Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 31 May 2014

BABA MZAZI WA SERGIO AGUERO ADAI MWANAYE ANAPENDA KWENDA BARCELONA

Star: Aguero scored 28 goals in 34 games last season as Man City won the Premier League and League Cup
BABA mzazi wa Sergio Aguero ameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Manchester City anapenda kujiunga na Barcelona na  vyombo vya habari nchini Hispania vimeripoti kuwa wababe hao wa Katalunya wanajiandaa kuweka mezani ofa ya paundi milioni 31.
Barcelona wapo tayari kufikia paundi milioni 47 ili kuinasa saini ya nyota huyo wa kimataifa wa Argentina kama Man City watakataa ofa yao ya kwanza.
Lakini kocha mpya wa Barcelona, Luis Enrique ameripotiwa kuvutiwa zaidi na Aguero na yuko tayari kumwaga kitita kirefu cha fedha kama Man City watakataa., hii ni kutokana na mtandao wa michezo wa Hispania.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

CHANZO FULL SHANGWE

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KATIKA KAMBI YA KIKOSI CHA JESHI LA KUJENGA TAIFA RUVU

001 (2)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohameed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, wakati alipofika kwenye Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo, ambapo jumla ya miti 8,000, imeandaliwa kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
2 (6)Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza, akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
01 (5)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiumwagia maji mti alioupanda katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
3 (5)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la msingi baada ya kupanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
4 (4)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi wa kambi ya JKT Ruvu baada ya kupanda miti. Picha na OMR
5 (1)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo, baada ya kupanda miti. Picha na OMR
22W


CHANZO FULL SHANGWE

SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA

DSC_0473Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
DSC_0429Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
DSC_0446
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
“Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia”,amesema Kinana.
DSC_0453Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
DSC_0463Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.

CHANZO FULL SHANGWE

ACADEMIE TCHITE YAISHIKISHA ADABU AL-MERREIKH, MBEYA CITY FC JIONI HII KUWASHIANA MOTO NA VICTORIA UNIVERSITY

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WENYEJI wa michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Al-Merreikh ya Sudan wametupwa nje ya michuano hiyo kwa penati 3-2 baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Merreikh ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza dakika ya 4 kupitia kwa Agab Ramadan, lakini dakika ya 22 Academie wakasawazisha kupitia kwa Manishimwe Alain na matokeo hayo yalidumu mpaka dakika ya 90 na mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati.
Wachezaji wa Al-Merreikh waliokosa penati ni Amir Kamal, Wawa Pascal na 
Tia Togbi Olivier. Waliofunga ni Only Sadjo Haman na Elbasha Ahmed.
Vijana wa Academie waliofunga penati jana ni Ngando Omar, Barampanze Shaban na Manishimwe Alain. Mlinda mlango wa Academie Sonzera Anslem ndiye alikuwa nyota wa mchezo huo.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
CHANZO FULL SHANGWE

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI

msangiTAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 31.05.2014.
  • MWANAMKE MMOJA AUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NA MUME WAKE.
  • MTU MMOJA AUAWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWA TUHUMA ZA WIZI.
  • MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AFARIKI DUNIA BAADA YA KUDONDOKA NA KISHA KUKANYAGWA NA POWERTILLER.
  • MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WANNE KUTOKANA NA TUHUMA MBALIMBALI.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHRISTINA HAYOLA (35) MKAZI WA KIJIJI CHA LIWALANJE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI, KIFUANI NA MGUU WA KULIA  NA MUME  WAKE AITWAYE MUSSA NSAGAJE @ MWAULAMBO.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAGAMBA, KATA YA ISANZA, TARAFA YA IGAMBA, WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI UGOMVI ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI ULIOTOKEA WAKIWA KILABUNI USIKU.
 MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ABDI SANGA (20) MKAZI WA ISANGA ALIUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE  NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO, MAWE NA RUNGU.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 03:45 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO ENEO LA FOREST YA ZAMANI KATA YA FOREST, TARAFA YA  SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA  MAREHEMU NA MWENZAKE MMOJA AMBAYE ALIFANIKIWA KUKIMBIA KUINGIA NYUMBANI KWA KASSIM ISSA (28)  MKAZI WA FOREST NA KUIBA VITENGE VYENYE THAMANI YA  TSHS 70,000/=,  MHANGA ALIPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA, HIVYO KUNDI LA WATU WALIJITOKEZA NA KUMSHAMBULIA. 
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA INA MADHARA MAKUBWA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
 KATIKA TUKIO LA TATU:
 MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU KATIKA SHULE YA MSINGI IBUMILA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA FATINA FESTO @ MWANDOSYA (12) MKAZI WA KIJIJI CHA MAHONGOLE ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA  KUDONDOKA KUTOKA  KWENYE POWER TILLER ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA AIZACK MWASHANGWA (22) MKAZI WA MAHONGOLE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA IBUMILA-MAHONGOLE, KATA YA SONGWE-IMALILO, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU NA WENZAKE WALIKUWA WANATOKA KUVUNA MPUNGA WA SHULE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA KUACHA POWER TILLER MARA BAADA YA TUKIO.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MAKONGOLOSI ALIYEMBALIWA KWA JINA LA ADEN PETER @NGOMBE (17) MKAZI WA MAKONGOLOSI AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.117 APK/T.150 AVM AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE ALLY MOSHI (35) MKAZI WA MBARALI.
TUKIO HILO LA AJALI LIMETOKEA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MAKONGOLOSI/LUPA. CHANZO CHA AJALI DEREVA ALIKUWA AMELEWAPOMBE. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI – MAKONGOLOSI.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WATUMIAPO VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUFUATA NA KUZINGATIA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI IKIWA NI PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO VYA KUVUKIA ILI KUEPUKA AJALI
TAARIFA YA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MWIYULEGHE MBUGHI (60) MKAZI WA KIJIJI CHA ITENTULA AKIWA ANAMILIKI BILA KIBALI SILAHA /BASTOLA MOJA AINA YA   BABY YENYE NAMBA 946663 ILIYOTENGENEZWA NCHINI UBELGIJI IKIWA NA RISASI TATU [03] KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00 USIKU WA KUAMKIA LEO HUKO KATIKA KIJIJI CHA ITENTULA, KATA YA   BARA, TARAFA YA ITAKA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA ALIKUWA AMEKUFICHA SILAHA HIYO CHUMBANI NDANI YA   NYUMBA YAKE. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA KWA JAMII KUACHA KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZA UMILIKAJI WA SILAHA KIHALALI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DEZDERIS JACKSON (30) MKAZI WA KIJIJI CHA SAZA AKIWA NA KETE 17 ZA BHANGI KWENYE KIBANDA CHA KUUZA SABUNI SAWA NA UZITO WA GRAM 85.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA SAZA, KATA YA   MKWAJUNI,   TARAFA YA   KWIMBA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA TATU:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA WILSON (23) MKAZI WA KIJIJI CHA BWAWANI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA  POMBE KALI ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI[VIROBA] AINA YA  BOSS PAKETI 51.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI NA KIJIJI CHA BWAWANI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA   KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA WAFANYABIASHARA KUACHA KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUKUFU NA SERIKALI KWANI ZINA MADHARA KIAFYA KWA WATUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA NNE:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ESTER MWALUGAJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA MAMBA-F ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA   POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA MBILI [02].
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 30.05.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MTANDE, KIJIJI CHA MAMBA -F, KATA YA   MAMBA, TARAFA YA   KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

            KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOJIHUSISHA NA MTENGENEZAJI NA UUZAJI WA POMBE HARAMU YA MOSHI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
CHANZO FULL SHANGWE