriamali yaliyotolewa na Tigo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

jitihada za kuwawezesha wafanyakazi wake wa kujitegemea kumudu changamoto mbalimbali za kikazi na kimaisha, Tigo imewapa wafanyakazi hao wapatao 4,767 mafunzo maalum ya ujasiriamali kupitia mpango wake wa mafunzo kazini.

MGODI WA BULYANHULU WATOA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'WALE KAMA USHURU WA HUDUMA.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akiwa na wafanyakazi wengine wa Bulyanhulu Gold Mine wakikabidhi mfano wa hundi kwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'wale Venance Ngeleuya ,Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahim Marwa .

MTEJA AILALAMIKIA TANESCO CHARAMBE KWA KUCHELEWA KUMUWEKEA UMEME

Mteja Ambwene Kyoga


Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Charambe Temeke jijini Dar es Salaam limelalamikiwa na mteja wake mmoja kwa kushindwa kumfungia umeme kwa wakati licha ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo kuagiza wateja wapya kufungiwa umeme katika kipindi kifupi.

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAFUTA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI.

Kulia ni Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

ATHARI ZA MVUA JIJINI DAR ES SALAAM

 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha.

KAMANDA WA MATUKIO BLOG YAPONGEZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA COVERAGE NZURI YA UCHAGUZI MKUU 2015

 Mmiliki wa Blogu ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam.

SAPOTI YAKO YAHITAJIKA KWA VIJANA HAWA KATIKA WIMBO HUU

waleo - sikuachi
This is Brand new Audio from Tanzanian Artist Called WALEO, Song Called "SIKUACHI" Produced by Fraga Studio:: Uprise Music.

KONGAMANO LA UNESCO NA WIZARA YA ELIMU LAMALIZIKA, VIPAUMBELE VYA ESDP VYAPATIKANA

1
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) lililofanyika katika ukumbi wa NACTE, jijini Dar es Salaam.(Picha na Philemon Solomon wa Fullshwangwe)

UNILEVER YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI TUMAINI

 Balozi wa Blue Band Ayubu Athumani akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa darasa la sita Joseph Deogratius wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka mshindi katika shindano la Band ‘Kula Tano’, jana. Wapili kulia ni mwalimu wa michezo Naelijwa Shaidi.

WAKABIDHIWA JENGO LA MAFUNZO NA MADAWATI KILOMBERO

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero
Mke wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Louise Bainbridge akiongea na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilombero, Muungano, Kantui, Ujirani, Lyahira na Mapinduzi (hapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi madawati  jana, Kilombero. Katiakti ni Meneja Mkuu wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Mark Roe-Scott na kulia ni meneja utawala wa kiwanda cha sukari cha Kilombero Allawi Mdee.

BENKI YA NMB YASHIRIKI MAONESHO YA WADAU WA KILIMO NA BIASHARA AFRIKA MASHARIKI

Meneja Mahusiano Programu za Wakulima Wadogo wa Benki ya NMB Plc, John Machunda (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka (wa pili kulia) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya biashara kwa wadau wa kilimo Afrika Mashariki yaliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

SI KWELI KWAMBA RAIS MAGUFULI KUZURU KENYA KUHUDHURIA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU JARAMOGI ODINGA NA FIDEL ODINGA

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii. 

SHUJAAZ RADIO SHOW YAENDELEA KUTISHA ZAIDI 2016 – SASA KUSIKIKA ZANZIBAR NA MIKOA YA KUSINI!


Ulimwengu wa burudani kupitia shoo za redio umeendelea kubarikiwa vilivyo na kijana DJ Tee kupitia shoo yake ya kila wiki ijulikanayo kama SHUJAAZ RADIO SHOW. Kuanzia Novemba 2015, SHUJAAZ imekuwa ikipasua mawimbi nchini Tanzania kupitia EAST AFRICA RADIO na kudhihirisha uwezo alio nao DJ Tee na kuleta burudani bora kwa vijana.

DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR

DAWASCO YAKAMATA 8 WIZI WA MAJI DAR

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limewakamata watu 8 wenye mashamba eneo la Sakoveda mbezi Juu wilayani Kinondoni baada ya kugundulika wakiliibia Maji shirika hilo.

TANGAZO LA KUOKOTWA VITAMBULISHO VYA EDDA MUSHI

 Picha ya msichana huyo kwenye moja ya vitambulisho vyake.

Wednesday 27 January 2016

KUTOKA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA, MAAMUZI YA KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA TARIME VIJIJINI.

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha Kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la Tarime Vijijini uliofanyika Novemba 25,2015. Kesi hiyo ilifunguliwa aliekuwa Mgombea wa Jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Christopher Ryoba Kangoye akiiomba Mahakama kutengua Ushindi wa Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche aliechaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo kwa kuwa uchaguzi huo haukuwa wa huru na haki.

BONNY MWAITEGE: TAMASHA LA PASAKA TULIPE UZITO WAKE


Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injil, Bonny Mwaitege ametoa wito kwa Watanzania kuilipa uzito wa aina yake Tamasha la Pasaka kwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria tukio hilo adhimu duniani.

CHAMA CHA WAENDESHA BODABODA JIJINI ARUSHA CHAIOMBA SERIKALI KUONDOA UTATA ULIOPO KATI YAO NA WAENDESHA PIKIPIKI ZA KAWAIDA.


 Waendesha pikipiki wakiwa mbele ya ofisi ya Mkuu wa mkoa.



Na Vero Ignatus , Arusha.

Chama cha waendesha bodaboda Jijini Arusha ( UWAPA) chaiomba serikali kutatatua utata uliopo kati ya waendesha bodaboda na waendesha pikipiki za kawaida kwa kuwawekea alama maalumu ambayo itawatambulisha, hii ni kutokana na maandamano ambayo yamefanyika siku ya tar 25./1 /2016 kwani ni kinyume kwakuwa chama hakina taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo.

THE TONY ELUMELU FOUNDATION, UNITED BANK FOR AFRICA PLC AND THE UNITED STATES DEPARTMENT OF COMMERCE PARTNER TO ENABLE ENTREPRENEURSHIP IN AFRICA

Group Shot
U.S Secretary of Commerce, Penny Pritzker; Select Tony Elumelu Foundation Entrepreneurs; Kehinde Yinusa, Evans George, Nosakhare Oyegun, Belema Alagun and Founder Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu during the panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Advisory Council on Doing Business in Africa (PACDBIA) and a diverse community of entrepreneurs hosted by Tony Elumelu Foundation and UBA Plc in Lagos yesterday.

UNESCO YAFANYA KONGAMANO LA KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU (ESDP) KWA MWAKA 2017 - 2021

IMG_1467
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP). Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

KAMPUNI YA MAGARI YA ALLIANCE AUTOS WAFANYA MAONYESHO NDANI YA JENGO LA GOLDEN JUBILEE TOWER (PSPF)

DSC_1573
Gari aina ya Amarok Pick up ikiwa katika maonyesho ya mauzo ndani ya jengo la Golden Jubilee Towers ambapo maonyesho hayo ambayo yanaenda sambamba na uuzwaji wa magari hayo yanaendelea hadi hapo kesho jioni kwa 'showroom' hiyo. (Picha zote na Andrew Chale, modewjiblog).

RAIA WA KENYA ADAIWA KUITEKA MANISPAA YA ILALA

Mjane Tabu Salum Tambwe


Dotto Mwaibale

MTU mmoja ambaye ametajwa kuwa ni raia wa Kenya anadaiwa kuiteka Manispaa ya Ilala kwa kushiriana na watendaji wasio waaminifu wa manispaa hiyo kudhulumu viwanja vya watu eneo la Pugu Mwakanga.

Tuesday 26 January 2016

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA KOCHA MINGANGE


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa Kocha Mkuu wa klabu ya Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Meja Mstaafu Abdul Mingange kufuatia kifo cha mke wake Fatma Juma kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.