Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 15 April 2014

ETI PENZI LA MAMA MKWE TAMU KULIKO LA MKEWE! DUNIA KWELI INA MAMBO, SIKIA KISA HIKI


Kuishi kwingi ni kuona mengi. Unaweza kusema dunia imekwisha. La Hasha! Wanadamu ndio wamebadilika, wamekuwa kama wanyama. Hata wanyama wengine wana staha na wanatushangaa sisi binadamu kwa mambo tunayoyafanya.
Siku hizi ni jambo la kawaida kusikia baba fulani anajivinjari na bintiye. Wapo wale wanaowabaka binti zao wadogo, lakini pia wapo wale ambao hata binti wenyewe wanafurahia kuvunja Amri ya Sita na baba zao. Usibishe. Wapo na wanafurahia mno, tena wanawaita 'Baby'? Eti baba yako mzazi unamwita 'baby', unachojoa nguo naye anachojoa. Duh! Laana.
Tulimsikia yule kijana kule Songea ambaye aliamua kuwaacha wake zake watatu baada ya kukolea na penzi la mama yake mzazi. Mama alipoulizwa katika kipindi cha 'Mimi na Tanzania' kinachoendeshwa na dada yangu Hoyce Temu, naye bila soni akasema mahaba yamekolea.
Sasa sikia kisa hiki kilichotokea huko Kenya, ambapo mwanamama mmoja analalamika kwamba mama yake mzazi ndiye aliyempora mume.
Akawafuma siku ya Jumapili wakivinjari bila aibu kwenye kitanda chake (matrimonial bed). Mumewe akamwambia hadharani kwamba ati yeye hayuko sex kama mama yake. Bila aibu, mama naye akaendelea 'kucheza sebene' kitandani mwa bintiye huku bintiye na wajukuu zake wakiangalia. Sikiliza mwenyewe. Inasikitisha na kuhuzunisha sana.

No comments:

Post a Comment