Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 13 December 2016

WANAHABARI NA ASKARI WA JESHI LA ULINZI WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 55 YA UHURU WAKABIDHIWA VYETI.



Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwemo Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Waandishi wa Habari wakishuka baada  ya kupanda mlima huo kwa siku sita.Zoezi hilo limeongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Witara (Mwenye fimbo mstari wa mbele) na Naibu Kamanda wa Kikosi cha Ardhini (JWTZ) Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba akipokea Washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro walipofika katika lango la Marangu,Kippi akisalimiana na Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu Jenerali George Waitara ,kiongozi wa msafara wa wapandaji wa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru akivishwa shada la maua mara baada ya kufika katika lango la Marangu.
Meneja wa Kampuni ya Utalii ya Zara Adeventure,Rahma Adam akisalimiana na Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba wakati wa mapokezi yaliyofanyika katika lango la Marangu.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Washiriki wa zoezi la upandaji Mlima Kilimanjaro kufika katika lango la Marangu zilipo ofisi za KINAPA.
Baadhi ya Washiriki wa changamoto ya upandaji Mlima Kilimanjaro baada ya kushuka kutoka kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Waioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,Jenerali Mstaafu George Waitara.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Naibu Kamnada wa kikosi cha ardhini,Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba aliyefanikiwa kufika kilele cha Gilman's umbali wa mita 5685 kutoka usawa wa Bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti cha kupanda Mlima Kilimanjaro,Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi ya Utalii (TTB) Balozi Charles Sanga aliyefanikiwaa kufika kilele cha Stella umbali wa mita 5756.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Star Tv ,Ramadhan Mvungi baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari. .
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwanadishi wa Habari wa Clouds Media Group ,Kilimanjaro na Mwakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini ,Dixon Busagaga baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi ,Arusha ,Zulfa Musa baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru ,umbali wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari akiwa ni miongoni mwa wasicha wawili waliofika kileleni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Mtanzania ,Arusha,Eliya Mbonea baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima,Charles Ndagulla mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Pascal Shelutete mara baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi makimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi ,Pte,Joyce Kaila baada ya kufanikwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi akimkabidhi Cheti Askari wa Jeshi la Ulinzi,Ally Said baada ya kufanikiwa kufika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mwandishi wa Habari ,Idd Uwesso baada  ya kufanikiwa kufika kilele cha Stella.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akimkabidhi Cheti ,Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlia Kilimanjaro,Charles Ngendo mara baada ya kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Mstaafu Jenerali George Waitara akiznungumza mara baada ya kushuka Mlima Kilimanjaro ambako timu ya Watu 36 wakiwemo Askari wa jeshi la Wananchi na Waaandishi wa Habari wamepanda mlima huo kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na askari wa jeshi la ulinzi waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari waliofanikiwa kupanda mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu ,Jenerali George Waitara na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waongoza watalii walioshiriki kufanikisha safari ya Waandishi wa Habari na Askari wa jeshi la Ulinzi  kupanda mlima Kilimanjaro.    Na Dixon Busagaga wa Blogu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment