Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 16 May 2016

JAMII YAASWA KUJENGA FAMILIA IMARA


Na Lorietha Laurence-Maelezo
16/05/2016. Dar es salaam.

Jamii nchini imeaswa kuendelea kujenga familia imara kwa kuwa ndicho kitovu cha mabadiliko katika jamii na maendeleo ya kiuchumi.

 Aidha, imekumbushwa kuwa masuala mbalimbali  hujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa.Hayo yamo katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa maadhimisho  ya Siku ya Familia iliyofanyika Mei 15, 2016.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Tanzania iliadhimisha siku hiyo chini ya kauli mbiu ya isemayo “Familia Yenye Afya Bora ni Mwanga wa Maendeleo” 

Taarifa hiyo imebainisha kuwa familia ni kitovu cha Maendeleo katika jamii hivyo haina budi kutambua kuwa uzingatiaji wa masuala ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hupaswa kujadiliwa, kupangwa na kutekelezwa kuanzia ngazi ya familia kwa ajili ya kuimarisha ushiriki thabiti wa jamii katika maendeleo ya taifa.

Imebainisha kuwa  maendeleo ya nchi hayawezi kufikiwa kama familia hazitakuwa na afya bora hivyo kauli mbiu ya mwaka huu inalenga kuchochea mafanikio ya malengo ya Maendeleo Endelevu yatakayozingatia uboreshaji wa huduma ya afya bora ya familia, malezi bora ya watoto na utunzaji wa afya ya watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.

“ Kila mwanafamilia anahitajika kushiriki  katika maadhimisho ya siku hii muhimu kwa kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo, ikiwemo  vyombo vya habari kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya ili kuharakisha uboreshaji wa afya za wanafamilia wote katika nchi yetu” imeeleza sehemu taarifa hiyo.  

Katika  hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) Bi. Lilian Liundi akiizungumzia siku hiyo katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani (DW) ameeleza kuwa hali ya familia katika maeneo mbalimbali haiko salama kutokana na changamoto za kiuchumi.

Ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto ya tatizo la mimba za utotoni kwa watoto wa kike na wanawake kuachiwa familia hivyo misingi ya familia inakuwa siyo bora kutokana na kuwepo kwa malezi ya upande mmoja. 

Naye mchambuzi wa Masuala ya Siasa kutoka nchini Kenya Bw. Bobby Mkangi  ameeleza kuwa kufuatia hali ngumu ya uchumi misingi ya familia imevurugika na hivyo kupelekea kuwepo na ajira za watoto ambao badala ya kuwa shule wanafanya kazi ndogondogo kusaidia kipato cha familia.

Siku ya Familia Duniani  huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu  wa Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa namba 47/257 la Septemba 20, 1993.

No comments:

Post a Comment