Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 29 May 2014

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUFANYA UTAFITI

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspo,Arusha.

Wafanyabiashara nchini wametakiwa kufanya utafiti kabla ya kuanzisha biashara kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kujua changamoto za biashara husika na namna ya kuzikwepa ili kuwa na biashara endelevu inayohimili ushindani wa soko la biashara.

Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake,Mkurugenzi wa Kampuni ya Alpha Associate ltd iliyopo jijini hapa inayojishughulisha na masuala ya ushauri kwa Wafanyabiashara,Alphonce Massaga amesema kuwa biashara nyingi zimekuwa zikianzishwa na kushindwa kuwa endelevu kutokana na ukosefu wa utafiti.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa utafiti huo unamsaidia mfanyabiashara kuwajua wateja wake aidha ni wakubwa ama wadogo,kupanga bei ya bidhaa pamoja na kuwafahamu wapinzani na kuweka mikakati ya kuhimili ushindani.

 Massaga ameeleza kuwa utafiti huo unamsaidia mfanyabiashara kufanya maamuzi sahihi,kubaini maeneo yenye changamoto na kukwepa changamoto.

Amesema kuwa iwapo mfanyabiashara hatafanya utafiti wa eneo husika analolifanyia biashara anakua hatarini kupata hasara ama kufukuzwa na serikali kwa kufanya kazi maeneo yaliyokatazwa hivyo kujikuta akipata hasara na kubakia kulaumu.

Pia amewataka Wafanyabiashara kutafuta elimu ya biashara itakayowasaidia kufanya biashara kitaalamu na kupata faida badala ya kuhatarisha mitaji.

No comments:

Post a Comment