TANGAZO LA MDAHALO WA KATIBA
Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa
wazi kuhusu Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya.
Mdahalo huo utafanyika tarehe 31/5/2014 katika Ukumbi wa
Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi
saa 10.00 Jioni.
Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio
ya Dodoma, pamoja na Chuchu FM na Istiqama Radio
za Zanzibar.
Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza Mdahalo
huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.
Watoa Mada ni waliokuwa
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba:
Prof. Mwesiga Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.
Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania
inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya Watanzania.
Wote Mnakaribishwa!!!
No comments:
Post a Comment