Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 30 May 2016

MUSA MCHEZAJI BORA WA MEI VODACOM

Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Mashindano
Mshambuliaji Abdulrahman Musa wa JKT Ruvu ameibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Mei 2016.
 Musa katika kinganyiro hicho aliwapiku Donald Ngoma wa Yanga na Ali Nassoro wa Mgambo Shooting. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Musa alicheza mechi zote tatu za timu yake na kufunga jumla mabao manne; mawili katika kila mechi.

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA YAENDELEA KUTIMUA VUMBI

Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2015/2016 inaendelea vizuri katika vituo vinne vya Kagera, Morogoro, Singida na Njombe ambapo itafikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Timu sita zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2016/2017. Timu hizo ni zile zitakazoongoza kila kundi, na washindwa bora (best losers) wawili kutoka makundi mawili tofauti.

MKWASA AISHTUKIA MISRI, WANYAMA NA KAZIMOTO WATOA NENO

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo kwa sasa, “Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu walikuwako. Najua  Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi, lakini hawataipata Tanzania.”

BASATA, HAANNEEL WAZINDUA MATUKIO YA SIKU YA MSANII KWA MWAKA 2016



Mkurugenzi wa Kampuni ya Haakneel Production Emmanuel Mahendeka ambayo ni waandaaji wa Siku ya Msanii akimwongoza Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kutia saini kitabu cha wageni wakati alipowasili kuzindua matukio ya Siku ya Msanii (SYM, 2016) kwa mwaka 2016 kwenye Ukumbi wa Alliance Francaise mwishoni mwa wiki.

YALIYOJILI KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LEO MJINI DODOMA

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson Mwansasu akiongoza kikao cha 32 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo mjini Dodoma.

DAWASCO YABAINI WIZI WA MAJI MSIMBAZI BONDENI



Fundi kutoka Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) akiondoa Mpira wa Maji uliokuwa umeunganishwa kwenye kisima kinyume na utaratibu ambapo walikuwa wakitumia huduma ya Maji bila kuwa na mita wala akaunti namba ambapo walinzi jengo hilo awali walidai maji wanayotumia ni ya kisima kwenye jengo lilipo eneo la Msimbazi Bondeni jijini Dar es Salaam.

Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco) limebaini wizi mkubwa wa Maji katika eneo la kata ya Ilala mchikichini mtaa wa Msimbazi Bondeni ambapo walinzi wa jengo hilo walikuwa wamejiunganishia huduma ya Maji kinyume cha utaratibu nakujifanya kuwa wanatumia Maji ya Kisima.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO AHIMIZA UWAJIBIKAJI

Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akitoa neno la shukrani mjini Morogoro, baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu ijayo.

HAWA HAPA WASHIRIKI 19 WALIOPITA KATIKA MCHUJO WA KWANZA SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA MSIMU WA TANO 2016

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster(aliyesimama) akiwapongeza washiriki wote waliojaza fomu za kushiriki  shindano la mama shujaa wa chakula msimu wa tano 2016 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

KIKOSI CHA TAIFA STARS KILICHOTOKA SARE NA HARAMBEE STARS JANA JUMAPILI

Kikosi cha kwanza cha timu ya Soka ya Tanzania -Taifa Stars kilichoanza dhidi ya Harambee Stars ya Kenya Jumapili Mei 29, 2016.

MKAKATI MPYA WA KITAIFA WA KUPANDA NA KUTUNZA MITI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.

JIJI LA DAR KUJENGEWA MFUMO WA KISASA WA UONDOAJI MAJITAKA, MIUNDOMBINU MIPYA YA KUSAMBAZIA MAJISAFI

Ramani inayoonesha Mpango wa upanuzi wa mfumo wa uondoaji wa majitaka katika jiji la Dar es salaam utakaotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuondoa wastani wa uondoaji wa majitaka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2017.

DIWANI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA AZINDUA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO PEOPLE'S

Diwani wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, Deus Mbehe (Chadema) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kikundi cha Kusaidiana cha USHIRIKIANO PEOPLE'S kinachoundwa na Wanachama zaidi wa 100 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mabatini.

Na BMG
Kikundi hicho kiliundwa baada ya kuibuka sitafahamu ya wananchi kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo misiba, baada ya baadhi ya wanachama wa Chadema kutengwa katika shughuli za misiba katika Kata ya Mabatini.

BENPOL AKONGA NYOYO ZA MAELFU WA MASHABIKI KATIKA TAMASHA LA NYAMA CHOMA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwanamuziki mahiri  wa Rnb hapa nchini  , Bernard Michael Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’ akitoa burudani  kwa maelfu ya wakazi wa Dar es salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka mitano ya  Tamasha la Nyama choma 2016,ambapo Tigo ilimdhamini kutumbuiza katika tamasha hilo , mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM LEO JIONI

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo jioni.

WADAU WACHANGAMKIA WINDHOEK TAMASHA LA NYAMA CHOMA VIWANJA VYA LEARDERS JIJINI DAR ES SALAAM

 Mtaalamu wa kuchoma nyama kutoka mkoani Arusha, Jackson Isaya akionesha ufundi wa kuchoma nyama katika Tamasha la Nyama choma lililofanyika ,viwanja vya Learders Dar es Salaam jana.

WILAYA YA MPWAPWA KUFANYA HARAMBEE YA KUPATA MADAWATI JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 4, 2016

 Mkuu wa Wilaya  ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.

Sunday 29 May 2016

BWANA EDWIN MASHAYO NA BI. MARY MOLLEL WAUAGA UKAPELA

Bwana Edwin Mashayo na Bi. Mary Mollel wakionyesha vyeti vyao vya ndoa mara baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la KKKT - Umoja lililopo chuo kikuu cha Dar es Salaam leo May 28, 2016. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog -(Kajunason Studio).

Saturday 28 May 2016

SERIKALI YAWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UPATIKANAJI MAFUTA YA NDEGE

Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akiongea na baadhi ya viongozi wa makampuni ya mafuta (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kukagua matanki ya kuhifadhia mafuta leo jijini Dar es salaam ili kujionea hali ya upatikanaji wa mafuta ya ndege baada ya kugundulika baadhi ya shehena ya mafuta hayo yaliyoingizwa nchini yalikuwa yamechanganyika na mafuta ya petroli.

SERIKALI YATANGAZA KIAMA KWA WATUMISHI WA UMMA WALIOTUMIA VYETI BANDIA KUPATA AJIRA

Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof.Joyce Ndalichako akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa majumuisho ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Na Aron Msigwa - DODOMA.
 
Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa kampeni ya kuwashughulikia na kuwaondoa katika utumishi wa umma watumishi wote walioajiriwa katika  sekta hiyo  wakitumia vyeti bandia.

SERIKALI YAAHIDI KUVIPATIA MAJI VIJIJI 100 VINAVYOZUNGUKA BOMBA KUU LA MAJI LA ZIWA VICTORIA NA MAENEO MENGINE YA PEMBEZONI MWA TANZANIA

 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

TANCDA YAPIMA AFYA ZA WABUNGE DODOMA

 Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata (CCM) Mkoa wa Rukwa, akipimwa mapigo ya moyo wakati wa programu maalumu ya wabunge kupimwa afya zao. Programu hiyo ilifanywa bure na Shirikisho la Vyama vya Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza katika Zahanati ya Bunge, Dodoma leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

SHIRIKISHO LA RIADHA TANZANIA LAMSHUKURU RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI KWA MCHANGO WA TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA OLYIMPIC


WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BENKI YA NMB KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

Mgeni Rasmi katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji,Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Benki ya NMB katika maeonesho hayo yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.

REKODI YA SERENGETI YAIVUTIA KENYA

Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) iliyorejea nchini kutoka ziara ya India ambako walishiriki mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF International Youth Tournament 2016), imerudi na rekodi ya kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Serengeti Boys imecheza mfululizo michezo 7 ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Kore, Malaysia, na Marekani (USA). Kabla ya hapo timu hiyo ilicheza michezo kadhaa ya ndani na timu za chini ya umri wa miaka 20 bila kupoteza hata mchezo mmoja.

VIJANA WANAOKUSANYA USHURU WA MAEGESHO YA MAGARI JIJINI MWANZA WALALAMIKIWA

Gari la mmoja wa wagonjwa katika kituo cha afya cha Bio Health kilichopo mtaa wa liberty jijini Mwanza likiwa limepigwa cheni.
Na BMG
Vijana wanaokusanya ushuru wa tozo za maegesho ya magari jijini Mwanza, wamelalamikiwa kwa namna wanavyotekeleza majukumu yao kinyume na taratibu.

MAONESHO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI YALIYOANDALIWA NA AGRIPROFOCUS YAFANYIKA UWANJA WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

Mgeni Rasmi katika maonesho ya Wakulima na Wagaji ,Mkuu wa idara ya Utumishi na Utawala Manispaa ya Moshi,Wencelaus Lindi akisoma hotuba ya ufunguzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa kusaidia Wakulima wa AgriProFocus yanayofanyika katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 

SIKU YA WADAU WA WINDHOEK ILIVYOFANYIKA HOTEL YA PROTEA COURTYYARD JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benadicta Rugemalira, akizungumza na wadau wa windhoek Dar es Salaam jana katika siku ya wadau iliyofanyika Hoteli ya Protea Courtyyard.

Friday 27 May 2016

CHUMBA CHA DEREVA TAX 'SHAROBARO' KILICHOJAA KINYESI NA MIKOJO CHAZUA KIZAA ZAA MTAA WA MBEZI MTONI GOLD STAR, DAR

Steven a.k.a Nyati 
Chumba cha Steven a.k.a Nyati kikiwa kimejaa chupa zenye mikojo pamoja na mifuko yenye kinyesi.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO

 Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.

MULTICHOICE TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA AFRIKA NA WADAU WAKE DAR

DSC_4273
Social Media Administrator wa MultiChoice (DStv) Tanzania, Shumbana Walwa akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam. (Picha na Modewjiblog)
Kampuni ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa bidhaa za DStv nchini usiku wa Mei 26 wameweza kujumuika kwa pamoja katika kusheherekea siku ya Afrika kwa kukutana na wadau wake Jijini Dar es Salaam na kufurahia paamoja fahari ya Afrika.
Wadau hao ni pamoja na wanahabari, Waendesha vipindi vya televisheni na radio, wasanii na baadhi ya wateja ambao walijumuika kwa pamoja usiku maalum ambao pia walipata kula na kunywa pamoja na kubadilishana mwazo.
Awali wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo maalum, Meneja Uhusiano na Masoko wa MultiAChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu alieleza kuwa, MultiChoice wanajisikia fahari katika ushiriki wao wa kuleta mabadiliko na maendeleo tangu kuanzishwa hapa Barani Afrika miaka 20 iliyopit huku ldngo kuu ni kuwa na maudhui ya kila siku ya kiafrika.
Aidha, Bi. Furaha Sumalu alibainisha kuwa, kwa kuthamini Afrika, hata chaneli wameweka zinazolenga Afrika zikiwemo: Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East ambapo ndani ya chaneli hizo zimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Afrika hivyo watanzania na waafrika kwa ujumla ni wakati wa kuchangamkia bidhaa bora za DSTV ilikufurahia uhondo huo wa Kiafrika na mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya Afrika nan je ya Afrika.

KAMPUNI YA TTCL YAZINDUWA NEMBO MPYA NA HUDUMA YA 4G LTE

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) akizinduwa nembo mpya ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) pamoja na kuzinduwa huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Bi. Edwina Lupembe akishiriki zoezi hilo.

UBA TANZANIA CELEBRATES AFRICA DAY 2016

MD and CEO Mr. Peter Makau
MD/CEO Mr. Peter Makau, (centre in white) poses for a group photo with HO staff members.

Like other in African countries and the rest of the world, UBA Tanzania celebrated Africa day, Wednesday, May 25, 2016.
Africa Day is designated to celebrate the uniqueness of the African continent and its people.
UBA celebrating the day across all countries where we have presence with the theme “Africa Rising”, as a demonstration of UBA’s optimism about the huge potential and resources the continent has been blessed with.

UCHAGUZI YANGA, FOMU KUANZA KUTOLEWA LEO


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza kesho Mei 27, 2016 kuanza kwa mchakato wa kuchukua fomu za kugombea uongozi katika Klabu ya Young Africans ya Dar es Salaam inayotarajia kufanya uchaguzi tarehe 25 Juni mwaka huu.

PICHA ZA MATUKIO YA BUNGE MJINI DODOMA MEI 26, 2016


Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea mjini Dodoma Mei 26, 2016.

Thursday 26 May 2016

KATIBU MKUU KIONGOZI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KINONDONI MWANANYAMALA DAR ES SALAAM LEO

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando (kushoto), akitoa taarifa fupi kabla ya kumribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (katikati), wakati wa ziara yake ya siku moja ya kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kinondoni ya Mwananyamala Dar es Salaam leo mchana. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Michael John, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Ali Hapi.

MAMIA WAJITOKEZA KUMUAGA MWANAHABARI MAKONGORO OGING' KUZIKWA MKOANI MARA KESHO KUTWA

 Picha ya Mwanahabari Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers alikokuwa akifanyia kazi Makongoro Oging', Eric Shigongo akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye lenye mwili wa marehemu Oging' wakati wa kuagwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ilala ya Amana Dar es Salaam mchana wa leo.

TIGO YAMDHAMINI MWANAMUZIKI BEN POL KUBURUDISHA TAMASHA LA NYAMA CHOMA

 Mkuu wa Kitengo cha Burudani na Digitali wa Tigo, Paulina Shao (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tamasha la nyama choma litakalofanyika  Viwanja vya Leaders kesho kutwa Jumamosi Mei 28, 2016 jijini Dar es Salaam, ambapo mwanamuziki Ben Pol atatoa burudani kwa udhamini wa kampuni ya Tigo. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi na katikati ni mwanamuziki Ben Pol.

TAIFA STARS KWENDA KENYA KESHO

Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa (pichani kushoto) na Hemed Morocco (kulia) kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

CAF YAMTEUA MICHAEL WAMBURA KUWA KAMISHNA

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limemteua Michael Richard Wambura (pichani) kuwa Kamishna wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Rwanda na Msumbiji unaotarajiwa kufanyika jijini Kigali, Juni 3, 2016.
Wambura ambaye amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), atakuwa Balozi mzuri katika mchezo huo unaokutanisha timu ambazo nchi imepana nazo. Msumbiji iko Kusini mwa Tanzania wakati Rwanda iko Magharibi mwa Tanzania.

TANZANIA KUTOANDAA CECAFA CUP

Shirikisho a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.

ESRF YAFANYA WARSHA KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO ENDELEVU (SDG)

DSC_2311
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi katika warsa iliyoandaliwa na ESRF ili kuzungumzia Mpango wa Mendeleo Endelevu (SDG). (Picha zote na Rabi Hume, Modewjiblog).

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Katika kusaidia kukamilika kwa Mpango wa Maendeleo Endelevu ambao unataraji kumalizika 2030, Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) imefanya warsha ambayo imekutanisha wadau mbalimbali ili kuona ni jinsi gani wanaweza kubadilishana mawazo ili kufanikisha mpango huo nchini.

MAONYESHO YA BIDHAA ZA PLASTIKI, MPIRA, KEMIKALI ZA PETROLI NA UJENZI KUFANYIKA MEI 27-29 MLIMANI CITY JIJINI DAR

Meneja Mkuu wa Expo One,  Ahmed Barakat, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana jioni kuhusu maonyesho hayo.

MATUKIO NDANI NA NJE YA UKUMBI WA BUNGE

 Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe. Allya Kessy akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.

Tuesday 24 May 2016

WACHAGA WAKUMBUSHWA KUISAPOTI TIMU YAO YA KILIMANJARO INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA WA MIKOA

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,(KRFA) Godluck Mosha akizungumza wakati wa kuwaaga mabingwa wa soka mkoa wa Kilimanjaro, timu ya Kitayosce wanaojiandaa kuelekea mkoani Singida kushiriki ligi ya Mabingwa wa mikoa katika kituo hicho.

MAAJABU: UBOVU WA BARABARA ZA MITAA KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA

Hii ni barabara ya Sabato-Kirumba iliyopo katika Mtaa wa Ngara, Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza. Barabara hii ni imeharibika kutoka na mvua zilizonyesha Mkoani Mwanza kwa zaidi ya miezi minne iliyopita.

NE-YO AWAKOSHA MASHABIKI WA MWANZA KATIKA JEMBEKA FESTIVAL 2016

RC Mwanza, John Mongella
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba, Mbunge wa jimbo la Nyamagama jijini Mwanza, Stanislaus Mabula pamoja na Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye wakimsikiliza Dr. Sebastian Ndege (hayupo pichani).

Katika kusherekea mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio ya Jembe FM iliyo na makazi yake jijini Mwanza, Mei, 21 kumefanyika tamasha lililopewa jina la JembekaFestival ambalo lilikutanisha mashabiki wa redio hiyo walio mikoa ya kanda ya ziwa kwa kupata burudani ya aina yake kutoka kwa msanii wa muziki wa miondoko ya R& B kutoka nchini Marekani, Shaffer Chimere Smith almaarufu kama NE-YO
Licha ya msanii NE-YO pia kulikuwapo na wasanii wa nchini wakiongozwa na Diamond Platinumz ambaye aliambatana na timu yake kutoka lebo yake ya Wasafi (WCB), wasanii wengine ni Fid Q, Baraka Da Prince, Ney wa Mitego, Maua Sama, Mo Music, Stamina, Juma Nature a.k.a Kiroboto, Ruby na wengine wengi.