Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
Baraza la madiwani Jijila Arusha limetoa siku 30 za kukamatwa kwa aliyekuwa mganga mkuu wa Jiji Dk. Isack Ibrahimu kwa kosa la kutaifisha na kujimilikisha mali za hospitali ya Levolosi ambazo zilitolewa na wafadhili.
Agizo hilo linakuja mara baada ya baraza hilo kubaini kuwa mali ambazo zilikuwa zimetolewa na Hospitali ya KCMC pamoja na FHI hazikukabidhiwa kwa uongozi wa Jiji.
Pia mali hizo ambazo zilitumika kwenye mradi wa utafiti ambao ulikuwa unafanywa chini ya hospitali hiyo na FHI zilipaswa kukabidhiwa kwa uongozi wa Jiji mara baada ya kukamilika lakini daktari huyo alijichukulia mali hizo kama zakeAgizo hilo linakuja mara baada ya baraza hilo kubaini kuwa mali ambazo zilikuwa zimetolewa na Hospitali ya KCMC pamoja na FHI hazikukabidhiwa kwa uongozi wa Jiji.
No comments:
Post a Comment