Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza akiongea na
waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na
Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao walitembelea kituo
hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Dkt. Robert Malima akitoa maelezo ya namna
watafiti wanavyofanya utafiti na kuwakusanya mbu katika chumba maalum cha
kufanyia utafiti kwa waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari
wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani
walipotembelea Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani
mkoani Tanga mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa
huo.
Mfanyakazi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa
ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Masha Mfinanga akichambua viluwiluwi
vya mbu na kuviweka kwenye kifaa maalum tayari kwa hatua nyingine za utafiti.
Sungura wanaofugwa katika Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha
Amani mkoani Tanga kwa lengo la kuwalisha mbu wanaofanyiwa utafiti, sungura
mmoja ana uwezo wa kulisha mbu 1500.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka Kituo
cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More”
kutoka nchini Marekani wakimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza (hayupo pichani)
walitembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa huo.
Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ) na
Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani wakimsikiliza Mkuu wa Kituo
cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William
Kisinza (wa pili kulia) walipowasili kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea
namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza akiwa katika picha
ya pamoja na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa
Kimataifa (ICFJ) na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani mara
baada ya kutembelea kituo hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania
inavyopambana na ugonjwa huo.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO,Tanga)
Na
Eleuteri Mangi-MAELEZO, Tanga
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza duniani kufanya majaribio ya
kupambana na mbu waenezao magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria kwa kutumia
kitambaa kilichowekewa viatilifu ili kudhibiti ugonjwa malaria ambao ni tishio
kwa afya ya wananchi wengi wanaoishi vijijini.
Hatua hiyo ya utafiti imefikiwa na watafiti wa magonjwa ya
binadamu katika cha taifa cha Magojwa ya Binadamu (NIMR) katika kituo cha Amani
mkoani Tanga ili kuweza kuwadhibiti mbu waenezao ugonjwa malaria ambao
unaathiri watu wa rika zote nchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) cha Amani mkoani Tanga Dkt. William Kisinza alipokuwa akiongea
na waandishi wa habari kutoka Kituo cha Waandishi wa Habari wa Kimataifa (ICFJ)
na Taasisi ya “Malaria No More” kutoka nchini Marekani ambao walitembelea kituo
hicho mwishoni mwa wiki kujionea namna Tanzania inavyopambana na ugonjwa huo.
Katika kufanikisha majaribio hayo, Dkt. Kisinza amesema kituo
hicho kinaendelea vizuri na majaribio ambapo wanatarajia mchanganuo wa utafiti
huo utafanyika mwishoni mwa mwaka 2016 na taarifa kamili itatolewa rasmi mwaka
2017 ili iweze kutumika nchi nzima na duniani kote.
Dkt. Kisinza amesema kuwa mafanikio ya taasisi yake yanatokana na
ushirikiano mzuri uliopo na taasisi nyingine za kitaaluma ndani na nje ya nchi.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Chuo Kikuu cha Afya cha Kilimanjaro
(KCMC), Kituo cha Kudhibiti Kuzuia na Magonjwa cha Marekani (CDC), Taasisi
ya Tiba, Dawa na usafi wa mazingira ya London nchini Uingereza (LSHTM) na Chuo
Kikuu cha Brandeis cha nchini Marekani.
Naye Mtafiti Mkuu anayesimamia zoezi la majaribio hayo ya mradi
huo wa vitambaa vyenye viatilifu hivyo vijulikanavyo kama “insecticide treated
wall liners”, Dkt. Joseph Mugasa amesema kuwa zoezi hilo linahusisha vijiji 44,
kaya zaidi ya 25,000 na idadi ya watu wanaonufaika na majaribio hayo ni zaidi
ya 100,000 katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga.
Mbali na kuangalia uwezo wa vitambaa hivyo, mradi huo unaangalia
pia uwezo wa vitambaa hivyo katika kukabiliana na upugufu wa damu kwa watoto
chini ya miaka 11, uwezo wa vitambaa kupambana na mbu sugu kwenye viatilifu
vingine na pia kufanya tathmini ya gharama anazoingia mwananchi katika
kugharamikia tiba za malaria.
Kitambaa hicho ambacho huwekwa kwenye kuta za nyumba kwandani
hutumika sambamba na chandarua ili kuweza kutoa kinga madhubuti mara mbili
kumkinga binadamu dhidi ya mbu waenezao magonjwa.
Mradi huo
wa majaribio wa kutokomeza ugonjwa wa malaria umeanza kufanyiwa utafiti nchini
miaka mtatu iliyopita kuanzia 2013 na unafadhiliwa na Shirika la Misaada la
Marekani (USAID) chini ya Mpango wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na Malaria
(PMI) ambao hadi kukamilika kwake utarajiwa kugharibu zaidi ya Dola za
Kimarekani milioni 3.
Kwa upande wake Meneja wa Mawasiliano Taasisi ya “Malaria No More”
ya nchini Marekani ambaye pia ni Mkuu wa msafara wa waandishi hao Dena Gudaitis
amesema kuwa wamefurahishwa kuona Tanzania ilivyosimama imara kujali afya za
wananchi wake hasa watu wa kipato cha chini ambao wengi wao wanaishi vijijini.
Katika kutekeleza wajibu wao wa kiuandishi, waandishi hao kutoka
ICFJ wanaongozwa na kaulimbiu ya taasisi hiyo inayosema “Andaa mazingira bora
ya mwandishi wa habari wa kimataifa ajaye”.
Waandishi hao wa habari wamefanya ziara ya siku tano nchini
kuanzia Mei 8 hadi 13, 2016 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Tanga
ambapo wametembelea baadhi ya zahanati katika mikoa hiyo, familia zenye watoto
walio chini ya mpango wa majaribio wa kudhibiti malaria, vituo vya utafiti vya
Korogwe na Amani pamoja na kiwanda cha kutengenezea vyandarua cha A to Z cha
jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment