Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 30 March 2016

SERIKALI KUSAIDIANA NA TAASISI YA MILLEN MAGESE MAPAMBANO DHIDI YA TATIZO LA ENDOMETRIOSIS

DSC_8548
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba yake katika semina hiyo. Kushoto ni Mwasisi wa Taasisi ya Millen Magese, Millen Happiness Magese. (Picha na Video na Andrew Chale,Modewjiblog).

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema kuwa ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mwanadada Millen Magese na Taasisi yake katika mapambano ya ugonjwa na athari za Endometriosis ambao unawapata wanawake wengi hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo Machi 30.2016 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla wakati wa kufungua rasmi semina maalum kwa vijana wapatao 500 wa shule za Sekondari zikiwemo za Turiani Sekondari, Makurumla na zinginezo za Manispaa ya Kinondoni pamoja na walezi na walimu, ambapo katika mkutano huo, Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, juhudi zinazofanywa na Mwanadada Millen Magese ni za kuungwa mkono hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.

SHULE YA AWALI YA SUNRISE YA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM YAWAFARIJI WATOTO YATIMA WA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA NA KUFANYA USAFI COCO BEACH


 Mkurugenzi wa Kituo cha Yatima na wale waliotoka katika mazingira magumu cha Watoto Wetu Tanzania (WWT), Evans Tegete akizungumza na wanahabari mwishoni mwa wiki wakati akipokea misaada mbalimbali kutoka Shule ya Awali ya Sunrise.

WAZIRI UMMY MWALIMU AWAKEMEA WANAOJICHUKULIA SHERIA KWA WATUMISHI WA AFYA

Ummy Mwalimu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kufuatia tukio la mmoja wa Madaktari kupigwa na mwananchi. Kulia ni Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akemea tabia inayotaka kujengeka ndani ya jamii ya kuwashambulia watumishi wa afya hasa Madaktari na Wauguzi.
Amevitaka vyombo ya dola kuwachukulia hatua wananchi wanaojihusisha na vitendo hivi ambavyo vitaathiri utoaji wa huduma za afya kwa wananchi hasa wa kipato cha chini.
Mhe Ummy amewasili Mtwara jana akiongozana na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Kambi ambapo alifanya mazungumzo na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.

WADAU WA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA WAKUTANA KUJADILI MPANGO KAMAMBE WA USAFIRI WA ANGA ( CIVIL AVITIATION MASTER PLAN) JIJINI DAR


Wadau wa sekta ya Usafiri wa anga nchini ,wamekutana katika warsha ya siku moja kujadili rasimu ya mpango kamambe wa usafiri wa anga  yaani ( the Civil Aviation Master Plan) makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini(TCAA), Banana-Ukonga.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAANZA VIKAO VYA MAPITIO YA RASIMU YA BAJETI YA WIZARA HIYO KWA MWAKA 2016/17

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Jeshi la Polisi pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi la Polisi. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI MKOANI KIGOMA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akisalimiana na wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa yanayohudumia wakimbizi katika Kambi ya muda ya NMC, iliyoko mkoani Kigoma, kushoto ni Mratibu wa Wakimbizi  Mkoani  Kigoma, Tonny  Samwel  Laiser.Naibu Waziri yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.

SERIKALI YAJIPANGA KUWASAIDIA WAKULIMA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI

DSC_1667
Wageni rasmi katika mkutano huo, Wa kwanza kushoto ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN), Njongenhle Nyoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai.

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhakikisha inawasaidia wakulima kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanaonekana kuendelea kuikabili nchi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Bi. Shakwaanande Natai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) na Taasisi ya Mtandao wa Kutathimini Sera za Chakula, Kilimo na Maliasili (FANRPAN) ili kujadili mpango wa Kilimo Salama (CSA).

JOH MAKINI NA G-NAKO NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA


Weusi @Joh Makini (L) & @Gnako Warawara (R) Wakiwa Rock City, Raha Yao ni Kusikiliza 102.5 Lake Fm, Radio Ya Wananzengo.
JE WEWE RAHA YAKO YA ROCK CITY NI NINI?
#‎Tune 102.5 LakeFm
‪#‎Raha Ya Rock City
‪#‎Radio Ya Wananzengo
Follow Facebook, Twitter & Instagram @lakefmmwanza

IZZO BUSINESS APAGAWISHA WAKAZI WA MBEYA KWENYE TAMASHA LA PASAKA

Msanii Emmanuel Simwinga maarufu “ Izzo Bizness “ akitumbuiza kwenye tamasha la pasaka la home sweet home lililodhaminiwa Tigo jijini Mbeya jumapili iliyopita.

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.

ASKOFU CHARLES GADI NA WACHUNGAJI WENZAKE WALIOMBEA TAIFA LIPATE MVUA

 Askofu  wa Kanisa la God News for all Ministry, Dk. Charles Gadi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhu kabla ya kuliombea taifa lipate mvua akiwa na wachungaji mbalimbali. Kulia ni Mchungaji Palemo Masawe.

RAIS DK.JOHN MAGUFULI ATOA HATI YA KIWANJA KWA BOHARI YA DAWA (MSD)

 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (kushoto), akimkabidhi hati ya kiwanja chenye ukubwa wa ekari tano Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu kilichotolewa na Rais Dk. John Magufuli kwa MSD kupitia Wizara hiyo Dar es Salaam.

SHUHUDIA EXCLUSIVE INTERVIEW YA VANESSA MDEE

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA BOHARI YA DAWA MSD JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, Peter Serukamba (kushoto), Wajumbe wa kamati hiyo na Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Banakunu (kulia), wakitembea wakati kamati hiyo ilipotembelea MSD Makao Makuu Keko Dar es Salaam.

WAZIRI MBARAWA AZITAKA TAASISI NA IDARA KUTUMIA KITUO CHA KUHIFADHI TAARIFA CHA TAARIFA

Mkuu wa Idara ya Mfumo wa Habari wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Khalfa Ally (kwanza kulia) akielezea namna Kituo cha Taifa cha Kuhifadhia Taarifa 'National Information Data Centre' kinavyofanya kazi kwa baadhi ya wawakilishi wa wakuu wa mashirika ya umma, taasisi binafsi, wizara na idara za Serikali leo jijini Dar es Salaam.

WASHINDI MBIO ZA MAGARI ZA VAISAKH RALLY 2016 WAKABIDHIWA ZAWADI

Mfanyabiashara Davis Mosha akiwa na mshindi wa kwanza katika mashindano ya Mbio za magari yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Moshi,Gurjit Dhan (kushoto) akiwa na msoma ramani wake Shameer Yusuf (kulia).

AZAM, YANGA DIMBANI ALAHAMISI

Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) linatarajiwa kuendelea Alhamisi kwa michezo miwili kuchezwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Azam FC watakua kwenye uwanja wa Azam Complex kuwakaribisha maafande wa Tanzania Prisons siku ya Alhamis saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

SERENGETI BOYS KUJIPIMA NA MISRI

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya Misri Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (The Pharaohs) jijini Dar es salaam.
Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys dhidi ya The Pharaohs utachezwa siku ya Jumamosi, Aprili 2 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku mchezo wa pili ukichezwa Jumanne Aprili 5 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

JAMII IWE MAKINI NA MATANGAZO YA NAMNA HII

Na:George Binagi @BMG
Hili ni miongoni mwa Matangazo yanayosambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii. Awali matangazo kama haya ikiwemo lile la Kujiunga na Freemason pamoja na watalaamu wa tiba asili yalizagaa pia mitaani na hata katika mitandao ya kijamii.

KWA NINI AGIZO LA AGP MANGU LINAPUUZWA?

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu.

Na:George Binagi @BMG
Kwa muda mrefu kumekuwepo na malalamiko kwamba waendesha bodaboda nchini wamekuwa hawatii sheria za usalama barabarani, hali ambayo imekuwa ikisababisha ongezeko la ajali zinazoweza kuzuilika.

Hali hiyo ilimsukuma Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu mwishoni mwa mwezi uliopita, kutangaza Oparesheni kamata bodaboda wasiotii sheria za usalama barabara nchini nzima katika kikao kazi kilichowahusisha Maofisa Wakuu wa Polisi nchini wakiwemo Makanda wa Polisi Mikoa, Vikosi na Makao Makuu, kilichofanyika Jijini Dar es salaam.

ACT WAZALENDO: UAMUZI WA MCC KUSITISHA UHUSIANO NA TANZANIA UTAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI


ACT WAZALENDO
     TAARIFA KWA UMMA
UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

1. CHAMA  cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.
2.MCC ni  Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya  kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Saturday 26 March 2016

USIKU WA MCHIRIKU NA TAARABU KUFANYIKA KESHO PASAKA DAR LIVE

DAR-LIVE

MUTFI WA TANZANIA AMUOMBEA DUA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA

 Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubery akiwa nyumbani kwake.

TAARIFA YA MSIBA WA ZEBEDAYO MAINGU MAFURU

Sky background. Sky and clouds background.Sky.
Zebedayo Maingu Mafuru enzi za uhai wake.

Ndugu Asheri Mafuru, anasikitika kutangaza kifo cha ZEBEDAYO MAINGU MAFURU wa KIBAMBA DAR ES SALAAM, KILICHOTOKEA KIBAMBA DAR ES SALAM ALFAJIRI YA TAR. 23/03/2016. 

Habari ziwafikie MAMA MZAZI RAHEL BISWALO WA KIBARA BUNDA, BABA MDOGO WA MAREHEMU GALIGWA MAFURU WA MRANGI MUSOMA, ONESMO NYABUGIKA WA MGANGO MUSOMA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE WALIPO. 

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KIBAMBA JIJINI DAR ES SALAAM. MAZISHI YATAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU JUMAMOSI TAREHE 26/03/2016. 

 BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Friday 25 March 2016

WAGOMBEA USPIKA BUNGE LAWAWAKILISHI ZANZIBAR WAMKATAA KIFICHO



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
HEKAHEKA zimeanza Visiwani Zanzibar ambapo wagombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Wawakilishi wameanza kupigana vikumbo kuwania nafasi hiyo huku sura mpya za vijana wenye damu mbichi zikijitokeza kuchuana na mkongwe aliyechukua tena fomu ya kutetea nafasi yake Mhe Pandu Ameri Kificho.

WAHOLANZI WAWILI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIA NA TUMBILI 61

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.

 Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .


VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu ,raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.

DAWASCO YATOA RAI ONGEZEKO LA MAJI JIJINI

Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imetangaza kuwako na ongezeko la Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam, pamoja na maeneo ya miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya mtambo wa Maji wa Ruvu chini kuanza kufanya majaribio ya uzalishaji wa Maji .

VIJANA WAANDAA MSAFARA WA HISANI KWA KUTUMIA MAGARI KUPINGA UJANGILI NA KUHAMASISHA UTALII WA NDANI

Mkurungezi mtendaji wa Bongo Ride Idrisa Magesa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea makamilisho ya maandalizi ya msafara wa hisani wa magari uliopewa jina Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) ambao utaambatana na kutembelea mbuga ya wanyama ya Tarangire Mkoani Arusha  ikiwa na lengo kupaza sauti kuhusu janga la ujangili na pia kuhamasisha utalii wa ndani,kulia kwake ni Meneja Mawasiliano wa BRCC Krantz Mwantepele na kushoto kwake ni Mkuu wa matukio Kelvin Edes,Pembeni yake ni Mkurungezi wa Teamtezza Kennan Richard.

KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI YATEMBELEA MSD

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (mwenye suti nyeusi kushoto), akiwatembeza Wajumbe wa  Kamati Bunge ya Mauala ya Ukimwi waliotembelea MSD Keko Dar es Salaam jana.

Thursday 24 March 2016

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA OFISI ZA WIZARA HIYO UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA KITUO CHA POLISI BUGURUNI

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisalimiana na maafisa wa Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara aliyoifanya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.  Katikati ni Mkuu wa wa Ofisi ya Uhamiaji katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Abuu Mvano.

STARS YAICHAPA CHAD 1- 0 N'DJAMENA

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager leo imeibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya wenyeji Chad katika mchezo uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Omnisport Idriss Mahamat Ouya uliopo jijini N’Djamena.
Kikosi cha Stars kilicheza vizuri kwa maelewano kwa lengo la kusaka bao la mapema, safu ya ushambuliaji ilikuwa mwiba kwa walinzi wa Chad katika dakika 30 za kipindi cha kwanza na kukosa nafasi zaidi ya nne za wazi kupitia kwa Ulimwengu, Farid, Samatta na Kazimoto.

BODABODA MKOANI MWANZA WARIDHIA KUANZISHWA KWA UMOJA WA KITAIFA WA BODABODA.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) akuzungumza katika Mkutano Mkuu Muhura wa Kwanza wa mwaka 2016 wa Umoja wa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Mwanza uliofanyika Jumamosi Machi 19,2016 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Pamba Jijini Mwanza. Kushoto kwake ni viongozi wa bodaboda Mkoa wa Mwanza.

BASATA LAONYA KUMBI, LAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO



PRESS RELEASE
24/03/2016


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.
Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.
HII HUKU...

Wednesday 23 March 2016

KAMPUNI YA MABIBO BEER YADHAMINI BONANZA LITAFANYIKA LEADERS CLUB JUMAMOSI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwonekano wa chupa ya bia ya Windhoek inayosambazwa hapa nchini na kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd.

