Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 30 May 2014

KAMBI RASMI YA UPINZANI YASUSIA BAJETI YA NISHATI

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Dodoma

WABUNGE wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakiongozwa na mkuu wa kambi hiyo Freeman Mbowe, leo wametoka nje wakisusia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Pamoja na jitihada za kuombwa wabaki, wabunge hao waligoma na kutoka nje huku wengine wakipiga kelele kwamba wamechoka kuburuzwa.
Akizungumza na wanahabari baada ya kutoka nje, Mbowe alisema sababu zilizowatoa nje ni mjadala wa bajeti hiyo kupewa muda mfupi wakati kuna masuala mengi tata yanayohitaji kujadiliwa kwa kina.
Alisema wanaamini kuna njama na michezo michafu inayoendelea katika wizara hiyo pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambalo linakabiliwa na tuhuma kadhaa zisizo na majibu.
"Hatuwezi kuendelea kuzungumzia bajeti ya Serikali isiyokuwa na sera, mimi kama kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni siwezi kuendelea kuiongoza kambi inayoburuzwa," amesema Mbowe na kuongeza: "Tunawaachia bungeni lenu mpitishe bajeti yenu ili siku zijazo mkutane na hasira za wananchi,kwakuwa haya mlishayapanga".
Hata hivyo, amesema kesho wataingia Bungeni kuendelea na vikao kama kawaida.
Awali akichangia mjadala huo, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) David Kafulila, alicharuka tena akitaka serikali itoe majibu kuhusiana na uchotwaji wa Shs. 200 bilioni katika akaunti ya Escrow iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na kampuni ya kufua umeme kutoka Malaysia, IPTL.
Kafulila ndiye aliyeibua tuhuma hizo Mei 8, mwaka huu katika kikao hicho wakati alipowatuhumu mawaziri wawili kwamba ndio waliohusika na uchotwaji wa fedha hizo.
Mbali ya mawaziri hao ambao hakuwataja majina, Kafulila pia aliwaunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwemo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.
Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Ingawa Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na AG ni Frederick Werema.
Kafulila alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.
Mbunge huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.
“Pamoja na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya Escrow,” alisema.
Mbunge huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004 na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema Kafulila.
Alisema fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.
Alitaka jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake na pia Waziri wa Fedha.
Alisema wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki hata kidogo.
Kafulila alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.
Alisema fedha hizo hazikupaswa kuchukuliwa kwa kuwa kulifanyika udanganyifu mkubwa kwamba PAP ilikuwa imenunua IPTL wakati jambo hilo si la kweli.
Alisema IPTL ilikuwa na makubaliano ya kufanya kazi kwa kampuni mbili ambazo ni VIP Engineering ya Tanzania iliyokuwa na hisa asilimia 30 na Mecmer ambayo ilikuwa na asilimia 70 ya hisa.
Hata hivyo, alidai kuwa anao ushahidi kuwa PAP ilikuwa imenunua hisa za VIP na hakukuwa na vielelezo vya kununua Mecmer kwa kuwa kampuni hiyo tayari ilishapoteza uhalali wake kwa kuwa ilikuwa chini ya muflisi nchini Malaysia.
Aliliambia Bunge kuwa wakati wa uchukuaji wa fedha hizo kutoka BoT, ilipaswa kulipiwa kodi lakini zilichukuliwa kinyemela bila hata ya kulipiwa kodi.

CREDIT: NYONGEZA KUTOKA MWANANCHI

No comments:

Post a Comment