Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 31 December 2016

MBUNGE MUSSA WA JIMBO TANGA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA WAKULIMA JIMBONI MWAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta, Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili.

MAONI YA WATEJA NI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO

Na Jumia Travel Tanzania

KUJA kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na kujionea.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHANDISI RAMO MAKANI AUNDA KAMATI YA KUSULUHISHA MGOGORO WA MUDA MREFU WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO, ATOA UFAFANUZI WA UTOAJI WA TAARIFA ZA FARU JOHN

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kupitia kikao hicho aliunda kamati maalum ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa pori tengefu la Loliondo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka.

Friday 30 December 2016

MHANDISI MAKANI ATOA WIKI MBILI KWA WAFANYAKAZI NGORONGORO KUWASILISHA TAARIFA ZA MIFUGO NA MAJENGO YA KUDUMU WANAYOMILIKI NDANI YA HIFADHI HIYO

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Freddy Manongi na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto). 

HARUSI YA WADAU JACKSON BINAGI NA MONICA SYAGA WA TARIME MKOANI MARA YAFANA.

Leo Disemba 29, 2016 ni siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa kijana Jackson John Binagi, wa Kenyamanyori Tarime mkoani Mara (wa tatu kushoto),aliyefunga ndoa na Bi.Monica Syaga wa Mogabiri Tarime, Mara.

MBUNGE MUSSA WA JIMBO LA TANGA AWATAKIA HERI YA MWAKA MPYA WANANCHI WA JIMBO LAKE

Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake  na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata mafanikio.

Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

TAASISI YA MO DEWJI YATOA ZAWADI KITUO CHA TUMAINI LA MAISHA

Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akimkabidhi Mwalimu Leonard ambaye ni mwalimu anayetoa elimu kwa watoto wenye kansa wanaopatikana kituoni hapo.

Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao.

Thursday 29 December 2016

TAMWA WAPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA MAKUNDI MAALUM YALIYOSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2015 MANISPAA YA IRINGA

Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.

MAAMBUKIZO YA VVU NA UKIMWI YASHUKA KWA ASILIMIA 20 NCHINI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) Dk.Leonard Maboko (katikati), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi katika mkutano wa kujitambulisha kwao tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kushika nafasi hiyo Julai 7 mwaka huu. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Muitikio ya Kitaifa, Dk.Hafidhi Amri, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Tacaids, Elizabeth Kaganda na Mkurugenzi wa Habari na Ulaghibishi, Jumanne Issango.

Tuesday 27 December 2016

ACT WAZALENDO KUANZA KAMPENI CHAGUZI ZA MARUDIO DESEMBA 31, 2016


TAARIFA KWA UMMA

Tunapenda kuwafahamisha wanachama wa ACT Wazalendo na umma wa Watanzania kwa ujumla, kuwa kampeni  kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania Bara ambazo chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi Desemba 31, 2016.

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO DAMIAN JAMES WA KATORO MKOANI GEITA

ASAKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU MLIMA KILIMANJARO

Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.

SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI AZIDI KUPUNGUZA BARAZA LA MAWAZIRI


 Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo akizungumza nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam  mwishoni mwa wiki, ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Rais John Magufuli azidi kupunguza Baraza la Mawaziri kufikia 15 na Kamati Kuu 15 pamoja na Halmashauri Kuu wajumbe 55. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

DR GEORDAVIE: JIJENGEENI TABIA YA KUSAIDIA YATIMA


 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini Arusha)

Sunday 25 December 2016

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH WASHIRIKI IBADA YA KRISMASI KATIKA KANISA KATOLIKI (KANISA KUU LA MOYO MTAKATIFU WA YESU) MKOANI SINGIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu  wa Yesu mkoani Singida.

MJENGO WA GHOROFA ALIOUACHA MPOKI BUKUKU TABATA DAR

 Nyumba ya ghorofa moja iliyopo Tabata Bwawani, Dar es Salaam, aliyoiacha aliyekuwa MpigaPicha Mwandamizi wa  The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku. Waliopo nje ni baadhi ya waombolezaji akiwemo Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati).PICHA NA RICHARD MWAIKENDA:KAMANDA WA MATUKIO BLOG

KANISA LA KKKT KIVULE DAR WAMPIGIA SALUTI YESU KRISTO IBADA YA KRISMASI


 Wanakwaya wa Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule, wakimpigia saluti Yesu Kristo walipokuwa wakiimba wimbo wa kumsifu Yesu wakati wa Ibada ya Krismasi.

IBADA MAALUMU YA KRISMASI, KANISA LA EAGT LUMALA MPYA LABARIKI WATOTO.

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, hii leo Disemba 25, 2016 akihubiri kwenye ibada maalumu ya Krismasi ambayo imeenda sambamba na kubariki watoto ikiwa ni ishara njema katika siku hii ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Somo limetoka Kitabu cha Marko Mtakatifu 10:07.

