LEONARD AKIHOJIWA NA MWANDISHI NA MTANGAZAJI WA TBC BENNY MWAIPAJA |
LEONARD AKIWA NA WASHINDI WENGINE WA TUZO ZA TANAPA 2013, KATIKATI NI VEDASTO MSUNGU NA KULIA NI GERALD KITABU WA THE GUARDIAN |
MWANDISHI wa magazeeti ya serikali
(Dailynews na HabariLeo) mkoani Iringa, Frank Leonard ametwaa tuzo ya uandishi
bora wa habari za utalii wa ndani, mwaka 2013.
Leonard ambaye pia ni mmiliki wa mtandao
huu wa www.frankleonard.blogspot.com maarufu kama BONGO LEAKS amekuwa mshindi
wa pili kwa upande wa magazeti katika tuzo hizo zinazotolewa na Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Kwa ushindi huo amezawadia Sh Milioni
1.5, cheti na ziara katika hifadhi mbalimbali nchini.
Mshindi wa kwanza alikuwa Gelard Kitabu
wa The Guardian aliyejinyakulia Sh Milioni 2, ngao, cheti na atapata safari ya
kwenda nje ya nchi (moja kati ya nchi za SADC) kutembelea vivutio vya utalii.
Mshindi wa tatu kwa upande wa magazeti
alikuwa Jackson Kalindimya kutoka Nipashe ambaye alikabidhiwa hundi ya mfano ya
Sh Milioni moja na cheti.
Kwa upande wa redio mshindi wa kwanza
katika kipengele hicho cha utalii wa ndani alikuwa David Lwenyagira wa Redio 5
ya Arusha aliyepata Sh Milioni 2, ngao na ziara ya utalii katika moja ya nchi
za Sadc.
Mshindi wa pili alikuwa Humphrey Mgonja
wa Redio SAUT FM ya Mwanza aliyepata Sh Milioni 1.5, cheti na ziara katika
hifadhi mbalimbali hapa nchini; kutoka redioni hakukuwepo na mshindi wa tatu wa
habari bora za utalii wa ndani.
Waliobuka washindi wa habari za utalii wa
ndani kwa upande wa Televisheni ni Kakuru Msimu wa Star TV aliyekuwa mshindi wa
tatu na Kasim Mdame wa Channel Ten aliibuka mshindi wa pili huku nafasi ya
kwanza ikikosa mshindi.
Waaliobuka washindi kwa habari za
uhifadhi kwa upande wa magazeti ni Salome Kitomri wa Nipashe aaliyeibuka
mshindi wa tatu, huku nafasi ya pili na ya kwanza zikikosa washindi.
Kwa upande wa Televisheni, mshindi wa
kwanza alikuwa Vedasto Msungu wa ITV, wa pili Raymond Nyamwihura wa Star TV,
huku nafasi ya tatu ikikosa mshindi.
Baada ya washindi hao kukabidhiwa zawadi
hizo, wakiwa pamoja na wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo mbalimbali
vya habari Mei 28 walitembelea hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Saanane jijini
Mwanza.
BONGO LEAKS
No comments:
Post a Comment