Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 27 December 2016

DR GEORDAVIE: JIJENGEENI TABIA YA KUSAIDIA YATIMA


 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini Arusha)


Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii leo
 Nabii mkuu akiwa anaendelea na huduma  ya sikuu kuu ya kukusanya hii leo


Nabii akiwa anamwaga upako kwa waumi waliouthuria katika siku kuuu hii ya kukusanya hii leo (picha na Woinde Shizza,Arusha )
 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo 


 Habari picha na woinde shizza,Arusha
Watumishi  wa madhehebu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kuwasaidia yatima ili nao waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii



Hayo yamebainishwa leo na Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie wakati akifanya  dua maalumu ya kupitisha bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya kukusanya iliyofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha.



Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtumishi kukusanya  na kutoa kile alichonauwezo nacho ili  kuweza kuwasaidia watoto yatima ,wananchi wasiojiweza  ili kuweza kuwafanya nao wajisikie ni sehemu ya jamii



Alisema kuwa mbali na watoto yatima pia aliwasihi makanisa ambayo yanajiweza kuweza kusaidia yale ambayo ni machanga ili kuweza kuwapa nguvu ya kuweza kuendelea kueneza injili na kumtangaza mungu  kupitia makanisa yao .

  Nabii mkuu Dr Geordavie alisema kuwa  kuwa lengo la sikukuu hii ya kukusanya nikuwasaidia watoto yatima kwa kuwapa chakula kama mchele, sukari pamoja na mafuta yakupikia ili nao wajisikie wanafuraha haswa katika kipindi hichi cha sikukuu.

Alisema kuwa  licha ya misaada hiyo kwenda kwa watoto yatima, pia atatoa fedha kwa watumishi wa mungu wenye makanisa madogo hapa nchini lengo likiwa ni kuinua huduma zao na kuwasaidia katika kuendeleza huduma zao ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kanisa, ununuzi wa vyombo vya muziki na shughuli nyingine za kanisa.

Sikukuu hii ya kukusanya  huadhimishwa na huduma ya Ngurumo ya Upako Duniani tarehe 26 ya kila mwaka, watu hutoa sadaka ya vitu mbalimbali ikiwemo fedha kwa mujibu wa maelekezo ya Nabii Mkuu na kisha hugawanywa kwa vituo vya watoto yatima  huku  fedha zikigawanywa kwa watumishi waliotuma maombi ya kupata msaada   wa kuendeleza huduma zao.

Mwaka jana msaada wa zaidi ya shilingi milioni 15 ulitolewa na waumini wa kanisa la Ngurumo ya upako na kugawanywa katika vituo mbalimbali vya watoto yatima huku fedha zikigawiwa kwa baadhi ya makanisa madogo  kwa ajili ya kuwasaidia mambo mbalimbali .

No comments:

Post a Comment