Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday, 31 May 2014

DA' JOY 'CHALI' MALAWI, PETER MUTHARIKA NDIYE RAIS MPYA

Rais wa Malawi aliyeanguka vibaya, Joyce Banda 'Da Joy'
Rais mpya wa Malawi, Peter Mutharika, akipunga mkono.

Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2 na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7.
Matokeo ya kura hizo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Malawi, yanaonyesha kwamba, Chama cha DPP kimepata kura 1,904,399 kikifuatiwa na MCP (kura 1,455,880) na PP (kura 1,056,230).
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .

Kesi Mahakamani
Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.
Na kwamba sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.

Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.

BBC

No comments:

Post a Comment