Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Said
Meck Sadiki kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Dkt. Rehema Nchimbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Said Thabit Mwambungu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma leo
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Magesa Mulongo kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Mara katika hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe.
Amina Juma Masenza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa leo Ikulu jijini Dar
es salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Halima Omary Dendegu kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Jordan Mungire Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akimwapisha Kamishna
Mstaafu wa Polisi Zerote Steven kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa leo Ikulu jijini Dar es
salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Dar es salaam leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Muhuga kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Katavi.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Ikulu
jijini Dar es salaam leo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Bw. Alphayo Kidata kuwa Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakiimba wimbo
wa Taifa kabala ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo
Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya wa Tanzania Bara
walioapishwa leo wakiwa katika picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakila kiapo
cha kuzingatia maadili ya viongozi wa umma katika kutekeleza majukumu yao leo Ikulu
jijini Dar es salaam.
Wakuu wa Mikoa wapya walioapishwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakisaini hati
za viapo vya maadili ya viongozi wa umma mara baada ya kuapishwa leo Ikulu
jijini Dar es salaam.Picha/Eleuteri Mangi na Aron Msigwa.
Na
Jacquiline Mrisho- Dar es salaam.
Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapa siku
15 Wakuu wa Mikoa kuwaondoa watumishi hewa walio katika orodha ya malipo ya
mishahara ya watumishi wa umma katika Mikoa yao.
Rais
Dkt. Magufuli amesema hayo leo Ikulu Jijini Dar es salaam baada ya kuwaapisha Wakuu
wa Mikoa aliowateua Machi 13 mwaka huu ambapo amewaagiza washirikiane na
Wakurugenzi wa Halmashauri kuwaondoa watumishi hewa.
“Nimewapa
siku 15 kuanzia leo mkashirikiane na Wakurugenzi wa Halmashauri zenu kuwatoa
wafanyakazi hewa, nikigundua kuwa bado kuna wafanyakazi hewa, Mkurugenzi husika
atafukuzwa kazi na atapelekwa mahakamani”,
Na
kusisitiza “Nimeamua kuwachagua nikiamini kwamba mtaniwakilisha vizuri katika
Mikoa yenu, nawaomba mkatimize majukumu yenu bila kuogopa” alisema Dkt.
Magufuli.
Aidha,
Mhe. Dkt. Magufuli amesikitishwa na
utafiti wa watumishi uliofanywa katika Mikoa ya Singida na Dodoma ambapo imegundulika
watumishi 202 wanalipwa mishahara hewa.
Wakati
wa utafiti huo, zaidi ya watumishi 26,900
walioko katika Halmashauri 14 za Mikoa hiyo, watumishi 3,320 hawakuwepo kazini
kwa sababu mbalimbali.
Kwa
mantiki hiyo, ukichukua utafiti huo wa Mikoa miwili ni dhahiri Serikali
inapoteza mapato mengi kwa kulipa mishahara ya watumishi hewa nchi nzima.
Vivyo
hivyo, Mhe. Dkt. Magufuli amewasisitiza Wakuu wote wa Mikoa wakasimamie ilani
ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwakuwa waliahidi kutatua kero za
wananchi na wahakikishe wanazitatua ili wananchi waishi vizuri kwa amani ndani
ya nchi yao.
Naye
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakurugenzi
wa Majiji na Halmashauri zote nchini wajiandae kupokea na kuzipangia matumizi
shilingi milioni 50 za kila Kijiji zilizoahidiwa wakati wa kampeni kwa lengo la
kuboresha na kuimarisha shughuli za maendeleo.
No comments:
Post a Comment