Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akitoa neno la shukrani mjini Morogoro, baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu ijayo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Mali za Serikali, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ezra Msanya, akijibu maswali ya baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa wilaya hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, (wa nne kutoka kushoto) akiungana na wafanyakazi wanaounda Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kuimba wimbo wa mshikamano daima, wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Mjini Morogoro Mwishoni mwa juma. kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika na kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Amina Hamis Shaban.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mkutano uliopitia bajeti ya Wizara hiyo na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akihutubia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo (hawako pichani) mjini Morogoro, ambapo amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kufanyakazi kwa bidii na kuacha mazoea ili kutimiza malengo ya kukusanya mapato na kusimamia matumizi yake kikamilifu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (aliyeketi katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro, mwishoni mwa juma.
Na Benny Mwaipaja, MoF
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo
kuacha kufanyakazi kwa mazoea badala yake waisaidie serikali kutimiza malengo yake ya kukusanya kodi ipasavyo na
kudhibiti matumizi yasiyo na tija ili kuharakisha maendeleo ya nchi
Dkt
Mpango ametoa wito huo mjini Morogoro, wakati akizindua Baraza Jipya la
wafanyakazi wa wizara hiyo khafla iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya B-Z, mjini
humo
Amesema
kuwa jukumu kubwa la wizara hiyo ni kukusanya mapato na kuyasimamia na kuomba
ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wote wa wizara hiyo watimize wajibu wao ili
kufikia malengo hayo
"Kama
kuna jambo muhimu nililokabidhiwa ili kufanikisha kazi yangu ya kuingoza wizara
hii ni rasimali watu wenye ujuzi na waliobobea katika masuala ya sera na
uchumi" Alisema Dkt Mpango
Amewataka
wataalamu hao kuhakikisha kuwa sera zinazotungwa zinakuwa rafiki na
zisibadilike badilike mara kwa mara ili
kuvutia uwekezaji na wawekezaji kuja kuwekeza nchini.
"Msiponisaidia
kusimamia manunuzi ya umma, ukusanyaji wa mapato na kuboresha ushiriki wa sekta
binafsi katika kukuza uchumi wa nchi,
malengo ya serikali ya kuongeza uwezo wa kimapato ili kuihudumia jamii,
yatakwama" alisisitiza Dkt. Mpango
Amesema
kuwa Jamii inahitaji kupata majibu ya uhakika kuhusu masuala mbalimbali
yanayoendelea ikiwemo mfumuko wa bei, matumizi ya dola kwenye soko la ndani,
kuporomoka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola, deni la Taifa, utitiri wa
kodi kwenye mazao ya kilimo, kupungua kwa uingiaji wa kontena bandarini pamoja
na kero nyingine kama vile umeme na maji.
Dkt.
Mpango amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kurejea hotuba iliyotolewa na Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, alipolihutubia Bunge wakati akilizindua Bunge hilo la
11 mjini Dodoma, hotuba ambayo amesema imebeba mambo mazito yanayotakiwa
kufanyiwa kazi ili nchi iweze kusonga mbele kimaendeleo.
"Wananchi
wana imani kubwa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John
Pombe Magufuli, baada ya kuona dhamira yake ya dhati ya kuwatumikia watanzania
wanyonge" aliongeza Dkt Mpango
Akizungumzia
bajeti ya Wizara inayotarajiwa kuwasilishwa Bungeni juma hili, ambayo imepitiwa
na kujadiliwa na Baraza hilo la wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria, Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa matumizi ya kawaida
yamepunguzwa na fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo
Amesema
kuwa ushauri uliotolewa na Baraza la wafanyakazi kuhusu kuboresha bajeti hiyo
kwenye baadhi ya maeneo ameuchukua na ataufanyia kazi
Kwa
upande wao, Manaibu Katibu wakuu, Amina Hamis Shaban na Dorothy Mwanyika,
wamesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango ndio moyo wa nchi na kuahidi kumpa
ushirikiano Waziri wa Fedha na Mipango ili aweze kutimiza malengo yake.
Akizungumza
katika tukio hilo la uzinduzi wa Baraza la wafanyakazi lililokwenda sambamba na
uchaguzi wa viongozi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Dkt. John
Ndunguru, amewataka watanzania, wakiwemo wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na
Mipango, kwenda kuwekeza mkoani mwake katika eneo lililotengwa kwaajili ya viwanda
vya kuongeza thamani ya bidhaa-EPZ.
Aidha,
amesema kuwa mkoa wake umepima viwanja vya makazi ambavyo bei yake imepunguzwa
kwa asilimia 50 ikilinganishwa na bei iliyotangazwa hapo awali na kutoa mfano
wa viwanja vilivyokuwa vikiuzwa kwa bei ya shilingi 10m ambavyo hivi sasa
vinauzwa kwa shilingi milioni 5.
Katika
Mkutano huo, Bw. Cyprian Kuyava alichaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango huku Bi. Faith Didas, akichaguliwa
kuwa Naibu Katibu wa Baraza hilo, ambao watadumu madarakani kwa kipindi cha
miaka mitatu ijayo.
No comments:
Post a Comment