Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 31 July 2016

JPM AKOSHWA NA DC WA IGUNGA JOHN MWAIPOPO, AAMURU STENDI YA BASI NA SOKO VIANZE KAZI JUMATATU

 Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo akielezea changamoto za Stendi ya Mabasi ya abiria na Soko jipya zinazoikabili wilaya hiyo wakati wa mkutano wake wa hadhara mjini Igunga leo Jumamosi Julai 30, 2016. Mkuu huyo wa wilaya ambaye ana mwezi mmoja toka aanze kazi alimweleza Rais kwamba kuanza kwa stendi ya basi kunasubiri kibali kutoka SUMATRA na kwamba soko jipya ambalo limeshamalizika kujengwa halitumiki kwa sababu ya mkanganyiko unaohusu badhi ya wafanyabishara kuhodhi sehemu kubwa ya soko jipya na kutolitumia huku wakiendelea kufanya bishara kwenye soko la zamani ambako nako pia wana sehemu za Biashara.

Saturday 30 July 2016

ZLATAN IBRAHIMOVIC SCORES IN MAN UNITED'S 5-2 WIN OVER GALATASARAY


Zlatan Ibrahimovic scored a bicycle-kick four minutes into his debut as Manchester United beat Galatasaray 5-2.
Ibrahimovic, 34, met Antonio Valencia's cross with a typically athletic volley which bounced kindly into the net.
The Turkish side then bossed the remainder of the half and led thanks to goals from Sinan Gumus and Bruma.
But a much-changed United side were rampant after the break. A Wayne Rooney double, Marouane Fellaini header and Juan Mata goal sealed victory.

MASAUNI AONGOZA MSAFARA WA MABALOZI WA USALAMA BARABARANI KUJIFUNZA KAZI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI , JIJINI D’SALAAM


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa amevaa mtungi wa hewa safi na salama ambao utumiwa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pindi anapokosa hewa wakati wa tukio la uzimaji moto au maokozi. Kushoto ni Mrekebishaji wa Vifaa vya Kupumulia wa Jeshi hilo, Sajini Paul Mwenda.   Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye. Masauni aliongoza msafara wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ambao walifanya ziara ya kujifunza kazi za Jeshi hilo katika Kituo cha Zimamoto, Mkoa wa Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SIA PIUS NDIYE WINDHOEK DRAUGHT MISS SINZA 2016

 Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.

WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAAGIZWA KUTENGA BAJETI ZA MAAFISA KILIMO

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah.

MBUNGE WA ILEMELA AANZA ZIARA ZA KUKAGUA MIUNDOMBINU JIMBONI HUMO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (katikati), jana amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.

Nelly Mwagosi: Nahamia Dar ‘soon’

SHINDA NYUMBA (2)
Nelly Mwangosi (kushoto) akikbidhiwa mkataba wa nyumba aliyoshinda kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers.

HIVI karibuni aliyeibuka mshindi wa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba, iliyoendeshwa na Global Publishers Ltd kwa muda wa miezi sita, alikabidhiwa mjengo wake wenye thamani ya mamilioni, uliopo Salasala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

MAKOCHA TANZANIA WAANZA KUIVA

Makocha 20 wa Tanzania wanaofanya kozi ya Leseni A kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), wamemaliza kozi hiyo hatua ya kwanza na kusema, “Tumenolewa na sasa tumeiva vya kutosha,” amesema mmoja wa wanafunzi hao, Wilfred Kidao leo Julai 30, 2016 wakati Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.

MKWASA AAHIRISHA KAMBI TAIFA STARS

Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya Ligi Kuu msimu unaoanza sasa, umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi, mwaka huu, imefahamika.

AfDB YAAHIDI KUENDELEA KUIPIGA JEKI TANZANIA KUKUZA UCHUMI WAKE

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) akiwa kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Frannie Leutier (katikati) na Mwakilishi mkazi wa Benki hiyo Bi. Tonia  Kandiero. (Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango).

SKY SPORTS YAUNGANA NA STARTIMES KUONYESHA LIGI YA CHINA


Na Dotto Mwaibale
Kituo cha matangazo ya luninga cha Sky Sports cha nchini Uingereza katikati ya wiki hii kilisaini mkataba mnono wa kuonyesha moja kwa moja ligi kuu ya China kwa misimu mitatu ijayo ambayo pia kwa Tanzania inaonekana kupitia visimbuzi vya StarTimes.

WAZIRI NAPE AONGOZA MAPOKEZI YA MWILI WA JOSEPH SENGA AIRPORT DAR


 Waombolezaji miongoni mwao wakiwemo waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa MpigaPicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaamm jana, ktuoka nchini India ambako alipatwa na mauti. Wa pili kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia alifika kwenye mapokezi hayo. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Friday 29 July 2016

U17 MADAGASCAR KUIJARIBU SERENGETI BOYS KESHO

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ya Madagascar kesho Jumamosi Julai 30, 2016 itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa wa Madagascar.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO

Naibu Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.

