Takriban wapiganaji 30 wanaounga mkono Urusi,wameuawa
katika mapigano yaliyozuka katika uwanja wa ndege mjini
Donetsk,Mashariki mwa Ukraine.
Mapigano yalizuka baada ya wapiganaji hao waliokuwa wamejihami wakiunga mkono kujitenga kwa mji wa Donetsk kutoka kwa UkraineWapiganaji hao walijaribu kuuteka uwanja huo mnamo siku ya Jumatatu.
Waandishi wa BBC walio karibu na uwanja huo wanasema walisikia milio ya risasi hata baada ya mashambulizi na ufyatulianaji wa risasi ingawa msemaji wa jeshi alisema kuwa hali ilikuwa imetulia.
Rais mpya Petro Poroshenko aliahidi Jumatatu kuwa operesheni dhidi ya makundi ya kile alichoita magaidi itakamilika baada ya saa chache wala sio miezi.
Mwakilishi wa mji wa Donetsk ambao tayari umejitangza kuwa taifa, aliambia BBC kuwa taarifa ya vifo vya watu 30 ni za kweli.
Waziri wa mambo ya ndani Arsen Avakov, amesema kuwa hapakuwa na majeruhi upande wa wanajeshi wa Ukraine.
Makabiliano yaliyozuka Jumatatu, yalianza baada ya wapiganaji wanaotaka kujitenga na Ukraine kuvamia uwanja wa ndege wa Sergei Prokofiev Donetsk mapema asubuhi.
Wakati huohuo,maafisa wa Ukraine wamedhibiti uwanja wa ndege mjini Donetsk mashariki mwa nchi hiyo huku idadi kubwa ya watu wakifariki. Hata hivyo, wandishi wa BBC walio nje ya kambi ya jeshi wanasikia milio ya risasi
Siku moja tu baada ya ushindi wa Rais mpya Petro Poroshenko, hali ya suitofahamu bado inaenea Mashariki mwa Ukraine.
Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa operesheni dhidi ya wapiganaji hao itaendelea huku walinzi wa mipakani wakisema kuwa magari yenye wapiganaji wa Ukraine.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment