Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday 28 April 2014

TIMU 72 KUSHIRIKI ESTER CUP 2014, BINGWA KUIBUKA NA MILIONI 1.5

IMG_3347
Mbunge wa Viti  Maalum kwa vijana kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ester Bulaya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Ester Cup yatakayofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba na uwanja wa Shule ya Msingi Bunda. (Picha na Mpigapicha wetu)


Na Mwandishi Wetu

Jumla ya timu 72 zitashiriki katika mashindano ya soka ya Ester Cup ambayo huandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, kwa tiketi ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ester Bulaya.

Mashindano hayo, yanafanyika mwaka huu kwa msimu wa nne katika Jimbo la Bunda, na yatachukua nafasi katika viwanja vya Sabasaba, Shule ya Msingi Bunda, Nyamswa na Mgeta.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana (leo), Bulaya alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa kulinganisha na miaka ya nyuma.

Alisema kuwa mwaka 2011 jumla ya timu 18 zilishiriki, mwaka 2012 timu 26 wakati mwaka jana ziliongezeka mpaka 38.

Bulaya alisema, ameamua kuendeleza mashindano hayo ili iwe fursa ya ajira kwa vijana wenye vipaji vya soka.
“Mimi ni mzaliwa wa Bunda na moja ya changamoto za jimbo letu ni kutokuwa na mashindano ya soka, nilipoanzisha mashindano ya Ester Cup nilileta kuhamasisha michezo jimboni kwetu, nafurahi kwa sasa lengo limetimia na hamasa katika jimbo hilo imeongezeka,” alisema Bulaya.

Alisema, tangu kuanza kwa mashindano, wilaya ya Jimbo la Bunda na wilaya nzima ya Bunda, imepata mafanikio makubwa na wachezaji wengi wamepata ajira kwenye klabu mbalimbali kubwa zinazoshiriki michuano mikubwa nchini.

Alifafanua kuwa ili kuleta maendeleo katika michuano hiyo, wamezuia wachezaji nje ya jimbo la Bunda kucheza Ester Cup jambo ambalo halitasaidia malengo yetu ya kuendeleza michezo kwa vijana wa jimbo husika.

Bulaya alisema kuwa jumla ya Sh15.4 zimetumika kugharimia mashindano ya mwaka  ambapo mshindi atapata Sh 1.5 million ambapo mshindi wa pili atazawadiwa Sh700,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Sh 500,000.

Aliongeza kuwa pia amefanikiwa kugawa vifaa mbali mbali kwa wilaya nne na kata 150 za wilaya nne, shule za sekondari na kutumia jumla ya Sh 75 million. Alisema kuwa wilaya ya Rorya na Tarime pekee ndizo hazijapata msaada huo na yupo mbioni kuwakabidhi.

CHANZO, MPENJABLOG

No comments:

Post a Comment