Hawa wananyonyana ndimi hadharani!
Huyu hata nguo ya kusitiri maungo ya ndani hakuihitaji kabisa.
Kama ni sarakasi, basi wamefuzu. Khanga moja wanasema laki siyo pesa!
Mambo ya kimjini au laana!
Ndugu zangu,
Dunia nzima inataka kuona maendeleo, na kwa hakika maendeleo yamepatikana kwa sababu hivi sasa dunia iko kiganjani, sayansi na teknolojia imeshika kasi.
Lakini pamoja na hayo, inaonekana jamii yetu imevuka mipaka kwani mambo yanayofanyika kwa sasa siyo tu yanakwenda kinyume na utamaduni wetu wa Kitanzania na Kiafrika kwa ujumla, bali ni kinyume na utu. Haiwezekani binadamu mwenye akili timamu akasaula nguo zote na kubaki mtupu mbele ya halaiki huku akikatika viuno, kama ambavyo video hizi zinavyoonyesha.
Siku hizi limekuwa jambo la kawaida kabisa, hasa mijini, kila panapokuwepo na sherehe - hasa za jikoni (kitchen party) wanawake wanasasambua kwa kubaki uchi wa mnyama ama wanacheza taarabu wakiwa watupu. Aghalabu vitendo hivi hufanyika hata mbele za watoto ama watu wenye heshima zao.
Wapo wale wanawake wanaocheza majukwaa wakiwa na khanga moja tu huku ndani wakiwa hawana nguo za kujisitiri maungo yao. Haya nayo twaweza kuyaita maendeleo?
Bratherdanny5 Blog imezitundika picha na video hizi kwa nia ya kukemea tabia hii, lakini pia kuanzisha mjadala kwa jamii nzima kama tuviache vitendo hivi viendelee ama tufanyeje. Maoni yenu ni muhimu sana ili tuijenge jamii iliyostaarabika.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega,
Iringa - Tanzania
0656-331974
No comments:
Post a Comment