Rekodi tatu za dunia zimevunjwa katika mbio za matimko na kupokezana vijiti.
Rekodi ya mbio za mita 1500 ya wanawake
ilivunjwa na wakenya Mercy Cherono, Faith Kipyegon, Irene Jelagat na
Hellen Obiri walipotumia muda wa dakika 16:33.58 zaidi ya sekunde 32
ndani ya rekodi ya awali.Timu ya wanaume ya wa Kenya nao hawakuwachwa nyuma walisajili muda bora wa dakika 14:22.22 .
Timu hiyo iliyojumuisha Collins Cheboi, Silas Kiplagat, James Magut na Asbel Kiprop
Ethiopia ilimaliza katika nafasi ya pili ikiongozwa Aman wote ambao waliandikisha muda wa dakika 14:41.22 .
Licha ya kushindwa matokeo hayo yaliipa Ethiopia rekodi mpya ya kitaifa.
Marekani ilifunga orodha ya tatu bora ikiongozwa na Leonel Manzan ambaye aliandikisha rekodi mpya ya kitaifa ya dakika 14:40.80.
Rekodi Nyengine iliyowekwa ni mbio za mita 200 kupokezana vijiti ambapo wajamaica
Nickel Ashmeade, Warren Weir, Jermaine Brown na Yohan Blake .
Wanne hao waliandikisha muda wa dakika moja 1:18.63.
Rekodi ya awali ya dakika 1:18:68 iliwekwa na Marekani miaka 20 iliyopita .
Shirikisho la riadha duniani IAAF liliwatuza washindi wote wa rekodi mpya dola elfu hamsini kwa juhudi zao.
CHANZO: BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment