Kamishna wa Umoja wa Mataifa
anayesimamia Haki za Kibinadamu, Navi Pillay, amejiunga na maelfu ya
watu duniani wanaoshutumu vikali mauaji ya mwanamke Mpakistani
aliyepigwa mawe hadi kufa nje ya mahakama na wanachama wa familia yake
kwa madai ya kuolewa na mwanamume aliyempenda.
Mume wa mwanamke huyo - Mohammed Iqbal -
aliambia BBC kuwa alishtushwa na kukasirisha na maafisa wa polisi
waliokuwepo karibu na mahali palipotokea kitendo hicho lakini wakakosa
kufanya lo lote kunusuru maisha yake."Kilichotokea ni kibaya sana. Mmoja wa jamaa yangu alivua shati na kuwapungia maafisa wa polisi ili waweze kuingilia lakini wakapuuza. Walishuhudia kimyakimya tu Farzana akiuawa na wao hawakufanya lo lote," alisema Iqbal
Mamia ya wanawake huuliwa kila mwaka nchini Pakistan kwa kuolewa na watu wasiopendwa na familia zao, jambo ambalo halikubaliwi katika jamii nyingi ambazo hazipendelei maisha mamboleo yanayotambua watu kupendana kabla ya kuoana.
Makundi mbalimbali ya kupigania haki za kibinadamu kote duniani hutoa wito kwa Serikali ya Pakistan kuhakikisha kuwa wanaoshiriki mauaji kama haya wanashtakiwa; lakini juhudi zao zimeambulia patupu.
BBC
No comments:
Post a Comment