Mabingwa wa mkoa Kilimanjaro timu ya Panone Fc yenye makazi yake mjini Moshi inatarajia kufanya usajili wa wachezaji 6 kutoka vilabu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi.
Afisa habari wa timu ya Panone Cassimu Mwinyi alisema kuwa timu hiyo itafanya usajili huo ili kuiongezea timu ngvu mpya wakichanganya na wachezaji waliopo kutokana na mipango waliyojiwekea ya kuhakikisha timu inafuzu kucheza katika michuano ya ligi kuu.
“Nia yetu ni kuweza kupata vijana wenye vipaji na watakaojituma zaidi katika mchezo kwani huu ni wakati wao muafaka wa kuweza kuijenga timu imara vile vile kuwaweka pamoja na kufanya mpira kuwa ajira yao itakayo wasaidia kuepukana na vitendo viovu ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya, .”alisema Mwinyi.
Kwa upande wa meneja wa timu hiyo Gido Marandu yeye amezungumzia mipango ya timu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanacheza mechi nyingi za kirafiki ili kuwawezersha vijana kuelewana.
“Tunatarajia kuialika timu ya simba sc kucheza naye mchezo wa kirafiki katika kujiweka sawa vile vile uongozi wa timu upo katika maandalizi ya kuandaa hafla kwa ajili ya kuwapongeza wachezaji wao kwa juhudi kubwa walioifanya katika kuiwezesha timu kushiriki ligi daraja la kwanza ambapo hafla hiyo itafanyika baada ya wachezaji kutoka likizo.”alisema Marandu
Huku akiwasihi wadau wote wa soka waendelee kuonyesha ushirikiano kwa timu yao hasa katika kuiunga mkono katika kinyang’anyiro cha kuelekea kushiriki ligi daraja la kwanza ili iweze kushinda na kuwakilisha vyema mkoa msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.
CHANZO FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment