Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday 29 May 2014

SERIKALI YAOMBWA KUWAPATIA BIMA WATOTO


Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Arusha

SERIKALI  imeombwa kuwapatia Bima ya Afya watoto wanolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Samaritan Village, kilichoko Moshono, mkoani Arusha.
Mratibu wa kituo hicho, Father Josephat Mumany, akizungumza hivi karibuni wakati wakutoa taarifa fupi ya kituo hicho kwa viongozi na wanachama wa kikundi cha uamsho cha Oldadai, waliotembelea kituo hicho kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali, alisema bima hizo zitwapunguzia adha watoto hao wanapougua.
Alisema kutokana na watoto hao kutokuwa na Bima ya Afya,hali hiyo imekuwa ikiupa shida kubwa viongozi wa kituo hicho,pale unapopataka kuwapeleka watoto hao hospitalini.
Father Mmanyi,alisema hiyo ni changamoto kubwa kwao, kutokana na kituo kukabiliwa na  uhabawafedha, hali amabayo pia huwafanya watotowanaougua kukaa na maradhi yao kwa muda mrefu pasipo kupata matibabu.
Katika hatua nyingine, Mmanyi alisema watoto wanaolelewa katika kituo hicho wanapelekwa na serikali baada ya kuokotwa mitaani, kutokana na kutupwa na wazazi wao baada ya kujifungua.
''Watoto hawa wanaokotwa katika mazingira magumu wengine wanavunjwa miguu na wazazi wao, wengine wanakutwa wametoboleatobolewa na wazazi wao kabla ya kuwatupa, inasikitisha sana unapoona mazingira ambayo watoto hawa walikotoka,'' alisema.
Pamoja na serikali,aliitaka jamii na mashitika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa,kukisaidia kituo hicho kwa hali  na mali, ili kiweze kumudu malezi ya watoto hao.
Hivi sasa, alisema wana miradi waliyopewa na wahisani inayowasaidia katika mambo madogomadogo. Nayo ni pamoja na bwawa la samaki, shamba la mahindi, pamoja na migomba.
Mweka Hazina wa kikundi cha Uamsho, kilichowatembelea watoto hao,Be Marry Mayagila, alisema wanaguswa na mahitaji ya watoto hao na kwamba kwa kuwa wao ni wanawake wenye moyo wa huruma,ndiyo maana wameme amua kuwatembea na kuwapatia misaada ya vyakula.
Alitoa wito kwa wanawake,na vikundi mbalimbali kuwa hurumia watoto hao kwa kuwapa misaada mbalimbali kwani hawawajui wazzi wao,ili nao wajione swa na watoto wengine.

No comments:

Post a Comment