Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 November 2016

ESRF YAFANIKISHA MKUTANO WA 5 WA MWAKA, WAJADILI UCHUMI

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)

Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.

Tuesday 29 November 2016

Fw: RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

TIMU YA BUNGE YATUA TANGA KUJIFUA NA MASHINDANO YA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI YATAKAYOFANYIKA KENYA DESEMBA 14


 Mwenyekiti wa timu ya Bunge,William Ngereja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza akizungumzia maandalizi ya timu ya Bunge kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Kenya.

KUTANA NA MTANZANIA WA KWANZA KUPANDA MLIMA EVEREST

Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (Mpaka Basi) akiwa na mgeni wake Ndg Wilfred Moshi wakiwasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar, kutembelea na kujionea shughuli za Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Ndg Wilfred Moshi ni Mtanzania wa Kwanza kupanda Mlima Mkubwa Duniani wa Evarest ukiwa na Mita 8,848, Mtanzania huyo Ndg Wilfred Moshi amepanda mlima huo mwaka 2012. akiwa ni Mwaafrika wa Tatu kupanda mlima huo na mwafrika wa Pili mweusi kupanda mlima huo Duniani kwa ukubwa.

MADAKTARI NCHINI WAMETAKIWA KUITISHA MIKUTANO YA KIJAMII ILI KUJADILI MAGONJWA


Katibu Mtendaji wa Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA), Fabian Magoma  (kulia), akizungumza katika Kongamano la 33 la siku tano la Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) linaloendelea Hoteli ya Kebby Mwenge jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni  Mwenyekiti wa TPHA anayemaliza muda wake, Daktari Bingwa  Elihuruma Nangawe.

UN NA EU WAENDELEZA KAMPENI YA UELEWA WA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Moblog)

WANANCHI WA KITARAKA SINGIDA WAOMBA MAENEO YA UKULIMA NA UFUGAJI

Wananchi wa Kata ya Kitaraka iliyopo katika Halmashauri ya Itigi, Wilaya ya Manyoni, Mkoani Singida, wamemuomba Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. William Ole Nasha, kuwapatia shamba linalomilikiwa na Serikali la Tanganyika Packers, ambalo Serikali imeacha kulitumia kwa zaidi ya miaka 20, ili walitumie kwa shughuli za Kilimo na Ufugaji.

RC SINGIDA AAHIDI KUREJESHA SHAMBA LA SAGARA LENYE EKARI ZAIDI YA ELFU TANO KWA WANANCHI.

Gari la Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe likisukumwa na wananchi wa kijiji cha Sagara baada ya kushusha neema kwa wakazi hao kwa kitendo cha kuwamilikisha shamba la ekari 5,430. Wananchi hao kwa miaka mingi wamekuwa wakitozwa shilingi elfu 30 kwa ekari moja katika msimu wa kilimo. Ushuru huo kwa msimu huu ulipandishwa hadi shilingi 40,000 kwa ekari. Kwa sasa hawatalipa tozo hilo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA ZAMBIA EDGAR CHAGWA LUNGU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Zambia Edgar Chagwa Lungu Ikulu jijini Dar es Salaam.

TANGA YAWATAKA WAWEKEZAJI KUTOKA NCHINI INDIA KUWEKEZA ILI KUWEZA KUNUFAIKA NA FURSA ZILIZOPO


Balozi wa India nchini Tanzania ,Sandeep Arya kushoto akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Thobias Mwilapwa wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa pili kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi.

Monday 28 November 2016

NYUMBA YA KISASA INAUZWA IPO JIRANI NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM CHAMAZI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM







Mwonekano wa Mbele wa nyumba hiyo.

NYUMBA INAUZWA IPO WILAYA YA TEMEKE KATA YA CHAMAZI KARIBU NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM NI SEIF CONTAINED NA INA MASTER ROOM NA CHUMBA KIMOJA CHA KULALA, SEBURE, JIKO NA CHOO NA BAFU LA NDANI, BEI NI SHILINGI MILIONI 19 KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA 0687-347676 AU O759-239338. 

RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI HUMO

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto

UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KAZI ZA CCM

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida (kushoto), akimkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,  Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano ya Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China, Jia Bo,  Dar es Salaam leo asubuhi, ambaye yupo nchini na wajumbe wenzake sita kwa zaiara ya siku saba ya kichama kukitembelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI DIRA TV


Friday 25 November 2016

SIMBACHAWENE AAGIZA FEDHA ZILIZOTOLEWA KWA KAYA ZISIZOKUWA NA SIFA KATIKA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI KUREJESHWA



Na Rebecca Kwandu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene ameziagiza Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya kuhakikisha kuwa fedha zilizotolewa kwa kaya zisizokuwa na sifa katika Mpango wa kunusuru kaya maskini unaofanywa kwa uratibu wa  Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF)  kurejeshwa ili ziweze kuwanufaisha walengwa.

MTANZANIA VICTORIA MWANZIVA ASHIRIKI KOZI MAALUM YA WANAWAKE KWA AJILI YA KUDUMISHA AMANI BARANI AFRIKA, ADDIS ABABA ETHIOPIA

Bi. Victoria Mwanziva (kulia) akitoa mchango wake katika kozi maalum kwa wanawake  kwa ajili ya kudumisha Amani Barani Afrika

KIKOSI KAZI CHAMALIZA KAZI YA KUANDAA MPANGO KAZI WA MATUMIZI YA ARDHI NA KINATARAJIA KUWASILISHA TAARIFA KWA WAZIRI WA ARDHI MH. LUKUVI

 Kikosi kazi katika mkutano wa siku mbili uliofanyika Morogoro

WAZIRI MWIGULLU AWAONYA MADEREVA WANAOACHA MITI NA MAWE BARABARANI

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigullu Lameck Nchemba akiwa katika kikao cha 38 cha bodi ya barabara ya Mkoa wa Singida.

BODI YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA KUPITIA UPYA MIKATABA YA UWEKEZAJI YA SHIRIKA HILO


Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania, Dk. Haruni Kondo (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu kuipitia upya mikataba iliyoingia shirika hilo na Taasisi mbalimbali na watu binafsi kutokana na baadhi yake kugundulika ikiwa na utata wa maslahi ya shirika hilo. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga na Kulia ni Katibu wa Shirika, Rochus Assenga. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)

WAFANYABIASHARA MKOANI SINGIDA WAJIPATIA BILIONI 1.8 KWA MAUZO YA KUKU

Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata.

WAFANYABIASHARA MKOANI SINGIDA WAJIPATIA BILIONI 1.8 KWA MAUZO YA KUKU

Mwenyekiti wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiongoza kikao hicho, kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dokta Angelina Mageni Lutambi, wa kwanza kulia ni Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Lameck Nchemba na anayefuata ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata.

Wednesday 23 November 2016

SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA KILA MWAKA NCHINI NZIMA

Naibu Waziri wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Suleiman Jaffo akikagua kitabu cha Risiti kulia anayemwangalia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Sabas Chambasi

ESRF YASHIRIKIANA NA GETENERGY KUANDAA MKUTANO WA AFRIKA WA MAFUTA NA GESI


Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) imeshirikiana na kampuni ya Getenrgy kuandaa mkutano wa Afrika wa Mafuta na Gesi (GETENERGY VTEC AFRICA 2016) ambao unafanyika nchini kwa siku tatu kuanzia Novemba, 21-23, 2016.

WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 WAANZA KAMBI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications L.T.D,Maria Sarungi Tsehai (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,kuhusu kuanza kambi kwa warembo wa Miss Universe Tanzania 2016 ambapo fainali itafanyika Novemba 25 katika Hoteli ya Collessium iliyopo Oysterbay. Kulia ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Collessium,Mustafa Dhanji na Mratibu wa shindano hilo,Mwanakombo Salim.(PICHA NA ELISA SHUNDA)

WAZIRI MBARAWA ATEMBELEA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME - TEMESA



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu akieleza utendaji kazi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alipotembelea Wakala huo, jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamini Sawe-Maelezo)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MZEE ALI HASSAN MWINYI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA MAHAKAMA YA AFRIKA MJINI ARUSHA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika.

SERIKALI: MAOFISA MIPANGO, MAENDELEO YA JAMII FANYENI KAZI KWA UZALENDO

Mkurugenzi Msaidizi wa Fedha na Mipango, Servus Sagday akielezea madhumuni ya warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG's) kwa Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini iliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua warsha hiyo inayoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa mikutano Hazina ndogo.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Miriam Mmbaga amewataka maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Mipango nchini kufanya kazi kwa uzalendo ili Tanzania iweze kufikia malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) ifikapo mwaka 2030 kama ilivyokusudiwa.

