KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
SAID RUBEYA, SWALEHE MADJAPA, USTADH M. HASSAN,
JACKSON J. SAGONGE & VALENTINE NYALU………………..……….. Waweka Pingamizi
DHIDI
MICHAEL RICHARD WAMBURA……………………………..………… Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka
Pingamizi waliotajwa hapo juu, ambao ni wanachama wa Simba Sports Club
wamemwekea pingamizi Mwekewa Pingamizi hapo juu kwa hoja zifuatazo:
i.
Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club mahakamani
katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3),
na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya Mwaka 2010.
ii.
Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji
ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na barua ya tarehe 6
Mei 2010, (Kumb. Na. SSC/MMKT/163/VOL.40/11) na hivyo basi anapoteza
haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club
iii.
Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa kuipeleka
Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.
iv. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni
v. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
vi. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
vii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.
Nakala
ya mapingamizi hayo na mwaliko wa kikao cha kusikiliza pingamizi
valikabidhiwa kwa mwekewa pingamizi tarehe 23 Mei 2014. Siku ya
kusikiliza Pingamizi, tarehe 25 Mei 2014, Mwekewa pingamizi aliwasilisha
mbele ya kamati ya uchaguzi “preliminary objections” mbili kama
ifuatavyo:
i. Dhidi ya waweka pingamizi wote watano(ona kiambatanisho “A”)
ii. Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba (ona kiambatanisho “B”)
Kabla
ya kuanza kusikiliza mapingamizi ya waweka pingamizi, kamati
ilisikiliza “preliminary objections” na kutoa maamuzi kama ifuatavyo.
Mosi,
“preliminary objections” dhidi ya wagombea watano (5), kimsingi ni
majibu ya pingamizi toka kwa ya wakewa pingamizi, hivyo basi, hoja hizo
zitapata fursa wakati mwekewa pingamizi anajibu hoja za waweka
pingamizi.
Pili, “preliminary objections” dhidi ya kamati zinatupiliwa mbali kwa misingi ifuatavyo;
a.
Uteuzi wa katibu wa kamati ya uchaguzi samba sports club
ulifanywa na kamati ya utendaji ambayo mweka “prelimary objections”
alihudhuria.
b. Kamati imeamua kuazima na kutumia
kanuni za uchaguzi za TFF kwasababu Kamati ya utendaji Simba haijaandaa
kanuni hizo.
c. Unapoazima na kutumia kanuni za
Mamlaka nyingine sio lazima uzitumie kama zilivyo, una uhuru wa kufanya
maboresha ili kuzingatia hali halisi ya Simba Sports Club.
d.
Pingamizi dhidi ya Bw. Evans Aveva ni malalamiko ya kawaida
ambayo Kamati inabidi iyazingatie kwa wakati wake na sio sehemu ya
mapingamizi kwasababu muda wa pingamizi umekwisha.
e. Kanuni hazielezi haki ya kuweka “preliminary objections”, lakini kamati ilitumia busara kuzisikiliza.
Hivyo basi kamati ilitupilia mbali “prelimary objections” na kusikiliza pingamizi katika mfumo wa kawaida.
Kamati,
awali ya yote, ilichambua masuala ya kimaadili na kuamua kuwa mambo
hayo ya kimaadili, yapelekwe katika kamati ya maadili ya TFF na waweka
pingamizi wenyewe. Mambo ya kupelekwa kamati ya maadili ni:
i. Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
ii. Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
iii. Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.
Kamati ilijadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi yafuatayo:
i. Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni.
Kamati
ilikwisha toa adhabu ya ONYO KALI dhidi ya Mwekewa Pingamizi kuhusu
kuanza kampeni kabla ya wakati, hivyo basi hawezi kuadhibiwa mara mbili
kwa kosa ambalo ameshaadhibiwa.
ii.
Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club
katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3),
na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya Mwaka 2010.
Ushahidi
uliotolewa mbele ya kamati unaonyesha kuwa Mwekewa pingamizi alifungua
kesi No. 100/2010 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Simba
Sports Club katika masuala ambayo hayapaswi kwenda mahakamani. Kitendo
hicho ni ukiukwaji wa Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba
ya Simba ya Mwaka 2010.
iii.
Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya
Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na hivyo basi anapoteza
haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club.
Kamati
imepokea ushahidi na kuridhika kuwa tarehe 5 Mei 2010, kupitia kikao
halali kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ilimsimamisha Uanachama
Mwekewa Pingamizi kwa tuhuma za kuipeleka Simba Mahakamani katika kesi
tajwa. Baada ya kusimaishwa uanachama na kamati ya utendaji kwa mujibu
wa Ibara 12(1),(2) & (3) ya katiba ya Simba mwaka 2010, jambo hilo
lilipaswa kupelekwa katika mkutano mkuu ili mkutano mkuu, utoe adhabu
au utoe msamaha. Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Ibara ya 55, adhabu ya
kosa hilo ni kufukuzwa uanachama. Si kamati ya utendaji wala Mwekewa
Pingamizi aliyepeleka suala hili katika mkutano mkuu ili litolewe
uamuzi.
Kamati imepokea barua tatu, toka kwa
Mwekewa Pingamizi, kuhusu uanachama wake Simba Sports Club. Barua ya
kwanza iliandikwa tarehe 6 Novemba 2012 toka kwa Bw. Michael Wambura
kwenda kwa Mwenyekiti wa Simba. Barua hiyo inakiri kosa la kuipeleka
Simba makahamani na kuahidi kuwa hatarudia tena. Barua ya pili toka kwa
Mwenyekiti wa Simba ya tarehe 15/09/2012, Ref. No. SSL/20/9/12, kukiri
kupokea barua toka kwa Bw. Michael Wambura na kuahidi kuwa suala hilo
litafanyiwa kazi, ingawa kamati ilibaini kuwa barua ya kujibu imeandikwa
takribani miezi miwili kabla ya ile ya awali jambo ambalo haliwezekani.
Barua ya tatu ni ya tarehe 25/9/1012, kumb. SSC 28/9/12 ambayo inasema
samba haina tatizo na Bw. Michael Wambura, lakini Uhalali wa Barua hiyo
unashaka kubwa sana kiasi cha kamati kuamua ipelekwe kwenye mamlaka
husika kwa hatua zaidi.
Hivyo
basi kamati imejiridhisha kuwa maamuzi ya Kamati ya utendaji ya tarehe 5
Mei 2010 ya kumsimamisha Mwekewa Pingamizi bado yanaendelea na yana
nguvu za kisheria kwasababu hakuna maamuzi yoyote ya Mkutano Mkuu
kubatilisha hatua hiyo.
Mwananchama ambaye
amesimamishwa uananchama hana haki ya kushiriki katika shughuli za simba
kwa mujibu wa Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010 na
Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2014.
iv.
Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na
FIFA kwa kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba
100/2010.
Kamati inapenda kurejea maamuzi yake hapo juu katika suala ka kwenda mahakamani kwa masuala ya Soka.
Hivyo
basi Muwekewa Pingamizi, Bw. Michael Richard Wambura ameondolewa katika
mchakato wa Uchaguzi, kwa sababu zilizotajwa hapo juu.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
GEOFREY NYANGE (KABURU) ……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Awali,
kamati ilipokea mapingamizi mawili dhidi ya Muwekewa Pingamizi toka kwa
Bw. Hafidh Bashir na Bw. Arthur Mwambeta, lakini katika mchakato wa
kusikiliza, Bw. Hafidh Bashir, aliamua kuondoa pingamizi hilo. Kwa
mujibu wa maamuzi hayo tuna Muweka Pingamizi mmoja, tajwa hapo juu. Hoja
za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati ya
Mwaka 2010-2013 alishindwa kuwasilisha Audited Accounts kwenye Mkutano
Mkuu wa Simba, kwa mujibu wa ibara ya 19 (6), (7), 30 (1) (f) na 33 (5)
ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii. Muwekewa
Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya Simba kati ya Mwaka
2010-2013 alishindwa kujaza nafasi ya Mjumbe wa kamati ya Utendaji
(Mwanamke) iliyowazi kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba
ya Simba ya Mwaka 2010.
iii. Muwekewa Pingamizi,
akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba Sports Club ya Mwaka 2005,
aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na maagizo ya Baraza la Wazee
na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6 (1) (iii) ya Simba.
Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja
zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya
utendaji ya Simba Sports Club na Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005.
Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi
haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya
utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu,
hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi binafsi na kama
Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio
kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Geofrey Nyange (Kaburu) limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
SAID ALI MANERO ………………………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
EVANS ELIEZA AVEVA ………….……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati
ilipokea mapingamizi dhidi ya Muwekewa Pingamizi, toka kwa Muweka
Pingamizi hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i.
Muwekewa Pingamizi, aliwahi kugombea uchaguzi wa DRFA
mwaka 2013 kwa jina la Evans Aveva lakini katika vyeti vyake anatumia
jina la Evans Eliyeza, hivyo anaweza kuwa mtu tofauti, elimu ikwa
haikidhi matakwa ya Katiba na uraia wake kutiliwa shaka, hivyo kuiuka
ibara ya 26 (1) (2) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya Muda ya Simba
Sports Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club kinyume na
maagizo ya Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya 6
(1) (iii) ya Simba.
Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hati
ya kusafiria ya Muwekewa Pingamizi namba AB 047458 iliyotolewa tarehe
26/08/2006 inamajina: Evans Elieza Aveva, hivyo hakuna utata wowote
dhidi ya jina la mgombea. Muweka Pingamizi ameshindwa kuleta Ushahidi
wowote kuhusu mashaka yake katika elimu, uanachama au uraia wa muwekewa
pingamizi, hivyo basi hoja yake ya awali katika pingamizi hili inakosa
miguu ya kikanuni na kutupiliwa mbali.
Hoja ya
pili ya pingamizi hapo juu inahusu tuhuma dhidi ya Kamati ya Muda ya
Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi.
Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya
kamati ya muda ya Simba ya Mwaka 2005 kwasababu zifuatazo.
Mosi,
Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005, ambayo hivi sasa haipo, sio
Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Pili,
hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi Binafsi na kama
Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio
kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Evans Elieza Aveva limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE ………………………………………………..………… Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati
ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka
Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji
ya Simba walifanya maamuzi ya kumpindua Mwenyekiti wa Simba Sports Club
kinyume na ibara ya 33 (3) (a) (b) (c) na (d) ya katiba ya Simba ya
Mwaka 2010.
ii. Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu
ya Kamati ya Utendaji ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi
ndani ya siku 90 kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya
Simba ya Mwaka 2010.
Muweka Pingamizi hakutokea
bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa
pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa
maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi
hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports
Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi ya kamati ya
utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo
basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI
MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
JAMHURI MUSSA KIHWELO……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE ………………………………………………..………… Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati
ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka kwa Muweka
Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni kama ifuatavyo:
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji
ya Simba walifanya kikao haramu kinyume na ibara ya 33 (4) ya katiba ya
Simba ya Mwaka 2010 na kufanya mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti.
ii.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji ya
Simba walipitisha maamuzi batili ya kuwafukuza walimu wa mpira bila
malipo na mamlaka hivyo kusababisha usumbufu mkubwa hadi leo.
Muweka
Pingamizi alitoa maelezo yake na wawekewa pingamizi walijibu hoja hizo.
Kamati ilisikiliza hoja na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na
hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja za
pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba
Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati
ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Aidha
kuhusu hoja ya Kufukuzwa Walimu wa mpira, kamati inamshauri muweka
pingamizi apeleke shauri hilo katika Kamati ya Sheria ya TFF au Mahakama
ya kazi kwasababu ni suala la mwajiri na mwajiriwa.
Hivyo
basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo juu; SWEDI
MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali na yale yanayohusu maadili yaenda katika kamati husika.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
SWEDI MKWABI………………………………………………………… Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Muweka Pingamizi aliondoa pingamizi lake. Hivyo kamati haikusikiliza pingamizi hilo.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
LUKA NGWAKO MBAPILA……………………….………………..……….. } Waweka Pingamizi
OMAR JUMA MUNGA …………………………………………………………}
SALIM R. SIMBA ………………………………………………………………...}
ABDALLAH MKOVA ……………………………………………………………}
DHIDI
SWEDI MKWABI………………………………………………………… Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji
ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa
mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii.
Taarifa za mahesabu kwenye mkutano mkuu ziliwasilishwa kwa
lugha ya kiingereza hivyo kumnyima haki ya kujua mapato ya klabu kwa
miaka minne.
Waweka Pingamizi hawakutokea bila
sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa
pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa
maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi
hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports
Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati
ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..………..} Waweka Pingamizi
SWALEHE MADJAPA ……………………………………………………….}
DHIDI
KARAHA HASSAN CHANO (ALMAS)………………………………………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i.
Muwekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya Utendaji
ya Simba (Mhasibu Msaidizi) hakuleta taarifa za fedha katika Mkutano
Mkuu ambayo ilisababisha kuondolewa katika uchaguzi wa 2010 baada ya
kuwekewa pingamizi na Asha Kigundula na hajawahi kusamehewa na mkutano
mkuu wowote.
Waweka Pingamizi hakutokea bila
sababu yoyote, hata hivyo, Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa
pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa
maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi
hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports
Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya
Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati
ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
No comments:
Post a Comment