WENGI WAJITOKEZA KWENYE MSIBA WA MPOKI BUKUKU TABATA


 Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

SALAMU ZA SIKUKUU YA CHRISTMAS KWA WANANCHI WA MKOA WA DAR ES SALAAM


Ndugu wana Dar es Salaam,

Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wetu, napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kuwatakia waumini wote wa kikristo na wana Dar es salaam kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas yenye furaha, upendo, amani na utulivu.

Ni muhimu wana familia kuchukua tahadhari za kiusalama katika siku hii ikiwemo kuongeza umakini na uangalizi wa watoto maeneo ya fukwe (beach) ili kuondoa uwezekano wa maafa, kutoondoka nyumbani bila kuacha angalau mtu mmoja mzima wa kubaki kutazama usalama wa nyumba na kuzidisha umakini katika matumizi ya barabara.

WAKRISTO WALIVYOSHIRIKI IBADA YA MKESHA WA KRISMASI JIJINI DAR ES SALAAM

 Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.

UCHAGUZI KANDA YA NYASA, CHAMA CHA DEMOKRASIA NA UBAKWAJI WA DEMOKRASIA HALISI


Mathias Canal (Picha na David Mtengile)

Na Mathias Canal

Katika sehemu ya maelezo yake Raisi wa 16 wa Marekani Bw Abraham Lincoln namnukuu aliwahi kusema kuwa Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile katika chaguzi. 

Friday 23 December 2016

MASAUNI KUYAFUTA MASHIRIKA YANAYOBARIKI USHOGA NCHINI, AWATAKA VIJANA KUISHI KWA KUFUATA MAADILI MEMA YA DINI



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa koti) akiwasili katika Ziara ya Shekhe Uwesu bin Muhammad Alqadiriya iliyofanyika katika Zawiya ya Shekhe Mahadh Kigamboni,  jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni aliwataka vijana kuwa makini na mashirika ambayo yanahamasisha ushoga nchini, na pia alitangaza kuyafuta mashirika hayo endapo yakigundulika. Kushoto ni Shekhe wa Wilaya ya Kigamboni, Abdalla Idd na Shekhe Mohammed Mussa (aliyevaa miwani). Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NDOA YA UPEPO YAFUNGWA TENA JIJINI MBEYA

Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi .

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.

SHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMAS KWA NAMNA HII


Na Jumia Travel Tanzania

JUMAPILI hii ya Desemba 25 ni sikukuu ya Krisimasi ambapo wakristo nchini wataungana na wenzao duniani katika kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa bwana wao Yesu Kristo.

MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum 'Mboto' Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza.

BASATA YAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

KOCHA AZAM FC ATAMBA: TUTAFIKA MBALI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, akitoa maelekezo kwa wachezaji wakati wa mazoezi hayo.

By Abducado Emmanuel
BAADA ya kuiona ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani iliyotoka juzi jioni, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameweka wazi kuwa amekipanga kikozi chake kufika mbali zaidi kwenye michuano hiyo.

SAFARI YA MWISHO YA WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI KATIKA KITUO CHA KIBO KABLA YA KUELEKEA KILELE CHA UHURU

Baada ya kupuumzika kwa siku mbili katika kituo cha Horombo kwa ajili ya kuzoea hali ya hewa ,safari ya kuelekea kituo cha mwisho cha Kibo ikaanza .

TAASISI YA UTAFITI YA MAGONJWA YA BINADAMU KILIMANJARO (KCRI) YAWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA UPENDO NA WALIOLAZWA KCMC

Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi walizopeleka katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Upendo cha mjini Moshi.

MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU

Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Ikonongo wilayani Kishapu, wakitoka Kliniki, ambapo baiskeli ni chombo kikuu cha usafiri katika wilaya hiyo.

Thursday 22 December 2016

SHAMTE ‘HATIHATI’ CITY VS TOTO AFRICANS


WAKATI ‘raundi ya 17 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  ikitaraji kuendelea  jumamosi hii,kikosi cha Mbeya City fc kieendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya mchezo  namba 130 dhidi ya wageni  Toto Africans ya Mwanza uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.

KUWAIT YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA UJENZI WA BARABARA MKOANI TABORA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait, kuhusu miradi ya miundombinu itakayofadhiliwa na Mfuko huo, ukiwemo mradi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Chaya kwenda Nyahua mkoani Tabora. Kulia ni mwakilishi wa Balozi wa Kuwait hapa nchini Bw. Mohammad Rashid Alamiri, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA KUFUNGIA BIASHARA YA USAFIRISHAJI WANYAMAHAI NJE YA NCHI


Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa ufafanuzi wa uamuzi wake wa kuzuia biashara ya usafirishaji wa wanyamahai nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na kusema kuwa uamuzi huo ulitolewa kwa lengo la kupanga vizuri biashara hiyo kwa faida ya serikali na wafanyabiashara wenyewe.

VPL: MECHI 14 ZA FUNGA MWAKA, MBILI KUFUNGUA MWAKA

Mechi 14 za Ligi Kuu ya Vodacom zinatarajiwa kufanyika wakati huu wa msimu wa kufunga mwaka 2016 na mbili za zitafungua mwaka 2017 ambako Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo, wamethibitishia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupata burudani kwa michezo yote kulingana na ratiba.
Katika Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), michezo 15 ya kipindi cha sikukuu za kufunga na kufungua mwaka inatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni isipokuwa ule wa Mbao FC na Mwadui uliopangwa kuanza saa 8.00 mchana kama itakavyojieleza hapo chini kwenye mtiririko wa ratiba.

LESSONS FROM SOCCER - 1




Article by: Allan Lucky
When defenders & goalkeepers work so hard to ensure clean sheets, when midfielders put in lots of effort to ensure balls are ready for delivery, when wingers provide enough crosses and strikers/forwards make sure balls get at the back of the net - the team wins.

MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO, IRINGA

Mwenyekiti wa  chama cha mapinduzi (CCM) wilaya  ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa  kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo

WANAKIJIJI WALIO KWENYE MRADI WA BACKBONE KUUNGANISHIWA UMEME KWA SHILINGI 27,000


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Singida
WANAKIJIJI wa vijiji 126 wanaopitiwa na mradi mkubwa wa umeme, Backbone wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa Kilovolti 400, kutoka mkoani Iringa hadi Shinyanga kupitia mikoa ya Singida na Dodoma, wataunganishiwa umeme kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha shilingi elfu 27,000/-, tu, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, (pichani juu) amesema.

JUMIA TRAVEL YAZINDUA KAMPENI YA PUNGUZO LA BEI KILA JUMATANO


KUFUATIA mafanikio makubwa ya kampeni ya ‘Black Friday’ iliyovunja rekodi ya mauzo kwa zaidi ya 30% kwa siku, Jumia Travel imerudi tena na ofa kabambe inayokwenda kwa jina la ‘Travel Wednesday’ itakayokuwa ikifanyika kila siku ya Jumatano kupitia kwenye tovuti yake. Promosheni hii ambayo pia itajulikana kama “Dream Deals” inajumuisha punguzo kubwa la bei kwenye hoteli za hadhi ya juu ambazo zinazopendwa na watu wengi ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia wateja machaguo mengi zaidi ya sehemu za kupumzika hususani kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.

KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA KRISMAS MULTICHOICE TANZANIA YAWAKUMBUKA YATIMA WA KITUO CHA AL-MADINA JIJINI DAR ES SALAAM

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania na wanahabari wakiwa ndani ya gari wakienda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

KCB YATOA MSAADA WA MILIONI 48

Meneja wa Benki ya KCB tawi la Arusha TFA Hogla Laizer (kulia) akikabidhi Msaada wa hundi ya shilingi milioni 48 kwa mkurugenzi wa shirika la Ereto East Africa foundation Godsave Ole Megiroo.Halfa ya Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Benki hiyo zilizopo jijini Arusha

WAZIRI WA AFYA APOKEA NYUMBA 20 ZA WATUMISHI WA AFYA ZILIZOJENGWA NA TAASISI YA BENJAMINI MKAPA MKOANI MWANZA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), hii leo akikata utepe kuashiria upokeaji wa nyumba 20 mkoani Mwanza, zilizojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa. Nyumba 10 zimejengwa katika wilaya ya Ukerewe na 10 katika wilaya ya Magu.
#BMGHabari

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATAMBULISHA ZANA MPYA NA KUBORESHA DHANA YA TIGO PESA KWA WATUMIAJI WA SMARTPHONE

  Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Tigo, Tawonga Mpore (kushoto), akizungumza Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kutambulisha zana mpya ya simu na kuboresha zana ya Tigo Pesa kwa watumiaji wa Smartphone. Kulia ni Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka Tigo, Suleiman Asilia.

MAHAFALI YA 28 YA SEKONDARI YA AL- HARAMAIN NA YA KWANZA KWA KWA CHUO CHA UALIMU


Vijana wa Madrasat Muhajrina ya Kinondoni wakiwaongoza wahitimu kwa kaswida, kuelekea kwenye viwanja vya mahafali, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Al Haramain jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

JESHI LA POLISI LAMTIA MBARONI MTUHUMIWA WA UTAPELI

Msemaji wa Polisi, Advera  Bulimba – ACP


Na Dotto Mwaibale

JESHI la Polisi nchini limefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa utapeli anayejulikana kwa jina la  Wilfred Masawe (36) , Kabila mchaga na  mkazi wa  Buza, Temeke jijini Dar es Salaam.