HOW UZIKWASA CONTRIBUTES TO THE 16 DAYS OF ACTIVISM AGAINST GENDER VIOLENCE IN PANGANI

November 25th is the International Day for the elimination of Violence against women in the world. The 16 days up to December 10th the Human Rights Day is a period of global activism dedicated to fight gender violence in all settings.
UZIKWASA, an organization based in Pangani, Tanzania has become known for its innovative interventions that encourage a voice among rural communities and the development of capable grass roots leaders who are committed to fight gender rights violations in Pangani.
UZIKWASA’s multimedia work that has addressed violence against women and girls (VAWG) includes:
-Pangani FM radio programs
*Leadership that Touches (UongoziwaMguso)
*Womens’ Voice (Sauti ya Mwanamke)
-Feature films
*Fimboya Baba (Father’s Stick: Early and forced marriage)
*Chukua Pipi (Sweet deceit, sexual abuse of school children)
*AISHA (Gang rape)
-Comic books
* Varangati
*Halafu series
*AISHA book
-Forum Theatre and Theatre for Development
-A series of TV spots
On December 2 UZIKWASA will participate in the 16 days of activism by launching theMinna Dada Day, abig bang event to create awareness on VAWGin Pangani District.The campaign is designed to start a deep reflection process among the Pangani people and their leaders about atrocities committed against women and girls including Intimate Partner violence.
Minna dada introductory TV Spot

The following four “Minna Dada” TV spots paint a picture of how intimate partner violence affects the lives of local Pangani women. Cinema Zetu of AZAM TV will broadcast the four spots during the next four months.

Tuesday 22 November 2016

WASTAAFU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KULIPWA MWEZI MMOJA MMOJA

Wastaafu mbalimbali wakiwa kwenye foleni kusubiri zamu yao ya kuhakikiwa jijini Dodoma.

SERIKALI imesema kuwa itaendelea na utaratibu wa kuwalipa wastaafu wanaohudumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, pensheni yao kila mwezi kwa mujibu wa sharia ya mafao ya wastaafu Na. 371 badala ya kuwalipa malipo hayo kila baada ya miezi mitatu.

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YAHAKIKI WASTAAFU MKOANI DODOMA

Mkaguzi  wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Stanslaus Mpembe akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango, mkoani Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JENERALI FAN CHANGLONG MAKAMU MWENYEKITI WA KAMISHENI KUU YA ULINZI YA JESHI LA UKOMBOZILA WATU WA CHINA (PLA)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

MZAZI WA DENI LA 300,000 ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PASIPO MASHARTI YOYOTE

Mzazi Sakina Lembo

Na Dotto Mwaibale

MZAZI Sakina Lembo (26) mkazi wa Mbagala Kibonde Maji ambaye alizuiliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  (MNH), kutokana na deni la sh. 338,257 baada ya kufanyiwa oparesheni ya uzazi uongozi wa hospitali hiyo umemruhusu kuondoka bila ya masharti yoyote.

PRECISION AIR YAANZA SAFARI KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI.

Ndege aina ya ATR namba 5H-PWE mali ya Shirika la ndege la Precision Air ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa ndege uliopo ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa na wageni 45 kutoka nchini Afrika Kusini waliofika nchini kwa ajili ya shughul za utalii.

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATANGAZA OFA YA KRISMAS YA SMARTPHONE

 Ofisa Mkuu wa Biashara wa Kampuni ya Simu ya Tigo,  Shavkat Berdiev (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kutangaza ofa ya Krismas ya Smartphone. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo, William Mpinga.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA GESI NA MAFUTA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa mkutano wa masuala ya soko la Gesi na Mafuta uliofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

MALINZI AMLILIA SHEKIONDO

Rais wa  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), Jamal Malinzi, amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club, Yussuf Manji kutokana na kifo cha Makamu Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Isaac Shekiondo ‘Clinton’.

HUU NDIO UAMUZI WA KAMATI YA SAA 72 YA UENDESHAJI NA USIMAMIZI WA LIGI

Uchunguzi dhidi ya waamuzi Martin Saanya, Samuel Mpenzu (mechi ya Yanga Vs Simba), Thomas Mkombozi (mechi ya Coastal Union Vs KMC) na Rajab Mrope (mechi ya Mbeya City na Yanga) umekaribia kukamilika.

Hatua ya mwisho ya uchunguzi huo ni wao kufika mbele ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ambapo watahojiwa ili kutoa ufafanuzi katika masuala mbalimbali yaliyojitokeza katika taarifa zao.

MKUU WA MKOA DAR AFANYA ZIARA AZAM FC, AIPONGEZA KWA UWEKEZAJI

Meza kuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kushoto kwake Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyanivana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, Makamu Mwenyekiti, Nassor Idrissa na Ofisa Habari, Jaffary Idd.

By Abducado Emmanuel
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Paul Makonda, leo mchana amefanya ziara kwenye Makao Makuu wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC akiwa na lengo kuu la kuipongeza kutokana na juhudi kubwa wanazofanya za kuwekeza katika soka la Tanzania.

TIGO 'YAIPIGA TAFU' HOSPITALI YA WILAYA YA ILEJE


Mkurugenzi wa Kampuni ya simu za mkononi, Tigo-Tanzania,  Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson Kiswaga, (kulia) akizungumza na wananchi wa Itumba Wilaya ya Ileje, waliofika kwa ajili ya kushudia msaada waliopatiwa kutoka Tigo-Tanzania kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya hiyo, kwa niaba ya kampuni hiyo. Tigo ilikabidhi vifaa vya afya hospitalini hapo ambavyo ni mashuka, mablanketi, Goves, Jokofu na mifagio ambavyo vinagharimu kiasi cha Sh20 Milioni.

Sunday 20 November 2016

WANANCHI WASHAURIWA KUENDELEA KUPIMA AFYA ZAO, UKIMWI BADO NI TISHIO

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa  kupima afya zao na kupatiwa matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai. 

10 WAFUZU MAJARIBIO AZAM FC U-17 MBEYA


By Abducado Emmanuel
VIJANA 10 wenye umri chini ya miaka 17, wamefanikiwa kuchaguliwa kwenye majaribio ya wazi yaliyoendeshwa na Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, jana Jumamosi katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.                 
Huo ni mwendelezo wa mpango wa mabingwa hao wa kutengeneza timu bora ya vijana wa umri huo kwa ajili ya kuwatumia kwa miaka ijayo na wengine kunufaika nao kwa kuwauza.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA ZIFF AZINDUA TAMASHA LA UONESHAJI FILAMU BURE MKOANI GEITA

Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI ILI KUHARAKISHA MAENDELEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, (aliyevaa joho jekundu), akiwa nje ya Ofisi Kuu ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar es salaam, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo hicho ambapo wahitimu 154 kutoka nchi nane Barani Afrika wametunukiwa Astashahada na Shahada za Takwimu Rasmi zinazotolewa na chuo hicho.

NDEREMO,VIFIJO VYATAWALA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA TUMAINI DAR


 Wanafunzi waliohitimu na kutunukiwa Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Biashara wakishangilia wakati wa Mahafali ya 10 ya  Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Dar es Salaam Tudarco yaliyofanyika leo Mwenge, Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick  Shoo, alitunuku  jumla ya wahitimu 733. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG}

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA ATUNUKU SHAHADA NA STASHAHADA KATIKA MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA

Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu tayari kwa mahafali.

WANATASNIA YA FILAMU MKOANI GEITA WAPEWA MTIHANI WA KUANDAA TAMASHA LA FILAMU

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fesso (kushoto), akizungumza kwenye kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita hii leo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita. Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, aliyewakilishwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Mahmood Thabith Kombo (wa pili kushoto). Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti Chama cha Waigizaji mkoani Geita, Rosemary Michael na anayefuata ni Herman Matemu ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita.

Friday 18 November 2016

WAZIRI SIMBACHAWENE AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI NA MAADILI YA VIJANA WAZALENDO 47 KIVUKONI JIJINI DAR ES ESALAAM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene, akisalimiana na Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, baada ya kuwasili Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kufunga mafunzo ya uongozi na maadili ya vijana wazalendo 47 yalifungwa chuoni hapo Dar es Salaam leo. Kulia ni Samuel Kasori, aliyekuwa Msaidizi wa Hayati Baba wa Taifa ambaye alipata fursa ya kuzungumza katika hafla hiyo kuhusu suala zima la maadili ya uongozi na uzalendo.