Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 29 June 2014

ARGENTINA ILIPOINYUKA UJERUMANI MAGHARIBI 3-2 KULE MEXICO 1986

800px-Azteca_entrance_96787.jpg
Uwanja wa Azteca, Mexico City

Na Daniel Mbega

Miaka 28 iliyopita, siku kama ya leo, kulifanyika mechi ya kihistoria ya fainali ya Kombe la Dunia baina ya Argentina na Ujerumani Magharibi.
Mchezo huu ulifanyika kwenye Uwanja wa Azteca jijini Mexico City na kuhudhuriwa na watazamaji 114,600, ambapo mpuliza filimbi alikuwa Romualdo Arppi Filho wa Brazil aliyesaidiwa na Erik Fredriksson (Sweden) na Berny Ulloa Morera (Costa Rica).
Argentina ilifanikiwa kushinda kwa mabao 3-2 ndani ya dakika 90.
Jose Luis Brown alianza kuipatia Argentina bao la kuongoza katika dakika ya 23 ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilipoanza Jorge Valdano akaongeza la pili katika dakika ya 56, lakini mshambuliaji hatari wa Ujerumani, Karl-Heinz Rummenigge akafunga bao la kwanza kwa timu yake katika dakika ya 74 kabla ya Rudi Völler kusawazisha mambo katika dakika ya 81.
Ingawa Diego Maradona alikuwa akichungwa kila mahali uwanjani, lakini pasi yake murua ya dakika ya 84 kwa Jorge Burruchaga iliifanya Argentina ipate bao la kuongoza na la ushindi katika fainali hizo, likiwa ni taji lao la pili baada ya lile la 1978. 
Jumla ya kadi 6 za njano zilitolewa, ikiwa ni rekodi ya mashindano hayo kabla haijavunjwa katika fainali ya mwaka 2010 kule Afrika Kusini katika mchezo baina ya Hispania na Uholanzi.
Kufuatia kipigo hicho, kocha wa Ujerumani Franz. Beckenbauer akapewa hadhi isiyofaa ya kupoteza fainali ya Kombe la Dunia akiwa mchezaji na kocha. Beckenbauer alikuwemo kwenye kikosi cha Ujerumani kilichofungwa na England katika fainali mwaka 1966 pale Wembley.
Vikosi vya siku hiyo vilikuwa; Argentina: Nery Pumpido (kadi ya njano 85'), José Luis Brown, José Cuciuffo, Oscar Ruggeri, Sergio Batista, Ricardo Giusti, Jorge Burruchaga/Marcelo Trobbiani 90', Héctor Enrique (kadi ya njano 81'), Julio Olarticoechea (kadi ya njano 77'), Diego Maradona (nahodha - kadi ya njano 17'), Jorge Valdano. Kocha alikuwa Carlos Bilardo.
Ujerumani: Harald Schumacher, Ditmar Jakobs, Karlheinz Förster, Hans-Peter Briegel (kadi ya njano 62'), Thomas Berthold, Andreas Brehme, Norbert Eder, Lothar Matthäus (kadi ya njano 21'), Felix Magath/Rudi Völler 62', Karl-Heinz Rummenigge (nahodha), Klaus Allofs/Dieter Hoeneß 62'. Kocha alikuwa Franz Beckenbauer.


No comments:

Post a Comment