Meneja
utetezi kutoka Oxfam Tanzania Eluka Kibona akitoa maelezo kuhusu
Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kuwa linaendeshwa Tanzania,Nigeria na
Ethiopia ambapo alisema lengo la shindano ni kutambua mchango wa
wanawake katika mapambano dhidi ya umasikini na kuleta uhakika wa
chakula.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Kilimo Paskarina Kayuma akitoa Shukurani kwa Shirika
la Oxfam Tanzania kwa kuendelea kuwanyanyua wanawake katika kilimo na
amewaomba juhudi hizo ziendelee.
Miongoni
mwa majaji Edna Kiogwe mshiriki wa mama Shujaa wa Chakula msimu
uliopita(Kulia) pamoja na Fredy Njeje kutoka Blogs za Mikoa (Kushoto)
wakielezea namna usaili ulivyofanyika mpaka kuwapata washiriki 19 katika
shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu wa tano kwa mwaka 2016
Aliyekuwa
mshiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula msimu uliopita Ester
Kulwa akionesha kanda zote ambazo washiriki wametokea.
Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Shirika la Oxfam kwa
upande wa Tanzania Shamim Mwasha ambaye pia ni Fashion Blogger(wa kwanza
kushoto), Jacob Stephen 'JB' Msanii Maarufu wa Bongo Movie(wa katikati)
na Khadija Mwanamboka wakitangaza majina 19 ya washiriki wa shindano la
Mama shujaa wa chakula 2016 msimu wa tano.
Suhaila Thawer(aliyesimama) ambaye ni 'Public Forum Officer' kutoka Shirika la Oxfam Tanzania akitoa neno la Shukurani
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa pili kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na Majaji,Wafanyakazi wa Oxfam pamoja na Mabalozi
wa Chakula na Kampeni ya Grow
Waliosaidia
katika kupitia Fomu za Mama shujaa wa Chakula kwa hatua ya Mwanzo
kutoka Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Oxfam Tanzania Jane Foster (wa saba kutoka kulia)
Hatimaye 19 watajwa kushiriki
katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa tano kwa mwaka huu 2016,
ambapo fomu 3000 zilizotumwa na wakulima wanawake kote nchini, fomu 1795
zilipitiwa na kuwapata washiriki hao ambao wataanza kutembelewa mmoja mmoja ili
kuhakiki iwapo kile walichokijaza kwenye fomu kinaoana na hali halisi. Mashindano
ya Mama Shujaa wa Chakula 2016, linatarajiwa kufanyika katika kijiji cha
Enguiki kilichopo Monduli mkoani Arusha, kuanzia Septemba 25 hadi Oktoba 16 na
kurushwa katika Runinga ya ITV.
Akizungumza wakati wa kutangaza
majina hayo, mmoja wa majaji wa shindano hilo Jacob Stephen ‘JB’ ambaye ni
muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania alisema katika uchambuzi wa fomu hizo
walikuwa ni wanawake wakulima ambao wanaelimu ya juu na baadhi ya viongozi wa
kisiasa na wale wadogo wadogo.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam
Tanzania Jane Foster alisema shindano hilo limeanza kuendeshwa kuanzia mwaka 2011
na sasa ni msimu wa tano na limefanikiwa kuwaunganisha wanawake wakulima wadogo
wadogo ambao ni asilimia 70 ya wanawake nchini. Alisema majaji wamefanya kazi
ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa mabalozi wa
kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe.
Alisema majaji
wamefanya kazi ya kuchambua fomu hizo na kuwapata washiriki ambao watakuwa
mabalozi wa kuwasilishwa matakwa yao ili changamoto zilizopo zitatuliwe. Aliongeza
kuwa shindano la mama shujaa wa Chakula linaendeshwa katika nchi tatu
Afrika ikiwemo Nigeria, Ethiopia na Tanzania. Ambapo Tanzania wamepita katika
mikoa mbalimbali na kukusanya wanawake wakulima wadogo wadogo ambao tunaamini
kwa kuwa pamoja wanaweza kupaza sauti kwa watunga sera kuhusu changamoto
wanazokutana nazo.
Afisa Uhakiki wa Ubora TBS, Stela
Mroso alisema shirika la viwango nchini liliungana na Oxfam mwaka jana ili
kuhakikisha wanawaleta wanawake pamoja na kutoa elimu zaidi kuhusu kilimo
chenye ubora na mazao yanayoweza kuwa na viwango vya kimataifa. Alisema bila
viwango wanawake hawawezi kufanya biashara, huku akitoa wito kwao kujitokeza
ili kuangalia ubora wa mazao wanayozalisha. Aliongeza kuwa asilimia 80 ya
wanawake nchini wanajishughulisha na Kilimo kwa hiyo ni muhimu chakula
kinachozalishwa kiwe katika ubora na afya pia kiweze kuzaliswa Kimataifa.
Washiriki wa Mama Shujaa wa
Chakula 2016 kuwa ni Betty Nyange (62) Mkoa wa Morogoro, Monica Charles
Mduwile (44) Mkoa wa Dodoma, Neema
Gilbet Uhagile (29) Mkoa wa Njombe, Mary Christopher Lyatuu (29) Mkoa wa
Arusha, Loyce Daudi Mazengo (39)
Mkoa wa Singida, Anjela Chogsasi
Mswete (48) Mkoa wa Iringa, Lucina Sylivester Assey (54) Mkoa wa Shinyanga,
Marta Massesa Nyalama (50) Mkoa wa Kaskazini Unguja, Christina Machumu (42)
Mkoa wa Mara, Happiness Paulo Raulent (35) Mkoa wa Kagera. Mary Bony Soko (42)
Mkoa wa Ruvuma, Mary Ramadhani Mwiru (39) Mkoa wa Kilimanjaro, Mwanaid Alli Abdalla (53) Mkoa wa Mjini
Magharibi, Maria Alfred Mbuya (43) Mkoa wa Mbeya, Eliza Richard Mwansasu (30)
Mkoa wa Rukwa, Mwajibu Hasani Binamu (46) Mkoa wa Mtwara, Eva Haprisoni Sikaponda (40) Mkoa wa
Songwe, Hidaya Said Musa (40) Mkoa wa Tanga na
Mwasiti Salim Mazuri (40) Mkoa wa Dar es salaam Wilaya ya Kinondoni.
No comments:
Post a Comment