Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha
ILI Tanzania iweze kuondokana na majanga mbalimbali ni lazima kwanza viongozi wa nchi, na madhehebu mbalimbali wahakikishe kuwa wanamrudia Mungu katika toba ili kuokoa nchi na laana.
Kwa sasa Tanzania inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya majaribu, na majanga na kutokana na hayo ni dalili kuwa kuna umuhimu wa nchi sasa kurudi mikononi mwa Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Samson Majaliwa ambaye ni Mkurugenzi wa Injili Jimbo la Kilimanajro (TEBE) kutoka EAGT wakati akiongea na waumini wa kanisa la EAGT Moria Mbauda mapema wiki hii.
Mchungaji Samson alisema kuwa ni vema na ni wakati wa mungu kutafutwa kwa nguvu zote na Watanzania pamoja na viongozi wa nchi kwani endapo kama hawataweza kufanya hivyo ni wazi kuwa majanga yatazidi kuongezeka maradufu.
Alisema, kama wananchi watakuwa na wokovu ni wazi kuwa wataweza majanga pamoja na majaribu ambayo kila siku yanaibuka kamwe hayatweza kuwasonga wananchi na badala yake wataweza kupiga hatua kubwa sana.
"Unajua watu wanashindwa kujua na kutambua kuwa kama haujasimama kwa mungu hata nchi uliyonayo itapigwa kama ilivyo kwenye hii nchi kwa sasa mambo ni mengi na wawimbi dhidi ya serikali nayo ni mengi sasa tusimame sisi kama viongozi lakini pia kama watu tunaomjua Mungu," aliongeza Mchungaji Samson.
Aliendelea kwa kusema kuwa wakristo wanapaswa kujua na kutambua kuwa wokovu sio gereza bali ni njia pekee ya kuweza kutatuliwa matatizo yako na ya nchi ambayo unaishi.
"kila shida uliyonayo tayari mungu anajua jinsi ya kutitatua wakumbuke paulo na sila walipokuwa gerezani je sisi kwanini tuogope wokovu na hata kama tunakumbwa na majaribu suluhisho kubwa hapo ni Mungu pekee," aliongeza Mchungaji Samson.
Pia aliwataka wakristo kuachana na tabia ya kuigiza wokovu kwani kwa njia ya kuigiza wokovu wakati mwinginen inasababisha wengi kuona kama wokovu ni gereza kubwa na hivyo kujikuta wakiwa wanaangukia katika majaribu mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment