Msemaji
wa kundi hilo ameiambia BBC kwamba mwanamme huyo anayeaminika kuwa raia wa Sweden-aliachiliwa
huru kwa misingi ya kiafya.
Mwangalizi
huyo kutoka Sweden anayeaminika kuugua ugonjwa wa kisukari alionekana
akisafirishwa kwa gari la Shirika la usalama na ushirikiano la mataifa ya Ulaya
OSCE .
Lakini
wenzake saba bado wanazuiliwa huku juhudi za kidplomasia kujaribu kuwakomboa
zikiendelea.
Awali
waangalizi hao walionyeshwa kupitia vyombo vya habari vya habari
.
Mmoja
wao ambaye ni Kanali kutoka Ujerumani , Axel Schneider, amesema waangalizi hao
walikua katika harakati za kidiplomasia na hawakuwa na silaha.
Shirila hilo la OSCE lina kundi
kubwa la waangalizi nchini Ukraine ambao walikubaliwa na Urusi, lakini
waangalizi hawa ni kutoka nchi kadhaa za shirika hilo waliokwenda nchini
Ukraine kwa mwaliko wa serikali.
CHANZO, BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment