Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 27 June 2014

ALGERIA NAYO YATINGA RAUNDI YA PILI, GHANA NA URENO NJE KOMBE LA DUNIA

Algeria imefuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia
Algeria imefuzu kwa raundi ya pili ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Urusi.
The Desert Foxes walitoka nyuma bao moja kwa nunge dhidi ya Urusi katika kipindi cha kwanza na kusawazisha na hivyo kufuzu kama mshindi wa pili katika kundi H nyuma ya Ubelgiji.
Algeria itaingia katika kumbukumbu za historia ya Soka Afrika kuwa mwakilishi wa 6 kuwahi kufuzu kwa raundi hiyo ya 16 bora nyuma ya Cameroon, Ghana, Nigeria, Morocco na Senegal .Hii ndiyo mara yao ya kwanza kupita mkondo wa kwanza.
Algeria ilikuwa imefungwa mapema katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mkwaju wake Aleksandr Kokorin aliyepata pasi murua kutoka kwa Dmitri Kombarov.
Hata hivyo vijana wa kocha Fabio Capello walianza kulinda ngome yao mapema bila ya tahadhari kuwa baop lolote la Algeria ingewarejesha nyumbani.
Mashambulizi ya Algeria yalizaa matunda kunako dakika ya 60 Islam Slimani alipoisawazishia Algeria kutokana na mkwaju wa freekick uliopigwa na Yacine Brahimi.
Wadau watachunguza tukio ambalo shabiki mmoja anadaiwa kumulika kifaa cha Laser usoni mwa kipa wa Urusi Igor Akinfeev kabla ya bao hilo la kusawazisha.
Kocha Capello amelalamikia hatua ya refarii kupuuza tukio hilo akisema kuwa huenda marefarii wananjama ya kuihujumu timu ya Urusi.
Urusi ilifanya mashambulizi kwenye lango la Algeria la Algeria lakini wapi safu ya ulinzi ilikaa ngangari na kuhimili mashambulizi hadi kipenga cha mwisho na hivyo kuipa Algeria alama moja muhimu iliyoiwezesha kuweka historia ya kufuzu kwa raundi ya pili ya Kombe la Dunia.

Algeria sasa imeratibiwa kukwaruzana na Ujerumani katika mechi ya 16 bora siku ya Jumatatu.
Katika hatua nyingine, licha ya Cristiano Ronaldo kuifungia Ureno bao la ushindi timu yake ilipoilaza Black Stars ya Ghana 2-1 katika mechi ya mwisho ya makundi, lakini timu zote mbili zimetolewa mashindanoni.

Ronaldo alifunga bao la ushindi dhidi ya Ghana
Kinaya ni kuwa Ureno ilikuwa keshabanduliwa nje ya kipute hicho baada ya kushindwa mechi zao za kwanza.
Ghana itajilaumu yenyewe kwa kushindwa kusajili ushindi uliohitajika kuihakikishia nafasi katika 16 bora baada ya John Boye alipojifunga mwenyewe.
Asamoah Gyan alifunga bao la kuisawazishia Black stars lakini haikutosha kuifufua kampeini yao kwani walihitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Ujerumani ishinde marekani iliwaweze kufuzu kama washindi wa pili katika kundi G.
Ronaldo hata hivyo atamshukuru kipa wa Ghana Fatawu Dauda kwa sifa alizopata baada ya kufunga bao la ushindi kufuatia kipa huyo kumzawadia mpira katika eneo la lango naye akaifuma kimiani.
Ghana ilikuwa bila Muntari na Boateng ilipochuana na Ureno
Kufuatia ushindi huo wa ureno Ghana ilikamilisha mechi za makundi ikiwa na alama moja pekee huku ureno ikiwa ya tatu na alama 4.
Marekani walijiunga na ujerumani katika mkondo wa pili licha ya Ujerumani kuibana marekani kwa bao moja bila ya jibu.
Ghana hata hivyo ilikuwa tayari inakumbwa na kashfa ambayo wachezaji wake wa kutegemewa Kevin Prince Boateng na Sulle Muntari walitimuliwa kambini huku wale waliosalia wakitishia kususia mechi hiyo ya Ureno kufuatia ubishi kuhusiana na malimbikizi ya marupurupu yao.
BBC

No comments:

Post a Comment