Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 22 December 2016

SHAMTE ‘HATIHATI’ CITY VS TOTO AFRICANS


WAKATI ‘raundi ya 17 ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara  ikitaraji kuendelea  jumamosi hii,kikosi cha Mbeya City fc kieendelea na mazoezi ikiwa ni matayarisho ya mchezo  namba 130 dhidi ya wageni  Toto Africans ya Mwanza uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Kwenye mazoezi ya timu hiyo leo asubuhi, Ofisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema maandalizi kuelekea  mchezo huo  yanaendelea  vizuri na wachezaji wote wakiwa na ari kubwa  licha ya kuwepo kwa taarifa za  majeraha kwa mlinzi Haruna Shamte aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar.
Kama unavyofahamu jumamosi iliyopita tulipata suluhu ya 0-0 na Kagera Sugar, mara hii tunafanya maandalizi makubwa kuhakiksha  tunashinda mchezo ujao, pointi tatu ni jambo pekee linalohitajika kwenye duru hii ya pili, tunaifahamu Toto kuwa ni timu nzuri lakini mara kadhaa sisi tumekuwa tunaibuka wababe dhidi yao, alisema
Akiendelea  zaidi Ten aliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo dhidi ya Toto, City inaweza kukosa huduma ya mlinzi wake Haruna Shamte aliyepata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita  ingawa  jopo la madaktari  wameahidi kutoa taarifa  mpya  juu yake siku ya kesho huku akigusia  pia  suala la ITC ya  kiungo Mrisho Ngassa.
Baadhi ya wachezaji wa kikosi cha City wakipata maji ya kunywa kwenye mazoezi leo asubuhi
Shamte alipata majeraha kwenye mchezo uliopita, huenda  asiwepo kikosini  jumamosi, ingawa hili litategemea na ripoti ya daktari siku ya kesho, kuhusu Mrisho Ngassa ni kweli ITC yake ilichelewa, hii ni kwa sababu ijumaa na jumamosi  ni siku ya mapumziko huko Oman, tulizungumza nao jana wakaahidi kututumia leo, hivyo tuna uhakika leo wataituma na ni wazi atakuwa sehemu ya kikosi  kwenye mchezo huo,alimaliza. 

No comments:

Post a Comment