Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 22 March 2016

MSUKUMA: TAMASHA LA PASAKA LIPIGIE VITA MAUAJI YA VIKONGWE, ALBINO

Joseph Kasheku 'Msukuma'

Na Mwandishi Wetu
MBUNGE  wa Geita vijijini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kasheku Musukuma amewahi kutamka bungeni kuwa vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wanauawa wanne kwa wiki kitu ambacho ni kibaya na sio cha kibinaadamu.
Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na kampuni ya Msama kutambua umuhimu wake wana kila sababu ya kuwaunga mkono  na angependa kuona wananchi wanajitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili kuzungumza na Mungu kupitia waimbaji na viongozi wa dini katika tamasha hilo litakalofanyika mikoa ya Kanda ya ziwa.
Alisema hiyo ni kama dawa ambayo imekuja kutibu tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe hivyo  anaamini kuwa  nguvu za Tamasha hilo wataweza kusonga mbele.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Alex Msama alisema tamasha hilo litafanyika mkoani Geita kuanzia Machi 26 kwenye ukumbi wa Desire, Machi 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba na Machi 28 litafanyika uwanja wa Taifa wilayani Kahama.
Waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment