Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 27 May 2014

MEYA ARUSHA ALIA NA WATOTO WANAOPANGIWA MBALI NA SHULE ZAO


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

MEYA wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo amewashauri wataalamu wa sekta ya elimu hususani maafisa elimu wa jiji hilo kuanza kuangalia upya namna ya kuwasaidia wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kwa kuwapanga katika shule ambazo zipo karibu nao kwani kwa sasa wanafunzi wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya ishirini kwa ajili ya kutafuta masomo.
Lyimo alitoa wito huo juzi wakati akiongea kwenye baraza la madiwani wa jiji ambapo alidai kuwa anakutana na wakati mgumu sana wa wanafunzi.
Alisema kwamba endapo kama baraza hilo litaridhia kwa kauli moja kuwa wanafunzi wasipangiwe umbali mrefu sana basi wataweza kuwasaidia wanafunzi kuondokana na adha ambazo wanazipata kwa sasa.
Alisema adha hizo ni pamoja nakuwa mzigo mkubwa sana kwenye familia zao kwani wakati mwingine wanalazimika kutumia kiasi kikubwa cha nauli wakati hawana uwezo wa nauli hizo.
Adha nyingine ambayo ameitaja ni pamoja na kuchelewa  kwa wanafunzi hao kuweza kufika shuleni hali ambayo nayo wakati mwingine inasababisha madhara kwa kuwa wanakosa vipindi vya asubuhi.
"Madiwani  wenzangu ninyi ni mashaidi jinsi ambavyo watoto wa Arusha wanavyoteseka barabarani kwa ajili ya usafiri na jinsi ambavyo wanatumia muda mwingi kwa ajili ya kwenda shule nashauri kuwa basi sisi kwa sisi tunapaswa kuliangalia hili ili hawa wanafunzi wa darasa la saba ambao wanamaliza mwakahuu wasikumbane na hali hii tena inachoshwa sana wanafunzi lakini pia hata wazazi na walezi," aliongeza Lyimo.
Wakati huo huo, Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya  Doita alisema kuwa pamoja nakuwa Jiji linajitaidi kuweka bajeti kubwa kwa ajili ya elimu lakini bado vipaumbele havionekani .
Doita alitaja Vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuweza kujenga shule za hosteli kwa ajili ya wanafunzi wanaotokea mbali lakini pia hata kuweka mazingira mazuri ya hosteli hizo.
Akitolea mfano wa shule ya Kinana ambayo ipo chini ya uongozi wa Jiji alisema kuwa shule hiyo pamoja na kuwa imekuwa msaada mkubwa sana kwa wasichana lakini bado mazingira yake hayaridhishi hata kidogo.
Alimalizia kwakutaka uongozi wa idara ya elimu kujiwekea utaratibu wa kuweka uzio kwenye maeneo ambayo yanazunguka hosteli za wasichana lakini pia  kuongeza hosteli hizo ambazo kama zikiwa nyingi basi zitaweza kuokoa maisha ya watoto wa kike.

No comments:

Post a Comment