Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Kassim
Majaliwa,akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa mama wa Mbunge
wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, alipofika kutoa pole kwa
wafiwa.Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk. Medard Kalemani na
anayefuatia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad
Masauni ,ambao waliongozana na Waziri Mkuu kwenda kutoa pole kwa wafiwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba
Kusini,Profesa Anna Tibaijuka,ambaye amefiwa na mama yake.Waziri Mkuu yuko
mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba
Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, aliyefiwa na mama yake,marehemu Aurelia
Kajumulo.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment