Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila
mwaka.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Mbarak Abdulwakil (kushoto) akifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba alipokuwa
akizungumza na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo
hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ngosi Mwihava.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira January Makamba akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani
ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO.
Serikali
imeandaa mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda na kutunza miti ili kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi hatua ambayo itarudisha hali ya mazingira kama
yalivyokuwa awali miaka ya nyuma.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
January Makamba alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Mazingira Duniani
ambayo hudhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka.
“Mkakati huu mpya umezingatia kurekebisha changamoto
zilizojitokeza katika kampeni za upandaji miti zilizofanyika katika vipindi
mbalimbali tangu uhuru wan chi yetu” alisema Waziri Makamba.
Ili
kukabiliana na changamoto hizo, Waziri Makamba amesema kuwa Serikali kupitia
Wizara yake imetenga kiasi cha Sh. bilioni 2 ikiwa kianzio kwa lengo la
kusimamia mkakati huo katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Katika
kuhakikisha suala la mazingira limepewa kipaumbele, Mfuko wa Taifa wa Mazingira
ambao ni mdau mkuu wa mazingira utatengewa vyanzo vya mapato yanayokadiriwa
kufikia Sh. bilioni 100 ikiwa ni juhudi za kugharimia mpango huo na mipango
mingine ya hifadhi ya mazingira.
Mkakati
huo ni wa miaka mitano ambao unaanza kutekelezwa 2016 hadi 2021 na unakadiriwa
kugharimu kiasi cha Sh. bilioni 105.2.
Aidha,
Waziri Makamba amebainisha kuwa masuala ambayo yatazingatiwa katika kutekeleza
mpango huo ni pamoja na uhamasishaji na utoaji motisha kwa watumiaji wa nishati
mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa.
Ili
kuhakikisha mazingira yameboreshwa na yawe rafiki kwa kila kiumbe, utekelezaji
na usimamiaji wa mkakati huo, utaanza kutekelezwa kuanzia ngazi ya chini hadi
juu ambapo kila kijiji, kitongoji, mtaa, kaya na kila taasisi itapewa lengo la
pandaji miti kama msingi wa zoezi hilo.
“Tutashindanisha
shule na vijiji katika upandaji na ukuzaji wa miti na tutatoa zawadi nono na
maeneo ya wazi ya Serikali yatapandwa miti” alisema Waziri Makamba.
Katika
kuhakikisha miti iliyopandwa inalindwa na kukua, Ofisi ya Makamu wa Rais itashirikiana na Ofisi
ya Rais Tawala za Mkioa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha halmashauri
zinatunga sheria ndogo ndogo za kuhimiza upandaji na utunzaji miti nchini.
Maadhimisho
ya mwaka huu Kimataifa yanafanyika nchini Angola ambayo yanalenga kupambana na
biashara ya meno ya tembo na pembe za faru yakiongozwa na kaulimbiu “Tunza
wanyama porini kwa maisha”
Siku
ya mazingira Duniani imeanza kuadhimishwa
mwaka 1972 ambapo Baraza la Umoja wa Mataifa lilifanya wa mkutano wake
wa kwanza unaohusu mazingira uliofanyika Stockholm nchini Sweden na kuundwa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira diniani (UNEP).
No comments:
Post a Comment