Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Showing posts with label ENZI HIZO ZAMANI. Show all posts
Showing posts with label ENZI HIZO ZAMANI. Show all posts

Tuesday, 25 August 2015

MWALIMU NYERERE NA WAANDISHI WAKE, UNAWAKUMBUKA HAWA?

Picha hii ilipigwa siku 10 tu kabla Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hajang'atuka madarakani mwaka 1985. Hapa akiwa na waandishi wake Ikulu, Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Sammy Mdee , Paul Sozigwa, Mwalimu mwenyewe, Hashim Mbita na Benjamin William Mkapa.

Tuesday, 17 December 2013

BOMOA TANZANIA, BOMOA...

Eti hakuna silaha iliyomshinda. Lakini akakimbia majeshi ya Tanzania yalipomshambulia.

UNABISHA? NITAKUTWANGA!

Idi Amini Dada alikuwa bondia, halafu bingwa wa uzito wa juu kwao Uganda. Ubabe wake haukuchagua mahali, wakati wala nani. Hapa anazipanga kwa mzaha na Ian Woodledge. Huyu jamaa alikuwa noma.

Monday, 16 December 2013

Saturday, 30 November 2013

WARAKA ULIOZUA VITA VYA KAGERA 1978 HUU HAPA


Telegraph (simu ya maandishi) kutoka kwa Idi Amin Dada Oumee kwenda kwa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1978 ndiyo inayodaiwa kwamba ilizua Vita ya Kagera. Inasomeka hivi: “I want to assure you that I love you very much and if you had been a woman I would have considered marrying you, although your head is full of grey hairs. But as you are a man, that possibility does not arise”

HAMADI! NYERERE AKUTANA NA NDULI IDI AMIN!

Nduli Idi Amin Dada Oumee (kushoto) akisalimiana na Mwalimu Julius Nyerere kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU wakati huo) baada ya Amin kumpindua Dk. Milton Obote wa Uganda.

Friday, 29 November 2013

NDULI AMIN ALIPENDA MICHEZO...

Alikuwa mwogeleaji mzuri, aliweza kukaa chini ya maji kwa muda mrefu.
Alikuwa bondia. Michezo yote aliyoshiriki, hata ile ambayo haikuhitaji nguvu, ilimalizika kwa vurugu.


KUUA MTU, KWAKE NI KAMA KUUA INZI!


Probably the most famous quote by Idi Amin Dada was in 1976 at the time his government had killed nearly a half-a-million Ugandans.
Commenting on the mass murders, the despot said casually: "In any country there must be people who have to die. They are the sacrifices any nation has to make to achieve law and order.''


MTAWALA PEKEE WA AFRIKA ALIYEBEBWA, KUPIGIWA MAGOTI NA WAZUNGU!

My mission is to lead the country out of a bad situation of corruption, depression and slavery. After I rid the country of these vices, I will then organize and supervise a general election of a genuinely democratic civilian government.
    • Quoted in Uganda, the Human Rights Situation (1978), by United States Congress. Senate, p. 13 - Civil rights - 1978

ETI NDULI IDI AMINI DADA ALIKUWA HAJUI KIINGEREZA!

His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Hadji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular. 

Thursday, 24 October 2013

SIKU BOLI ZOZO ALIPOIBUKIA JANGWANI!

Kikosi cha Yanga cha mwaka 1994. Kutoka kushoto waliosimama ni Salum Kabunda 'Ninja', Constantine Kimanda, Steven Casmir Nemes, Kenneth Pius Mkapa, Selemani Mkati. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Nico Bambaga 'Machine', Sekilojo Chambua, Edibily Lunyamila, James Tungaraza 'Boli Zozo', na Said Mwamba 'Kizota'.

Na Daniel Mbega
YOUNG Africans, ambayo mwaka 1993 iliteswa sana na wapinzani wake wa jadi, Simba, baada ya kutamba misimu miwili ya nyuma, hatimaye Jumamosi Februari 26, 1994 iliingia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakabili ‘wanyama hao wakali’ wa Msimbazi, ambao mwaka huo walikuwa wameongeza makucha yao kwa kuwasajili wachezaji mahiri na wauaji wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania Bara, Yanga.

Wednesday, 23 October 2013

MNALIKUMBUKA SCUD LA JANGWANI LILILOBOMOA MSIMBAZI MARA MBILI 1991?

Said Sued 'Scud' (wa tano kutoka kulia) akiwa na kikosi cha Yanga 1991


Na Daniel Mbega

ZIKIWA zimesalia siku tatu tu kabla ya pambano la Simba na Yanga, mashabiki wa timu hizo walikuwa wamepamba moto kucharurana mitaani, lakini wadadisi wa mambo walikuwa wamefikia uamuzi kwamba, pambano hilo lingekuwa kama fainali ya ligi hiyo, kwa sababu, timu yoyote ambayo ingeshinda Jumamosi Agosti 31, 1991 ingekuwa vigumu kuzuiwa na timu nyingine huko mbele isitwae ubingwa wa Tanzania Bara msimu huo.

Sunday, 20 October 2013

DUA ALIVYOWADUWAZA YANGA 1993


 Dua Said

Na Daniel Mbega
LIGI Kuu ya Muungano iliyosadikiwa kuwa na msisimko wa kipekee msimu huo kwa vile ilikuwa inawahusisha kikamilifu mamilionea wote watano waliokuwa wanafadhili soka nchini Tanzania, ilianza rasmi Jumamosi Septemba 25, mwaka huo 1993 na ilitarajiwa kupamba moto zaidi Jumapili katika kindumbwendumbwe cha aina yake kwa kuzikutanisha Simba na Yanga.

SIMBA YANUSURIKA KUSHUKA DARAJA TENA 1988


Kikosi cha Simba cha enzi hizo.

Na Daniel Mbega
SIMBA, siyo tu kwamba iliokoka na kuteremka daraja msimu huo ukiwa ni msimu wa pili mfululizo kunusurika, bali ushindi wao wa magoli 2-1 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Yanga Jumamosi Julai 23, 1988 mwaka huo kwenye Uwanja wa Taifa uliifanya ilinde hadhi yake.

Saturday, 19 October 2013

UNAIKUMBUKA YANGA-KATIBA NA YANGA-UKUTA?

 
Kikosi cha Yanga cha mwaka 1987.

Ndugu zangu,
Najitahidi kuwaletea vidokezo vya historia ya soka nchini. Nimewaletea kuhusu matukio katika timu ya taifa, Taifa Stars, matukio ya mechi za Simba na Yanga na hata mgogoro mkubwa wa Yanga wa mwaka 1975 uliozaa Pan Africans.
Leo hii nawaletea vidokezo vingine - vyote hivi kutoka katika miswada yangu ninayoiandalia vitabu ya 'MIAKA 50 YA UBINGWA WA SOKA TANZANI' na 'SIMBA NA YANGA: VUTA-NIKUVUTE'.