NELLY MWANGOSI AKABIDHIWA NYUMBA YAKE

SHINDA NYUMBA (22) SHINDA NYUMBA (23)
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James pamoja na mshindi wa nyumba Nelly Mwangosi wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa nyumba hiyo iliyopo Salasala.

TAMWA kupambana na ajali za barabarani kuokoa vifo vya akinamama na watoto


Mgeni rasmi katika hafla ya TAMWA wakizinduwa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima. Mgeni rasmi katika hafla ya TAMWA wakizindua mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo. TAMWA wamezindua mradi huo ikiwa ni jitihada za kupunguza ajali hizo ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wanawake, watoto pamoja na jamii nzima.

MRADI WA HARAMBEE NI MKOMBOZI WA WANANCHI WA KIJIJI CHA CHOLE, MAFIA - PWANI

Mwenyekiti wa Kijiji cha Chole, Shehari Ahmadi akielezea waandishi wa habari maendeleo ya kijiji cha Chole ikiwa ni pamoja na kutolea ufafanuzi suala la kauli iliyoleta mkanganyiko hivi karibuni ya kuwa mwekezaji amemilikishwa mapango ya kale kinyume cha sheria jambo ambalo si halina ukweli wowote kwa vile linachafua sura ya kijiji chao. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. 

Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog - CHOLE, MAFIA. 
Wananchi wa kijiji cha Chole, wilayani Mafia - Pwani wameusifia mradi wa Harambee unaowapatia elimu watoto wao. 
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog iliyoweka kambi kijijini hapo kujionea hali halisi ya kisiwa hicho, wananchi hao walisema ujio wa mwekezaji umekuwa mkombozi wa wanachi kwa vile ni mambo mengi waliyofaidika kwa muda wote ambao amekuwepo mwekezaji kijijini hapo.

HOMA YA INI B NA C KUTOKOMEZWA IFIKAPO MWAKA 2030

 Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo mchana.

WAZIRI MAKAME MBARAWA ATEMBELEA MABWEPANDE NA KUAGIZA TBA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na Afisa Uhusiano wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bi. Edna John wakati alipotembelea ujenzi wa mradi wa nyumba za wafanyakazi eneo la Bunju B jijini Dar es salaam.

Tigo yadhamini mkutano wa wadau wa simu duniani (GSMA)

Mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Diego Gutierrez (kushoto) akijibu swali wakati wa mahojiano kwenye mkutano wa wadau wa Makampuni ya simu Duniani (GSMA) wanaokutana jijini Dar es Salaam.

Ratiba ya Usaili Maisha Plus East Africa 2016

Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania. 
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub 
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden 
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge 
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden 
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
 13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe 


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu. 

 Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
   

 Bofya hapa chini kuona video 33 fupi za usaili wa Maisha Plus Dar es salaam.

MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI

Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau.

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MSIBA WA JOSEPH SENGA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga kutokana na kifo cha Joseph Senga – Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima.

KATIBU MKUU TFF ATOA SABABU ZA AIRTEL KUIBUA VIPAJI

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amesema kutimia kwa malengo ya Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imesukuma kampuni hiyo kuendelea kudhamini mashindano ya soka kwa vijana - wavulana na wasichana.

MSIWE WACHOYO WA ELIMU – WALLACE KARIA

Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amewaagiza waamuzi wenye Beji kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kadhalika waamuzi waandamizi waliohitimu kozi leo Julai 29, 2016 kutokuwa wachoyo wa kutoa elimu waliyopata kwa wenzao wa madaraja ya kwanza, pili na tatu.

MAKONDA, MALINZI KUPAMBA UZINDUZI AIRTEL RISING STARS KESHO


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (pichani) kesho Jumamosi Julai 30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Wednesday 27 July 2016

KAMPUNI YA MGODI WA GEITA GOLD MINING (GGM) YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI.

Mkuu wa wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiongozana na kundi la wapanda mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya Mgodi ya Geita Gold Mining (GGM) waliopanda kwa lengo la kuchangisha fedha za kusaidia taasisi mbalimbali zinazo shughulika na mapambano dhidi ya Ukimwi.

DC MUHEZA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA TEULE MUHEZA,AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipofanya ziara ya kuitembelea hospitali ya Teule kuangalia changamoto zinazoikabili kulia ni Mganga Mfawizi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.

DUA ZOTE KWA SERENGETI BOYS


Dua na sala za Watanzania zielekezwe pia kwa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, iliyoondoka leo saa 12.00 Uwanja wa Ndege ya Mwalimu Julius K. Nyerere, Dar es Salaam, Tanzania kwenda Antananarivo, Madagascar kupitia Uwanja wa Ndege wa Ndege ya Oliver Tambo jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

SHEIKH SAID BADO MAKAMU MWENYEKITI TPLB



Bwana Said Mohamed bado ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kuingia kwenye wadhifa huo katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 2013.

Nafasi hiyo ya Bw. Mohamed ni kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji za TPLB, na aliipata kupitia uchaguzi huo. Pia Makamu Mwenyekiti huyo ni Mwenyekiti wa klabu ya Azam FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.

Bw. Mohamed alikuwa Meneja Mkuu wa Kampuni ya Salim Said Bakhresa ambayo pia inamiliki pia timu ya Azam FC kabla ya kustaafu Mei mwaka huu. Licha ya kustaafu ajira yake ndani ya SSB, lakini Bw. Mohamed bado ni Mwenyekiti wa Azam FC.

Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa TPLB pia ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho hilo na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.


Uchaguzi ujao wa viongozi wa TPLB ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Hamad Yahya unatarajiwa kufanyika mwakani.

INFANTINO AMSIFU MALINZI


Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino amemsifu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwa ni miongoni mwa viongozi wa vyama vya soka duniani walioamua kuendesha soka kwa weledi kutokana na kuratibu mafunzo mbalimbali kwa makocha na waamuzi.

Salamu za Infantino zimetolewa na Msimamizi Mkuu wa kozi ya waamuzi nchini, Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini akisema, “Infantino ana ripoti zote ya namna mpira wa miguu unavyoendeshwa duniani. Anasifu Tanzania kwa  namna mnavyopiga hatua. Ana ripoti idadi ya makocha walivyokuwa wachache na sasa mna makocha wengine wako kwenye kozi.

“Mbali ya makocha, leo tuko nanyi waamuzi, ni hatua kubwa ambayo Rais Infantino amemsifu Rais wa TFF, Bwana Malinzi,” alisema Henrique.

Henrigue aliyeka waamuzi hao kujikita zaidi kusoma namna sheria 17 za mpira wa miguu zilivyoboreshwa kwa kuondoa zaidi ya maneno 1,000 ili kuja kusimamia vema michezo wa soka huku akiwataka kuwa mahiri wakati wote. Henrique anafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na Mark Mzengo kutoka Malawi, Felix Tangawarima wa Zimbabwe na Gladys Onyago kutoka Kenya.

Kozi za Waamuzi wa Mpira wa Miguu wa Tanzania sasa ilianza  jana Julai 25, 2016 kwa waamuzi wenye Beji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) na waaamuzi waandamizi wanaotarajiwa kuveshwa beji hizo kwa majina yao kupendekezwa FIFA kama watapata matokeo mazuri kwenye kozi inayoendelea.

Kozi ilianza kwa ratiba ya waamuzi wote kuchukuliwa vipimo (physical fitness test) kwa kila mwamuzi chini ya wakufunzi hao kutoka FIFA. Baada ya vipimo, darasa la waamuzi hao litaanza kwa nadharia na vitendo. Darasa hilo litafikia mwisho Julai 29, 2016 kabla ya kuanza darasa la waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) na makamishna wa michezo kwa msimu wa 2016/2017.


MKWASA AITA NYOTA 24 STARS


Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 24 watakaoanza kambi ya awali kuajindaa na mchezo dhidi ya Nigeria utakaofanyika Lagos, Septemba 2, 2016.

MBUNGE WA SEGEREA BONNAH KALUWA AREJESHA KIWANJA KWA WANANCHI WA KATA YA BUGURUNI

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,  Bonnah Kaluwa (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo na wafanyakazi wa Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited iliyokodishwa kiwanja kilichopo nyuma ya Kituo cha Polisi Buguruni ambapo ametoa siku tatu waondoke kupisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni. Mapato ya kiwanja hicho kwa zaidi ya miaka 10 yalikuwa hayajulikani yalipokuwa yakienda.

Kampuni ya Tigo yakabidhi vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijijini

Katibu wa chama cha mpira mkoani iringa (IRFA) Ramadhani Mahano akiwa na Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na kulia ni katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa chama cha mpira wa miguu wilaya iringa vijiji kwa ajili ya mashindano ya ligi  daraja la pili, Tigo  ndio wadhamini wa mashindano hayo.


Meneja wa kampuni ya Tigo kanda  ya Kusini DAVIS KISAMO na katibu wa chama cha mpira iringa vijijini JUMA LALIKA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu shiriki

BENDI 10 MAARUFU ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO JUMAMOSI VIWANJA VYA LEADERS NI KATIKA TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA DANSI

 Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.

SERENGETI BOYS YATUA SALAMA MADAGASCAR


Msafara wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfajiri Dar es Salaam, Tanzania imetua salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.

MAAGIZO KWA KLABU ZA LIGI KUU, LIGI DARAJA LA KWANZA


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa Wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha, madaktari na wachezaji kabla ya kuingia kandarasi.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.

Mshindi wa Nyumba Atua Global Tayari Kukabidhiwa Nyumba Yake

SHINDA NYUMBA (1)
Mshindi wa nyumba ya Global, Nelly Mwangosi (katikati) akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya kwenda kukabidhiwa nyumba yake. Kulia ni mumewe Karolo Stephen Magani na kushoto ni kijana wao, Emmanuel Karolo.

SERIKALI YAILIPA BHARTI AIRTEL BILIONI 14.9, TTCL SASA KAZI TU

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kulia) akizungumza kwenye mkutano wake na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (kulia) akizungumza kwenye mkutano wake na Wafanyakazi wa Kampuni ya TTCL wa Makao Makuu na Ofisi za Mkoa wa Dar Es Salaam ulofanyika leo katika Ukumbi wa Azania Front jijini Dar es Salaam.

Sunday 24 July 2016

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO (MoU) UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (aliyeipa mgongo kamera), akizungumza jambo kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHANDISI RAMO MAKANI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.

WANAFUNZI WATARAJIWA CHUO CHA UDSM WAFUNDWA JUU YA MAISHA YA CHUO

Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya NMB, Edith Mwiyombela (kulia) akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM. Meneja wa Mafunzo na Maendeleo wa Benki ya NMB, Edith Mwiyombela (kulia) akiwasilisha mada kwenye Semina kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadhi ya wanachuo iliandaliwa na Kampuni ya Bridge Tanzania Limited kwa kushirikiana na DUFA chini ya udhamini Mkuu wa Banki ya NMB, pamoja na wadhamini wengine wakiwemo PSPF, Crown Cartilage, ACCA na Clouds FM.

WALIOKUWA WANAFUNZI WA BWAWANI SEKONDARI WAIKUMBUKA SHULE YAO KWA KUITEMBELEA

 Baadhi ya wanafunzi tuliosoma Shule ya Sekondari Bwawani tukiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuelekea kuitembelea shule yetu hiyo.

JESHI LA POLISI MKOA WA DAR ES SALAAM LAINGIZA SH.MILIONI 198 KATIKA ZOEZI LA KUHAKIKI SILAHA 14107

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Sirro, akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana alipokuwa akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya uhalifu pamoja na mchakato wa uhakiki wa silaha.

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO



Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert Bwele huku akicheza ngoma ya Ndolela ya kundi la Utandawazi Theatre la mjini Nansio, Ukerewe. Mama Maria Teresa alikuwa ziarani kisiwani humo kuangalia kilimo cha viazi lishe pamoja na usindikaji wa bidhaa mbalimbali za zao hilo kilachotekelezwa kupitia mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Mfuko wa Wanawake Afrika, ambao yeye ndiye rais wake.
 
WAKATI wasanii wa kundi la ngoma za utamaduni la Utandawazi wanajipanga kutumbuiza, watu wengi waliokusanyika kwenye viwanja wa shule ya msingi Bukongo mjini Nansio walikuwa wanajiuliza mtoto Gozbert Bwele (8) aliyekuwa amekumbatia ngoma alikwenda kufanya nini pale.

Monday 18 July 2016

KONGAMANO LA VIJANA WAJASIRIAMALI NA WAWEKEZAJI MKOANI MWANZA LAFANYA.

Mgeni Rasmi, Meneja wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO mkoani Mwanza, Damian John Changa, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, katika ufungaji wa Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza lililohitimishwa jana katika Viwanja vya Gandh Hall Jijini Mwanza. 

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA BARABARA YA MBINGA-MBAMBABAY KM 66 NA BANDARI YA MBAMBABAY


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiongea jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) wakati alipokagua uwanja wa Songea Mkoani Ruvuma. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kuanza ujenzi wa maegesho ya meli katika bandari ambazo meli mbili mpya zinazojengwa na Mamlaka hiyo katika bandari ya Itungi Wilayani Kyela, zitatoa huduma ya usafiri baada ya kukamilika. 

KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI AIPONGEZA TIMU YA UCHUKUZI KWA KUIBUKA MSHINDI MASHINDANO YA MEI MOSI


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Leornard Chamuriho kulia akopokea moja baadhi ya vikombe 11 ambavyo timu ya uchukuzi imeshinda katika mashindano ya mei mosi yaliyofanyika mapema mwezi mei mkoani Dodoma, anayemkabidhi ni Katibu wa Uchukuzi Sports Club Bw. Alex Temba.(Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).