UNDER HEAVY SECURITY, OBAMA TOUCHES DOWN IN ARGENTINA IN HISTORIC STATE VISIT

U.S. President Obama and First Lady Michelle Obama arrive with their daughters Sasha and Malia at Ministro Pistarini International Airport in Ezeiza, Argentina.
(Photo: JUAN MABROMATA, AFP/Getty Images)

Kamilia Lahrichi, USA TODAY
BUENOS AIRES — Following his historic visit to Cuba, President Obama and the first family arrived in Argentina early Wednesday for a two-day visit, his first trip to the country since he became president.
Obama, the first lady and their two daughters landed around 1 a.m. GMT (12 a.m. ET) in the capital, which has beefed up its security presence since the terrorist attacks that shook Brussels Tuesday morning. Authorities had shut down several streets and subway stops by midnight. Helicopters were seen flying in the sky, according to the national newspaper, Clarin.
“I consider the rapprochement between the two countries very positive and I would like that they keep having a good relation in the future regardless of who wins the upcoming elections,” said Sofi Romero, an Argentine.

OIL PRICE STUCK AS IEA BRANDS SUPPLY DEAL 'MEANINGLESS'


The oil price is stuck at around $40 a barrel and may even move lower in the next month or so as optimism in the market rests on a deal to freeze supplies that the global energy watchdog has warned could be "meaningless".

Since hitting multi-year lows early last month, oil has rallied by around 50 per cent. International benchmark Brent crude hit $27 a barrel on 11 February and has hit several new 2016 highs in the past two weeks, with the latest coming on Tuesday, when it peaked at just shy of $41.80. US benchmark West Texas Intermediate is also currently a little more than $41 a barrel.

MAREKEBISHO YA RATIBA YA VODACOM PREMIERSHIP


Utangulizi;
-Marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom yamezingatia mechi za viporo za timu za Azam na Yanga zinazoshiriki mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho).

-Pia ushiriki wa Azam na Yanga katika mechi zijazo za mtoano (play offs) zinazokutanisha timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na zile zilizosonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho.

TIGO YATOA 300M/- KUDHAMINI WANAFUNZI WA TEHAMA VYUO VIKUU

Meneja mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kutangaza udhamini wa kampuni hiyo kwa wanafunzi tisa wanaochukua mafunzo ya Tehama katika vyuo vikuu vya hapa wa jumla ya shilingi million 300 mapema leo  jijini Dar Es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula na kushoto ni Meneja wa huduma za Jamii Tigo, Woinde Shisael.

DAWASA YATOA DARASA KWA VIONGOZI WA JUMUIYA 15 ZA WATUMIA MAJI DAR ES SALAAM, KIBAHA NA BAGAMOYO

 Meneja Uhusiano wa Jamii wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es salaam (DAWASA) Bi.Neli Msuya akizungumza na viongozi wa Jumuiya 15 za Watumia Maji zilizojengwa chini ya mradi wa Maji Yetu uliofadhiliwa na Serikali ya Ubelgiji uliogharimu shilingi Bilioni 14.5 alipokutana nao leo jijini Dar es salaam.

CCM YAMPONGEZA DK. SHEIN KWA USHINDI MNONO


MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU CHINI YA UNESCO YAZINDULIWA CHUO KIKUU HURIA, DAR

Faith Shayo - Unesco, Tanzania
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT), Prof. Elifas Bisanda (hayupo pichani) kufungua rasmi mafunzo ya Tehama kwa walimu nchini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

MAFUNZO kwa walimu watakaotumia teknolojia ya mawasiliano na habari (Tehama) kufundisha masomo ya sayansi ikiwamo hesabu yamefunguliwa katika maabara za Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.

Tuesday 22 March 2016

MARUFUKU KUCHEZA MICHEZO YA KUBAHATISHA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inapenda kuwakumbusha wanafamilia wa mpira wa miguu juu ya ibara ya 59 kifungu kidogo cha 11 kinachotamka:
"TFF Family members shall at all times comply with the following ethical principles "To not take part in betting connected with football and do not tolerate any form of manipulation or unlawful influencing of match results".

STARS KAMILI KUWAVAA CHAD KESHO


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimekamilika baada ya kundi la pili lenye wachezaji nane kuwasili leo mchana nchini Chad tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya wenyeji kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017.

TIGO YATOA MSAADA WA MADAWATI 500 KWA SHULE ZA MSINGI DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda akihutubia wananchi na wanafunzi katika makabadhiano wa msaada wa madawati 500 yenye thamani ya shilingi milioni 82.5 kwenye shule kumi za msingi katika mkoa wa Dar es Salaam. 
Sherehe ya makabidhiano ilifanyika shule ya msingi Kawawa iliyopo Kigogo Luhanga.

MSUKUMA: TAMASHA LA PASAKA LIPIGIE VITA MAUAJI YA VIKONGWE, ALBINO

Joseph Kasheku 'Msukuma'

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE  wa Geita vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kasheku Musukuma amewahi kutamka bungeni kuwa vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wanauawa wanne kwa wiki kitu ambacho ni kibaya na sio cha kibinaadamu.