Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akisalimiana na viongozi wa dini wakati alipowasili katika kambi ya Rumasi-Lukole
iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera,kambi
hiyo hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae
hupelekwa katika makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo
mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Kikundi cha ngoma za kitamaduni
cha Umoja, wakicheza ngoma wakati Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa alipowasili
katika kambi ya Rumasi-Lukole iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera, kambi hiyo
hutumika kupokea wakimbizi wanaotoka nchini Burundi ambapo baadae hupelekwa katika
makambi ya Nyarugusu yaliyopo mkoani Kigoma.Waziri Mkuu yupo mkoani Kagera kwa
ziara ya kikazi.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma
kwa Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi,Harrison Mseke, akisoma taarifa ya kambi ya Rumasi-Lukole
mbele ya Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu kambini
hapo kukagua kambi hiyo na kuongea na raia wa Tanzania na wakimbizi wa Burundi
wanaoishi kambini hapo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni,akizungumza na wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Rumasi-Lukole(hawapo
pichani),wakati ya ziara aliyoongozana na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa.Kambi
hiyo iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kagera hupokea wakimbizi kutoka nchi ya
Burundi kabla ya kuwapeleka kwenye makambi ya wakimbizi ya Nyarugusu,mkoani
Kigoma.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,akizungumza
na raia wa Tanzania pamoja na wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya
Rumasi-Lukole(hawapo pichani), Waziri Mkuu alitembelea kambi hiyo iliyopo
wilayani Ngara,mkoani Kagera na kuwaasa
wakimbizi hao kuishi kwa kufuata sheria za nchi pasipo kuvunja amani iliyopo
nchini.
Raia wa Tanzania pamoja na
wakimbizi kutoka nchi ya Burundi, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa(hayupo pichani),wakati wa mkutano aliozungumza nao katika kambi ya
wakimbizi ya Rumasi-Lukole,iliyopo wilayani Ngara,mkoani Kigoma.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa(wa
tatu kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Wakimbizi,iliyopo
chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Harrison Mseke (wapili kulia),wakati
akielekea kukagua mabweni wanayolala wakimbizi kutoka Burundi katika kambi ya
Rumasi-Lukole,iliyoko wilayani Ngara,mkoani Kagera.Wa kwanza kushoto ni Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Dk.Medard Kalemani , wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni mwakilishi wa
Shirika la kuhudumia wakimbizi Duniani(UNHCR),Gerald Ndabimala.
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa,akikagua
mabweni wanayolala wakimbizi kutoka nchini Burundi katika kambi ya Rumasi-Lukole inayotumika kupokelea wakimbizi
hao.Kambi hiyo iko wilayani Ngara,mkoani Kagera.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara
ya Huduma za Wakimbizi,iliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi,Harrison Mseke.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
No comments:
Post a Comment