Mhandisi Mathew Mtigumwe akila kiapo mbele ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ameamuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.
Mhandisi Mathew Mtigumwe aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo tarehe 07 Desemba, 2016 baada ya Rais kufanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia alifanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa.
Uteuzi huo ulimfanya Mhandisi Methew Mtigumwe kuchukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo.Ambapo Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Katika uteuzi huo pia Dkt.
Magufuli alimteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu
Mawasiliano.
MWISHO
No comments:
Post a Comment