Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
“Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia”,amesema Kinana.
CHANZO FULL
SHANGWE
No comments:
Post a Comment