Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu na
Wananchi pamoja na Watumishi wa Kituo cha Huduma za Sheria, mjini Unguja,
Zanzibar (hawapo pichani). Masauni katika hotuba yake, alisema matukio ya
unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi kujitokeza
kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa wakati.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof.
Chris Maina Peter na kulia ni Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji
Mpatani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa
anatoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu katika Kituo
cha Huduma za Sheria, mjini Unguja, Zanzibar. katika hotuba yake, Masauni
aliwataka wananchi nchini, kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika
vyombo husika kwa wakati. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Khamis Rashid Kheri baada ya kupokea
Matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto yalioandaliwa na
Baraza hilo, Mnarani Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Wapili kulia ni
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni
akizungumza na na vijana wa vikundi mbalimbali vya michezo
(hawapo pichani) walivyoshiriki katika matembezi ya kupinga Udhalilishaji wa
Wanawake na Watoto ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Haki Za Binadamu. Tukio hilo
liliandaliwa na Baraza la Taifa la Vijana, Zanzibar na lilifanyika Mnarani
Mwembe Kisonge, mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba yake, Masauni alisema
matukio ya unyanyasi yanaongezeka kwa wingi nchini, hivyo amewataka wananchi
kujitokeza kutoa taarifa za ukatili na unyanyasaji katika vyombo husika kwa
wakati. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Sehemu ya vijana ambao walishiriki Matembezi ya Kupinga
Unyanyasaji wa Wanawake na Watoto wakiwa wameshika bango ambalo lina ujumbe
unaowataka askari kuwasaidia wananchi zaidi katika mapambano ya kudhibiti
matukio ya unyanyasaji nchini. Vijana hao walipokelewa na mgeni rasmi katika
tukio hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(hayupo pichani). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa), Mwenyekiti
wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC), Prof. Chris Maina Peter (wapili
kushoto waliokaa), Mkurugenzi wa Kituo wa Kituo hicho, Harusi Miraji Mpatani (wa
pili kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Maadhimisho
ya Siku ya Haki za Binadamu Duniani. Masauni alikuwa mgeni rasmi katika tukio
hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ZLSC, mjini Unguja, Zanzibar. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment