CHANZO FULL
SHANGWE
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Friday, 30 May 2014
MIGOGORO YA ARDHI YAWA KERO KUBWA MKOANI MANYARA, KINANA AAHIDI KUFUATILIA SUALA HILO
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vikundi vya ngoma wakati alipowasili katika kata ya Gallapo kijiji cha Ayamango jimbo la Babati vijijini akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, Huku akiimarisha uhai wa chama cha mapinduzi. Katika ziara hiyo Kero kubwa iliyochukua nafasi ni ya migogoro ya ardhi ambapo kumekuwepo na uvamizi wa maeneo mbalimbali aidha ya wakulima au wafugaji ama hifadhi, Jambo ambalo limemfanya Katibu huyo Ndugu Abdulrahman Kinana kuwaambia wananchi hao kwamba atahakikisha anafuatilia suala hilo na kulifikisha kwa Rais Jakaya Kikwete ili aweze kuona ni kwa jinsi gani litatatuliwa kwani yeye ndiyo mwenye mamlaka ya kufuta hati za umiliki wa ardhi kwa mtu au taasisi yoyote. Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali katika mkoa wa manyara.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BABATI -MANYARA)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amezingirwa katikati na kikundi cha ngoma wakati akipokelewa alipowasili katika eneo la mkutano uliofanyika katika kijiji cha Amayango kata ya Gallapo.Akina mama wakipiga ngoma wakati wa mapokezi hayo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Manyara wakiwasili katika eneo la mkutano uliofanyika kijiji cha Ayamango.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwa amevalia vazil rasmi la kimila la heshima ya wazee wa kijiji cha Amayango.Wasichana wakiwa wamevalia mavazi ya kiasili.Baadhi ya kompyuta zilizokabidhiwa kwa shule mbalimbali na mbunge wa jimbo la Babati vijijini Mh. Jitu Son wakati wa mkutano huo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa meza kuu pamoja na viongozi wa mkoa wa manyara.Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo.Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo uliofanyika katika kijiji cha Amayango kata ya Gallapo.Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali wakiendelea na kazi yako ya kuchukua matukio katika mkutano huo.Mmoja wa wanavijiji waliofika katika mkutano huo Bw.Sumi Mtuka kutoka kata ya Kashi Babati akitoa kero zake mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Naye Bi.Elizaberth Manda mkazi wa kata ya Gallapo akitoa kero zake katika suala zima la ardhi ambalo limekuwa ajenda kubwa katika ziara hiyo hasa kwa wakulima na wafugaji.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mhandisi wa maji Babati Injinia Emmanuel Konkomo ambaye alitakiwa kueleza sababu za idaya ya maji katika wilaya hiyo kuchukua mradi wa maji ulioanzishwa na wananchi katika kata ya Gallapo na kuanza kuwatoza gharama kubwa za malipo ya bili za maji bila hata ya kukubaliana nao jambo ambalo limelalamikiwa na wananchi hao.Mhandisi wa maji Babati Injinia Emmanuel Konkomo akijaribu kutoa maelezo kwa wananchi ambao walionekana kutomwelewa na kukubali maelezo yake kutokana na suala hilo kuchukua muda mrefu bila kutatuliwa.Baadhi ya wamjengo ya chuo cha walimu wa Sayansi kilichojengwa katika kijiji cha Mamire.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na viongozi wa taasisi ya Rotary Club ya Babati ambayo imechangia kiasi cha shilingi milioni 50.000 katika ujenzi huo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mbunge wa jimbo la Babati vijijini Mh. Jitu Son wakati alipokagua ujenzi wa chuo hicho.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Amayango.Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano huo uliofanyika kijiji cha Amayango.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment