Alisema
kuwa sera hiyo itawasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni kabla ya
kupelekwa bungeni hatimaye itapatikana sheria ya kusimamia taasisi ndogo za
fedha-microfinance Act, 2016.
"Serikali
inatambua changamoto ya taasisi binafsi za fedha zinazosumbua wananchi, hivyo
sheria hiyo ikitungwa itasaidia kuondoa matatizo hayo" alisisitiza Dkt.
Kijaji
Naibu
Waziri huyo wa Fedha na Mipango alikuwa akijibu swali lililoulizwa na Mhe. Rahisa
Abdalah Musa (Viti maalumu), aliyetaka kujua serikali ilikuwa na mpango gani wa
kudhibiti utitiri wa taasisi za fedha pamoja na mabenki ili yalete tija kwa
Taifa kwa kuwakopesha wananchi
Akijibu
swali la msingi na maswali ya nyongeza yaliyoulizwa na Mhe. Faida Mohamed Bakar
(Viti maalumu) aliyetaka kujua mikakati ya serikali ya kuanzisha benki ya
wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kuwawezesha kupata huduma bora, Dkt.
Ashatu Kijaji alisema kuwa serikali haina mpango wowote wa kufanya hivyo.
Alisema
kuwa badala yake serikali inafanya jitihada za kuimarisha benki zake zilizopo
ikiwemo Benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya Rasilimali (TIB) ili
kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara wa kada mbalimbali.
"Serikali
imeiboresha kimuundo, Benki ya Rasilimali (TIB) kwa kuunda kampuni tatu
zinazofanyakazi kwa kujitegemea lakini kwa ushirikiano wa karibu"
alisisitiza Dkt. Kijaji
Alizitaja
kampuni hizo kuwa ni TIB Benki ya Maendeleo itakayotoa mikopo ya muda wa kati
na mrefu kwa wafanyabiashara wakubwa na wa kati, TIB Benki ya Biashara
itakayowahudumia wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na TIB Rasilimali
itakayohusika na masuala ya ushauri kwenye Soko la Hisa na Mitaji la Dar es
salaam
"Pamoja
na mambo mengine, kampuni hii inawajibika kuwashauri wafanyabiashara, hususan
wa sekta ndogo ya fedha kupata mitaji kupitia Soko la Hisa la Dar es
salaam" aliongeza Dkt. Kijaji
Dkt.
Kijaji alisema kuwa pamoja na juhudi za serikali za kuboresha benki hizo,
ikiwemo Benki ya Posta, Serikali kupitia Benki Kuu (BOT) inaendelea kuweka
mazingira wezeshi ikiwemo kutunga sheria, kanuni na taratibu za kusaidia nguvu
za wananchi na sekta binafsi kuanzisha benki au taasisi za fedha katika maeneo
yao
"Ni
matarajio yetu kuwa wananchi wanatumia fursa ya mazingira mazuri ya uwekezaji
yaliyopo nchini kuwekeza wao wenyewe au kuzishawishi benki za biashara
kuanzisha huduma za kibenki katika maeneo yao" alisema Dkt. Kijaji
Kuhusu
ombi la mbunge huyo kuitaka serikali iingilie kati masuara ya riba zinazotozwa
na taasisi za fedha na kuwaumiza wananchi, Dkt. Kijaji alisema kuwa serikali
haiwezi kudhibiti wala kuingilia jambo hilo.
Alisema
kuwa Serikali ilijitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za
kifedha tangu mwaka 1991 ili kuruhusu ushindani huru na kuboresha huduma katika
sekta ya fedha hivyo viwango vya riba na mikopo vinavyotozwa na benki hizo na taasisi
nyingine za fedha zinapangwa kutokana na nguvu ya soko.
Dkt
Kijaji alieleza kuwa katika upangaji wa viwango vya tozo na riba mbalimbali
benki na taasisi za fedha huzingatia gharanma za upatikanaji wa fedha,
halikadhalika gharama za uendeshaji na sifa alizonazo mkopaji"Alisisitiza
Dkt Kijaji
Imetolewa
na:
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya
Fedha na Mipango
DODOMA
12/5/2016
No comments:
Post a Comment